Ninja
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 354
- 546
Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu:
Anayekushauri utumie mkono wa chuma anataka upoteze msingi wako asilia wa ushindi na usimame juu ya msingi usioujua.
Kwenye mapigano ya asili, naweza kuwa mpiganaji mzuri nikiwa juu ya farasi lakini nikawa mnyonge nikiwa bila farasi. Au naweza kuwa mpiganaji mzuri ardhini bila farasi lakini nikawa mnyonge nikiwa juu ya farasi. Eneo langu asilia la mapigano hunipa faida dhidi ya adui ikiwa nitalitumia vema katika mapambano.
Pia soma: Kuna la kujifunza hapa kutoka na sera zetu za mkono wa chuma
Maandiko matakatifu 1Samweli 17:38-39: "38Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii. 39Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua."
MSISITIZO:
Mwanzo wa ushindi wa Daudi eneo la vita ilikuwa ni kujiondoa kwenye msingi wa nafasi ya mapigano ambao haukuwa asili yake ili kurudi kwenye asili yake. Na akashinda vita.
1Samweli 17:39c "Basi Daudi akavivua" Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu: Tafadhali nakuomba uvivue. Kisha vaa vitu vyako wewe. UTASHINDA. Vinginevyo sikuoni popote 2025.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Kwa maoni yako, nani anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2025?