Rais Samia akemea suala la siri za Serikali kuvuja mitandaoni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,176
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri na manaibu Waziri wahakikishe siri za serikali hazivuji kufika katika mitandao ya kijamii kama ambavyo imeendelea kuwa

Nukuu
'Imekuwa kama maradhi, document za Serikali tunazikuta mitandaoni, watu wanabishana huko mtu anaende kuchomoa document inapigwa picha inawekwa kwenye mtandao, kama mnabisha ushahidi ni huo, hii haipendezi na hakuna serikali inaendeshwa hivyo.

Serikali inatoka kwenye ofisi zetu inaingia kwenye mitandao, kudhibiti siri za Serikali, ziwe za siri 'classified' hata zile ambazo haziko 'classified', tunatakiwa mambo ya Serikali yaishie ndani ya serikali.''


Ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya na mawaziri na manaibu Waziri aliwateua na kuwaapisha hivi karibuni

Pia Rais amewataka waende kuwa wasimamizi wazuri wa miradi ya serikali kwa kuwa serikali ipo kwa ajili ya watu
 
Kwani si huwa wanakula viapo vya kutovujisha siri?

Sasa kwa nini siri zinapovuja, yeye kama Rais huwa hafanyi uchunguzi kujua chanzo cha uvujifu?
 
Siri za serikali ni zipi? na kwanini serikali inayowatumikia wananchi iwe na siri kwa wananchi inaowatumikia? na ni faida gani serikali inapata kwa kuficha mambo yake kwa wananchi?

Huu msemo "siri za serikali" unatakiwa kukomeshwa, ni msemo unaoendekeza ukiritimba wa mambo mengi ya hovyo yanayofanywa na serikali.

Mambo mengi mabaya hufanywa siri, mfano ufisadi, kama hii ndio sababu ya Samia kutaka siri za aina hii zifichwe basi hayupo ikulu kwa ajili ya kuwatumikia watanzania kama anavyosema kila siku, yuko ikulu kulinda interest zake na kundi lake.
 
Rais Samia amesema imekuwa kama maradhi vile watu wananyofoa documents za serikali na kuziweka mitandaoni, hii haipendezi.

Unakuta mtu anabishana kisha ananyofoa document ya serikali na kuiweka mitandaoni, hakuna serikali inayoendeshwa kwa utaratibu huo, amesema Rais Samia.

Source: East Africa radio
 
Ndio maana namna kero za muungano zilivyotatuliwa imekuwa Siri!Mnaficha nini?
 
Back
Top Bottom