Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,616
- 13,302
View: https://www.youtube.com/watch?v=1ukeVgqCvHo
View: https://www.youtube.com/watch?v=_bs_27YOIos
RAIS SAMIA: TUMEKUBALIANA KUUNDA UMOJA WA WAZALISHAJI WA KOROSHO AFRIKA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Nchi zinazozalisha Korosho Barani Afrika ikiwemo Tanzania zinatarajiwa kuwa na umoja wao ili kuwa na sauti katika zao hilo.
Amesema hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Julai 2, 2024 alipomkaribisha Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi ambaye yupo kwenye ziara ya siku nne Nchini.
Aidha, Rais Nyusi anatarajiwa kutumia nafasi hiyo kuwaaga Watanzania akielekea kumaliza muhula wake wake wa pili wa uongozi mwishoni mwa Mwaka 2014 tangu alipoingia madarakani Januari 2015
============= =================
Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi amepolekewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Dar es Salaam, leo Julai 2, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake rasmi ya kikazi ya kuimarisha uhusiano na biashara Nchini Tanzania.
Rais Filipe Nyusi ametumia nafasi hiyo pia kuwaaga Watanzania akielekea kumaliza muhula wake wake wa pili wa uongozi Oktoba, 2024.
Kuona mapokezi yake alivyowasili, bonyeza hapa ~ Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi alivyowasili Tanzania (Julai 1, 2024) kwa ziara ya Kitaifa ya siku nne
Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba alisema ziara hiyo ya siku nne, imetokana na mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kiongozi huyo.
Makamba alisema ziara hiyo inaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria, kidugu na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ambao uliasisiwa na viongozi wa mataifa hayo, Kiongozi wa kwanza wa Chama Tawala cha Msumbiji (FRELIMO), Hayati Eduardo Chivambo Mondlane na Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere.
Rais Nyusi pia anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), kesho Julai 3, 2024 ambapo ataambatana na mwenyeji wake, Rais Samia.
Rais Nyusi anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 04 Julai, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan anazungumza:
Tumetoka kwenye mazungumzo maalum, nitagusia maeneo machache tuliyozungumza, kwanza namshukuru Rais Filipe Nyusi kwa ujio wake na kukubali kushiriki katika Maonesho ya Sabasaba mbapo atakuwa mgeni rasmi.
Uhusiano wa Tanzania na Msumbiji ulianza hata kabla ya mchakato wa uhuru, Nchi hizi ni ndugu.
Kuonesha sisi ni ndugu na hata kwenye lugha tunaelewana, Rais Filipe Nyusi ameahidi kuwa kesho atahutubia kwa Kiswahili katika Maonesho ya Sabasaba.
Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Nchi hizi mbili ulianza Mwaka 1977 kwa kusaini makubaliano ya pamoja ya kushughulikia uhusiano wetu wa masuala mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, uhamiaji, Kilimo na afya.
Kupitia mazungumzo yetu, tumekubaliana kuwa na Kituo Kimoja cha Forodha kitakachoshughulikia changamoto za kibiashara baina ya Nchi hizi.
Mwaka 2022, Biasharaya Tanzania -Msumbiji ilikuwa Dola Milioni 57.8 lakini Mwaka 2023 kiwango kilishuka, tumekubaliana kuliangalia hilo.
Inawezekana kuna maeneo ambayo biashara haifanyiki rasmi na hivyo Wafanyabiashara wanatumia njia za pembeni na kukosesha mapato.
Takwimu zinaonesha kuna wawekezaji wawili wamewekeza Tanzania wakitokea Msumbiji, pia kuna Wawekezaji 16 wa Tanzania wamewekeza Msumbiji, tumeona hiyo ni idadi ndogo, kuna haja ya kuongeza ili kuboresha uhusiano wa kiuchumi.
Tumezungumza kuhusu ushirikiano wa Uchumi wa Bluu, tumekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kuiendeleza sekta hiyo.
Nchi zote mbili ni wazalishaji wa Korosho lakini sio wapangaji wa bei za korosho Duniani, tumekuwa tukipanga katika soko la ndani, tumekubaliana kuunda umoja, kama mnakumbuka alipokuja Rais wa Guinea-Bissau nilimpa wazo hilo naye akalikubali, hivyo tunaenda kuwa na umoja wetu ili tuwe na sauti moja katika masoko.
Eneo la ulinzi na usalama, mpaka wetu ni mkubwa sana, Tanzania inashirikiana na SADC katika kuimarisha ulinzi.
Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi anazungumza:
Tunatambua mchango mkubwa wa Tanzania na ndio maana tumekuwa tukifika hapa mara kwa mara.
Namshukuru Rais Samia ametupa hoteli nzuri na kama isingekuwa mkutano huu ningekuwa bado nimelala.
Sisi tunazo rasilimiali, nishati, ardhi, watu na vingine vingi, tunatakiwa kutumia rasilimali hizo zote wa faida.
Tunatakiwa kufanya biashara kwa pamoja, mfano bidhaa ya Korosho ikichukuliwa na wenzetu sisi hatufaidiki zaidi, kuwa na Umoja wa Nchi zinazosalisha Korosho ni jambo linaloweza kutokea baadaye.
Tunatakiwa kuwa na Barabara zinazoweza kutuunganisha Nchi na Nchi, lengo ni kutimiza adhma ya viongozi wetu waasisi walioanzisha umoja na ushirikiano wa mataifa haya.
Uwepo miundominu inayoweza kutuunganisha kama vile Barabara itaongeza uzalishaji wa mambo mengine.
Naishukuru Tanzania kwa kuwa sehemu ya majeshi yanayotusaidia, wao pamoja na nchi nyingine kadhaa, hawana pesa nyingi ya kutupa lakini wanatumia umoja wao kutusaidia, mfano Mwaka 2021 hali ilikuwa mbaya zaidi kutokana na matukio ya ugaidi.
Kwa sasa Watu wameanza kurejea katik makazi yao, vita ya ugaidi ni ngumu kwa kuwa magaidi ni watu wanaohamahama na wanaweza kuhama sehemu moja kwenda nyingine kwa ajili ya kufuata mahitaji.
Tunashuruku majeshi kwa kuweza kurejesha amani.
Watu wa Msumbuji hawawezi kusahau mchango wa Tanzania katika masuala ya uhuru, hata vijana wapya wanatakiwa kutambua kuwa ushirikiano huu hautakiwi kuishia miaka ya nyuma, unatakiwa kuendelezwa.