Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,806
- 13,574
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Akifunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania, Viwanja vya Jeshi la Polisi CCP Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 17 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameungana na Watanzania katika kulaani mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ally Kibao yaliyosababisha mshtuko na hisia kali nchini.
"Siku kadhaa zilizopita ndugu zangu nchi yetu imepata msiba wa kuuawa kwa mmoja wa viongozi wa CHADEMA, kifo kilichosisimua miili na akili za sisi wananchi na kuibua hisia kali hasa kwa wafuasi wa chama hicho. Kifo hicho kimeleta majonzi sio tu kwa Watanzania bali pia kwa wawakilishi wa baadhi ya mataifa ya nje wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania"
Ameongeza kuwa hivi karibuni alipokea ripoti kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kuhusu watu watatu waliouawa Dodoma, lakini matukio kama hayo hayaibui hisia za umma kama ilivyokuwa kwa kifo cha Kibao katika kudhihirisha namna Watanzania na jamii ya kimataifa ilivyoguswa kwa mauaji ya kibao.
Rais Samia amesisitiza kwamba, licha ya kifo cha Kibao kuibua hisia na lawama nyingi dhidi ya serikali, ni muhimu kwa Watanzania wote kukemea vifo vyote bila kujali ni nani aliyeuawa. "Kifo ni kifo, tunachotakiwa kufanya Watanzania wote tukemee mambo haya, damu ya Mtanzania ituume," amesema Rais, akisisitiza umuhimu wa kulinda utu wa kila raia wa nchi.
Pamoja na hayo, aliendelea kusema, "Kifo cha ndugu yetu Kibao kimeibua wimbi kubwa kulaani, kusikitika, kulaumu, kuita serikali ya wauaji, hii sio sawa. Kifo ni kifo, na hatupaswi kupuuza damu ya Mtanzania."
Kuhusu Uchaguzi Rais Samia Suluhu Hassan amesema;
"Katika kipindi cha uchaguzi kila mmoja wetu anatakiwa kujipanga kufanya kazi zake vizuri zaidi tumejipambanua kulileta Taifa letu pamoja, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha Taifa letu linabaki kuwa moja na salama, uchaguzi utapita lakini Tanzania itabaki, tunataka kubaki na Tanzania iliyo salama na Tanzania yenye utulivu ili shughuli za maendeleo ziweze kuendelea".
"Nalitaka Jeshi la Polisi kuwa macho katika kipindi chote cha kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Polisi ihakikishe yeyote anayejaribu kuhatarisha amani ya nchi yetu kwa kisingizio za chaguzi hizo anachukuliwa hatua haraka na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria".