Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,646
Fuatilia matangazo haya ya moja kwa moja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akifunga mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Chuo cha Uongozi cha Mw. Nyerere, Kibaha - Pwani.
View: https://www.youtube.com/live/6w995GGGrS4?si=8EBhTwCrgxbyhJNG
Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
~ Viongozi katika ngazi zote wanatakiwa kubadilika kutokana na mabadiliko ya dunia na hivyo kuchangia katika kuleta maendeleo.
~ Viongozi wanatakiwa kuacha kujidogosha na kusubiri maelezo kutoka juu, badala yake wawe macho kufatilia mambo na kwenda haraka na mabadiliko hivyo kuleta maendeleo.
~ Rais Samia ataka viongozi wawe na ndoto zao, wajue nini wanataka kufanya kuendana na sheria, kanuni, miongozo ya serikali, mipango na mikakati ya serikali, katika kutumiza kazi zao na kuleta maendeleo sehemu walipo. Kiongozi asisubiri Rais aseme Mkuu wa Mkoa fanya badale yake kiongozi afanye kwa mtindo wake, akijituma, kujielewa, na kujua nini anafanya, bila kuyumbishwa katika nafasi yake.
~ Viongozi wanatakiwa kuwa na hoja za kutetea maamuzi yao pale wanapopewa changamoto na watu, bila kuwa na kichwa ngumu, bali ni kwa kufuata miongozo, kanuni na sheria zilizopo kitaifa.
~ Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala watakiwa kuhakikisha usalama katika maeneo yao ikiwemo ulinzi wa vijana nchini, sababu miradi mingi inayoletwa inalenga sehemu ambazo zitawapata vijana na kuwaharibu, hivyo ni muhimu kuangalia miradi hii inafanya nini ili kulinda vijana nchini. Akiongeza kuwa kazi yao ni kulinda vijana kubaki katika tamaduni za Kitanzania, na sio kuharibiwa na tamaduni za nje.
~ Rais Samia asema ana taarifa za mtindo wa Maafisa Elimu, Afya nk, kutaka wakatiwe magawio yao kwanza ndio fedha zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo, akisema kuwa ingawa sasa wamepunguza kidogo lakini bado wapo wenye kufanya vitendo hivyo, akiagiza Wakuu wa Mikoa wakasimamie vizuri maeneo yao.
~ Kero zisikilizwe chini kabla ya kumfikia Mkuu wa Wilaya, jambo litakalopunguza mrundikano wa kero kwa Mkuu wa Wilaya pamoja na watu kwenda kutoa kero zao kwenye misafara ya Rais kupitia mabango yao.
~ Wakuu wa Mikoa watakiwa kupunguza migogoro ya ardhi ambayo baadhi inasababishwa na Watendaji, Madiwani pamoja na TAMISEMI, akisema ardhi ni moja ya jambo linalosababisha mitafaruku kwa kiasi kikubwa.
~ Rais Samia akemea Wakuu wa Mikoa kutowachukulia hatua Wakuu wa Wilaya, akisema hata kama hawana mamlaka ya kuwatengua bado hawatoi hata taarifa ngazi za juu, juu ya uozo unaofanywa mpaka Kassim Majaliwa apeleke ripoti kwake. Mpaka inatokea Mkuu wa Wilaya anahongwa kuhamisha miradi na kupeleka isikotakiwa, hadi wananchi wanarudisha kadi za chama na kusema hana imani na Mkuu wa Wilaya anayesababisha kadi zirudishwe, na kutokana na hili Rais Samia alimfuta kazi Mkuu wa Wilaya Mtwara Hanafi Hassan.

"Nilivyokuwa Mbeya kwenye maadhisho ya Nanenane nilikuta kadhia, Maafisa wa Halmashauri wametengeneza mtandao wao mbali wa ule unaokusanya fedha za serikali kiuhalisia, kuna mwingine wa pembeni na umekusanya pesa nyingi sana, baada ya wao kufanikiwa wakawapa jirani zao, nao wakawapa jirani zao. Nilikuwa nasubiri ripoti kutoka kwa waziri hajaleta bado lakini nalijua na mimi nafuatilia kwa njia zangu, sasa hiyo ripoti ije diluted.
"Kwa hiyo kuna hayo na pale mlipo kuna DC, DED, TAKUKURU, DSO lakini bado watu wamethubutu kufanya mitandao ya pembeni kukusanya pesa ya serikali iingie mifuko mingine na zimekusanywa. sasa unajiuliza hawa watu wote hawa wanafanya kazi kule waliko au wanafanya nini au wanajifanyia kazi badala ya kuwafanyia watu na kuisaida serikali kufanya kazi wanajifanyia wenyewe kazi, sababu kama watu wote hawa wapo kazini hili jambo lingeonekana mapema. Kama kuna ma internal auditor kule lingeonekana mapema lakini kinachoonekana kuna syndicate, kuna makundi yanatengenezwa hela zinakatwa mpaka kila mtu anapata fungu lake, vinginevyo huu mfumo usingeishi, umeishi kwasababu kuna syndicate." Rais Samia amesema hayo na kuwataka viongozi wakasimamie vizuri kwenye maeneo yao.