Rais Samia ampokea Rais wa Guinea-Bissau, Ikulu ya Dar - Juni 22, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,293
12,886

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, leo Juni 22, 2024, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Embaló ana ziara ya kikazi kwa siku mbili nchini, ikiwa ni mara ya kwanza kwake kufanya ziara nchini Tanzania tangu nchi hiyo ipate uhuru.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa ziara hiyo itatoa fursa kwa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano na uhusiano ambao umedumu kwa muda mrefu ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Amilcar Cabral wa Guinea-Bissau wakati wa kupigania uhuru.

Viongozi hao wakuu wanatarajia kuongoza mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Tanzania na Guinea-Bissau na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ushirikiano (General Framework Agreement) ambao utaongeza mahusiano kati ya nchi hizi mbili.

Aidha, Rais Embaló anatarajiwa kutembelea Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Makao Makuu ya Sekretarieti ya Taasisi ya Viongozi wa Afrika ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria (ALMA) yaliyopo hapa nchini, ambapo yeye ni Mwenyekiti wa ALMA.

Snapinsta.app_448920451_766089509064208_6040444345476934002_n_1080.jpg

Snapinsta.app_448887449_784631390318581_3611417268897602418_n_1080.jpg

Snapinsta.app_448974348_3667749550221010_4964037491224075477_n_1080.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaló, leo tarehe 22 Juni, 2024 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais Embaló yuko nchini kwa ziara ya kikazi.
Snapinsta.app_448970649_1153774305935374_4731046667916776655_n_1024.jpg

Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Juni, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan:
Nchi yetu imepata fursa ya kutembelewa na mgeni ambaye ni kaka yangu na rafiki mkubwa wa Tanzania ambaye pia anazungumza Kiswahili pia.

Ziara hii ni ya Kihistoria ni mara ya kwanza kwa Rais wa Guinea-Bissau kuitembelea Tanzania.

Nchi zetu zina uhusiano mzuri hata kabla hatujapata uhuru, viongozi wa mataifa haya mawili Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Amilcar Cabral wa Guinea-Bissau walikuwa na ushirikiano wakati wa kupigania uhuru.

Ziara hii imetupa fursa ya kujadili yale ambayo baba zetu waliyaanza, muda mfupi uliopita mimi na Rais tumezungumza na tumebadilishana mawazo ikiwemo ukuzaji amani na biashara, kuimarisha sekta ya kilimo na biashara pamoja na Uchumi wa Buluu.

Tumerejea adhma yetu kutumia eneo huru la biashara kati yetu, Nchi hizi mbili ni wazalishaji wa Korosho, tumekubaliana kuanza katika eneo hilo.

Eneo lingine ni maeneo huru ya uwekezaji, Rais Embaló atapata nafasi ya kutembelea Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).

Pia tumezungumza kuhusu Uchumi wa Buluu, sote tupo katika nafasi nzuri ya kufanya biashara katika Nchi zinazotuzunguka, tumezungumza kushirikiana katika mambo kadhaa.

Tumesaini makubaliano ya kuanza mazungumzo katika sekta ya Uchumi.

Mgeni wetu, Rais Embaló ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Viongozi wa Afrika ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria (ALMA) tumepongeza kwa nafasi hiyo.

Raia wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló:
Tanzania ilitoa mchango mkubwa katika kupinga Ukoloni na ubaguzi wa rangi Afrika.

Nipo hapa kutoa heshima kwa Rais Nyerere ambaye alifanya mambo makubwa katika Hisotia, alitembelea Nchi yetu Mwaka 1976.

Mataifa ya Afrika yakifanya kazi pamoja yana nafasi ya kufanya makubwa katika mustakabari wa Dunia.

Ndugu zangu wa sekta Binafsi mnakaribishwa Guinea-Bissau ili muweze kunufaika katika biashara kwenye nyanja mbalimbali na pia nchi yetu inaweza kuwa njia au mlango wa kwenda nchi nyingine mbalimbali.

Tuko hapa Tanzania na tunajisikia kuwa na furaha na amani. Viongozi wetu wote waliopigania uhuru walikuja hapa Dar es Salaam.

Guinea-Bissau hatutasahau kuhusu Tanzania, tukiwa shuleni tulifundisha kuhusu Mwalimu Nyerere.

Tupo tayari kuibariki Tanzania mkituhitaji, kipindi channgu chote cha Urais nipo tayari kufanya kazi kwa ukaribu zaidi.

Nikirejea Guinea-Bissau nitahakikisha Wanafunzi wanakuja hapa kujifunza Kiswahili, mimi pia nitakuwa Mwanafunzi wa kwanza wa Lugha ya Kiswahili.

Snapinsta.app_448988440_7763715863723242_43767798596489253_n_1024.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.
Snapinsta.app_448977791_967475688392467_7455882826856345566_n_1080.jpg

Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.​
 
Umaro = Omari. Safi sana; ziara za viongozi wa mataifa nchini mengine akina Guinea Bissau ni ishara ya nchi kutambulika na kukubalika kimataifa.
 
Back
Top Bottom