Rais Samia ashiriki Halfa ya Utoaji Tuzo za Wasanii wa Uchekeshaji Tanzania. Na kupewa tuzo ya Champion of Comedy

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,934
13,689
Rais Samia akishiriki Halfa ya Utoaji Tuzo za Wasanii wa Uchekeshaji Tanzania Ukumbi wa The Super Dome Februari 22, Dar es Salaam.

Pia soma: Pre GE2025 - Rais Samia kuwa mgeni rasmi wa kwenye tuzo za Tanzania Comedy Awards

Updates....
- Rais Samia apewa tuzo ya Champion of Comedy; nami nasema anafaa

-Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameshinda tuzo ya Kiongozi Mcheshi katika Usiku wa Tuzo za Ucheshi (TCA) Zilizofanyika katika Ukumbi wa Super Dome Jijini Dar es salaam.

Katika Kinyanganyiro hicho Makongoro alikuwa akichuana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, Mchingaji Hananja, Mkuu wa Mkoa Mstaafu Aggrey Mwanri na Sheikh Kipozeo.

-Wachekeshaji Steve Mweusi na Ndaro wameibuka washindi katika kipengele cha Best Comedy Duo katika tuzo za wachekeshaji Tanzania.

-Mchekeshaji maarufu Bongo, TX Dullah ameibuka mshindi katika kipengele cha Best Male Digital Comedian of The Year (Mchekeshaji Bora wa Kiume wa Kidijitali wa Mwaka) katika Tuzo za Wachekeshaji Bongo.

-Leonardo ameibuka Mshindi wa Jumla akinyakua Tuzo kubwa ya Overall best comedian of the year kwa wanaume na wanawake.

-Mama Mawigia ameshinda Tuzo ya Best Female Digital Comedy of the Year leo Februari 22, 2025 jijini Dar es Salaam.

-Msanii wa Muziki, Omary Nyembo maarufu Ommy Dimpoz amesema kuanzia siku ya leo Februari 22, 2025, wachekeshaji (comedians) wa Tanzania, hashtag yao ni "Cheka na Samia" na popote alipo Rais Samia Suluhu Hassan nao wapo!

"Kwa hiyo, sisi wenyewe kwa kufurahi na kufurahishwa na uwepo wa Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan), leo tukasema kuanzia leo tutaita wachekeshaji wote kuhakikishia kwamba tunamsapoti Rais na tutaenda kama 'Cheka na Samia'.

- Eliud Samwel amenyakua tuzo ya mchekeshaji bora wa jukwaani maarufu kama Stand Up Comedy.

- Lucas Mhuvile, maarufu kama Joti, ameshinda tuzo ya The Best Actor Comedian of The Year

- Dogo Sele amepokea tuzo ya mwaka 2025 kama mchekeshaji bora mtoto

- Neyla Manga Amechukua Tuzo ya Mchekeshaji Bora wa Kike wa Jukwaani kwa mwaka 2025.

-Familia ya marehemu King Majuto imepokea tuzo ya heshima katika Tanzania Comedy Awards, ikitambua mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya vichekesho

Katika hali ya utani, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wazo lililotolewa na wachekeshaji la kucheza mchezo wa ‘upatu’ linaweza kuwa zuri endapo likibadilishwa na kutafutiwa namna bora ili kusaidia masuala ya kifedha ya nchi za Kiafrika.

Rais Samia amesema wazo hilo likichukuliwa kitofauti litakuwa na mchango wa kujitegemea kifedha, kama wakikubaliana na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuunda mfuko wao.

Rais Samia akishiriki Halfa ya Utoaji Tuzo za Wasanii wa Uchekeshaji Tanzania Ukumbi wa The Super Dome Februari 22, Dar es Salaam.

Pia soma: Pre GE2025 - Rais Samia kuwa mgeni rasmi wa kwenye tuzo za Tanzania Comedy Awards

Updates....
-Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameshinda tuzo ya Kiongozi Mcheshi katika Usiku wa Tuzo za Ucheshi (TCA) Zilizofanyika katika Ukumbi wa Super Dome Jijini Dar es salaam.

Katika Kinyanganyiro hicho Makongoro alikuwa akichuana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, Mchingaji Hananja, Mkuu wa Mkoa Mstaafu Aggrey Mwanri na Sheikh Kipozeo.

-Wachekeshaji Steve Mweusi na Ndaro wameibuka washindi katika kipengele cha Best Comedy Duo katika tuzo za wachekeshaji Tanzania.

-Mchekeshaji maarufu Bongo, TX Dullah ameibuka mshindi katika kipengele cha Best Male Digital Comedian of The Year (Mchekeshaji Bora wa Kiume wa Kidijitali wa Mwaka) katika Tuzo za Wachekeshaji Bongo.

-Leonardo ameibuka Mshindi wa Jumla akinyakua Tuzo kubwa ya Overall best comedian of the year kwa wanaume na wanawake.

Hivi Tukio hilo kweli Lina 'upako' hadi kufaa au kuwa na sifa za kuweza kumualika na Rais wa nchi ili ahudhurie??
 
Ivi mama etu huwaga anatembea na sh ngap Kwa mkoba wake? Yaan yeye mtu akimsogelea anapewa bahasha 😀
Kwa kweli kazi yake ya kututumikia watanzania ni takatifu na nzito haswa ,ndio maana CHIEF COMFORTER OF THE NATION ni yeye peke yake....

Mwenyezi Mungu amlinde ,amhifadhi na kumpa afya njema mama yetu ,aaamin aaamin !

#JMT milele dumu !
 
Neila Manga amezingua, hakupaswa kuperform maneno yale mbele ya Rais na watu wazima.
Aibu nimeona mimi!
 
Back
Top Bottom