Rais Samia atengue kauli yake ya yeye na Magufuli ni wamoja, au aombe radhi kwa madhila yaliyowapata baadhi ya watanzania kwenye awamu ya 5

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
15,564
21,371
Baada tu ya kuingia madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema kuwa yeye na Magufuli ni wamoja.

Sijui kama wakati ule au hata wakati huu Rais anafahamu uzito wa maneno hayo. Kusema kuwa ni mmoja na mtu mwingine kunaweza kumaanisha mengi ila kwa uchache katika hili kunaweza kumaanisha kuwa Samia anaunga mkono yote aliyoyakubali na kuyatenda hayati Magufuli.

Tunaelewa utata na controversy zilizokuwapo katika utawala wa Magufuli ambapo tulishuhudia uvunjwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu ikiwa ni pamoja na kupokwa kwa demokrasia na uhuru wa kujieleza.

Rais Samia anawajibika mbele ya umma kueleza msimamo wake kuhusiana na kauli yake hiyo ya kwamba yeye na Magufuli ni wamoja. Je, anaunga mkono upokaji wa demokrasia na mengine mabaya tuliyoshuhudia wakati wa Magufuli?

Je, si vyema kwa rais Samia kuomba msamaha kwa yote mabaya aliyofanya mtangulizi wake kama kweli yeye na mtangulizi wake ni wamoja?
 
Kuna tofauti ya "we are same" and "we are one" wana sheria saidieni huyu atofautishe hayo maneno.
 
Back
Top Bottom