15 December 2021
Dodoma, Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akemea fujo na vurugu za vyama vya kisiasa
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Disemba 15, 2021 amefungua mkutano wa wadau wa vyama vya siasa nchini ambao unalenga kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini.
Akabainisha kuwa mikutano yenye fujo , vurugu, kuchochea migomo (civil strife) , kuharibu Mali za watu, kuandamana bila vibali ndiyo imepelekea mikutano imefungiwa mpaka sasa asema Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.
Akasisitiza wanasiasa na vyama vyao pamoja na wanachama wajiepushe na mienendo hiyo isiyofaa kwani mikutano hiyo itaendelea kuzuiwa.
Mh. Rais awataka viongozi wa kisiasa na vyama vya siasa kujitathmini na kutumia mkutano huo wa leo Disemba 15, 2021 kujirekebisha ili kuondokana na kufungiwa shughuli hizo za kisiasa ambazo kimsingi katiba inaruhusu na ni haki mikutano ya kisiasa kufanyika amesisitiza Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.
Watu mashuhuri na taasisi ziliizohudhuria mkutano huo ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa , wenyeviti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa na Zanzibar, Jeshi la Polisi, Spika Mstaafu Anne Makinda, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba.
Mkutano huo wa siku mbili unaofanyika jijini Dodoma umeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Baraza la Vyama vya Siasa.