Pre GE2025 DSM Rais Samia akizindua Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 Toleo la Mwaka 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
4,048
13,863
Rais Samia akizindua Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 Toleo la Mwaka 2025 Mlimani City, Dar es Salaam


Viongozi mbalimbali wa chama tawala na serikali, pamoja na viongozi wa dini, wamewasili kwenye ukumbi wa Mlimani City kushiriki Kilele cha Wiki ya Maji 2025.

1742635054939.png


1742635083745.png

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wananchi wa mkoa wake zaidi ya milioni 5 wamepata nafuu ya upatikanaji wa maji ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan

Chalamila amesema hayo wakati akitoa salamu za mkoa kwenye kilele cha wiki ya maji 2025 katika ukumbi wa Mlimani City ambapo mgeni rasmi ni Rais Samia kwenye sherehe hizo

Chalamila ameongeza kuwa kumefanyika miradi mikubwa katika mkoa huo yenye thamani ya shilingi trilioni 1.9 ambapo mingine ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi

Aidha amesema kuwa mradi wa Kinyerezi na Ukonga wenye thamani ya shilingi bilioni 36.7 itakuwa mkombozi wa wananchi wa maeneo hayo huku mradi wa shilingi bilioni 23 wa Chamazi na Kijichi na maeneo mengine utakuwa mkombozi wa wakazi wa Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, amesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji nchini imefikia asilimia 83 vijijini na 91.2 mijini.
 
Back
Top Bottom