Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,715
- 4,455
Wakuu,
Kuna namna viongozi wetu wanatuchukulia sisi ni wasahaulifu au hatutilii maanani yale maneno ambayo wanayasema. Wanatuchukuliaje?
Baada ya jengo la kariakoo kuanguka tuliambiwa kuna tume inaundwa chini ya usimamizi wa Majaliwa ili kujua kinagaubaga cha jengo hilo kuporomoka, lakini mpaka leo kimya lakini mpaka sasa, miezi 3 baada ya jengo hilo kuanguka hakuna ripoti imetoka.
Na huu umekuwa kama utaratibu. Ahadi zinatolewa, hakuna kitu kinafanyika, life goes on
Hii imenikumbusha kipindi kile cha moto wa Kariakoo.
At least kipindi kile tume ilifanya kazi na ripoti alikabidhiwa Rais Samia lakini ripoti hiyo haijawahi kutolewa kwa umma wakati ni suala linalohusu umma.
Soma pia: Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024
Huenda na kwenye Tume ya kuchunguza ghorofa la kariakoo serikali ilikuwa na taarifa zote lakini walipuuzia huenda na rushwa ikatembea ghorofa likatema sasa tunasahaulishwa wanaotakiwa kuwajibika kupata haki yao.
Kuna kipindi tuliona kuhusu kukamatwa kwa mmiliki wa jengo hilo pamoja na kufikishwa mahakani ikaishia hapo! Kwanza kesi imeendaje? Alikutwa na hatia au la? Ama alipofikishwa mahakani ndio ilikuwa imetoka hiyo?
Soma pia: Wamiliki jengo lililoporomoka Kariakoo wafikishwa Mahakamani Kisutu
Leo wakati Rais anakula cha mchana na hao waokoaji, tunataka tujue tume iliyoundwa kwa ajili ya janga la Kariakoo iko wapi? Na wale wamiliki wa jengo kesi yao imefikia hatua gani?