Rais Samia Ajihadhari na Mtego wa Wa Fomu 1.

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,996
47,958
Rais Samia alipoingia madarakani, kutokana na yale aliyoweza kuyatenda mwanzoni, alisifiwa, alipendwa na kuungwa mkono na watanzania wengi wenye akili timamu wenye mapenzi mema kwa Taifa:
1) Alifuta kesi za kuwabambikia wapinzani

2) Mara kadhaa alikemea vitendo vya kishetani vilivyokuwa vikifanywa na polisi dhidi ya raia.

3) Aliteua kamati ya ushauri kuelekea kwenye mchakato wa katiba mpya

4) Alikuja na falsafa ya 4Rs

Wabaya wake, hawakufurahishwa na umaarufu wa Samia ndani ya ya kipindi kifupi. Wakajipanga vizuri kuhakikisha hapati mafanikio. Kila alichokipanga, wao walifanya kinyume chake, na mzigo wa chuki ulienda kwa Samia.

Katika kuchukiwa na wananchi, wakiwemo wapinzani ambao walimwunga sana mkono, Samia hakuwa na chaguo jingine zaidi ya kuwaangukia waovu ambao walifanikiwa kumhadaa aone kuwa wao ndio wanampenda na kumtakia mema kuliko watu wengine wote. Machawa wanafiki, waovu na wenye hila wakawa wameshinda.

Leo:
1. Huwezi kumsikia Samia anaongelea 4Rs
2. Leo huwezi kumsikia Rais Samia akiwalaumu polisi kuhusiana na matukio ya utekaji na mauaji ya wakosoaji wa Serikali yake, iwe ni kwa kuhusika kwao au kushindwa kutimiza wajibu wao.

3. Rais aliyekuwa anajinasibu ni mwanademokrasia, mahasimu wake wamemwandalia mtego wa kuchapisha fomu moja kwaajili yake pekee yake, na yeye hawezi kukemea, na yumkini, anafurahia!!

Unapotoa fomu 1 kwaajili ya mgombea mmoja, ni sawa na kusema kuwa hakutakuwa na uchaguzi ndani ya chama, maamuzi ni tayari.

Lengo la mtego huu, ni kumwingiza Samia kwenye orodha ya marais madikteta wa Afrika. Na hao ndio wanamtengenezea mazingira ya kufuta uchaguzi wa Rais nchini Tanzania, yaani kuufanya kuwa uchaguzi bandia, uchaguzi wa maigizo. Bila shaka watazamaji wa kimataifa, hapo mwakani watakuja kushuhudia uchaguzi wa kidikteta kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa kwenye taifa lolote Duniani ambapo kuliwahi kuwepo waangalizi wa kimataifa. Na hiyo itaufanya utawala wa Samia kutengwa na Dunia yote ya watu wastaarabu, na hapo hawa maadui zake watakuwa wamefanikiwa, maana atakuwa amefunga milango yote na kuamsha mijadala mikali itakayoweza kusababisha mabadiliko makubwa kwenye mifumo ya utawala.
 
Umenena vema kabisa. Na la kuhusu uchaguzi wa mwakani uko sahihi kabisa mwakani tutashudia unyama na ukatili mwingi kutoka kwa vyombo vya dola hasa polisi na Usalama wa Taifa ili kufanya CCM ipate ushindi wa 99% kwani mfano tumeuona kwenye uchafuzi wa serikali za mitaa, amabapo wagombea wa upinzani walipigwa risasi na polisi na wengine kuuliwa kwa kukatwa mapanga. Uchafuzi wa 2019 Magufuli hakuua bali aliamua kuwafutilia mbali wagombea wa upinzani ili CCM ipate ushindi wa 100%, lakini huu wa safari hii walifutwa wapinzani na kuuwawa waliuwawa. Na katika ukatili na ubatili huu wa majuzi Samia amekaa kimya ishara ya kuafiki kilichofanyika kukipa chama chake ushindi wa 99%.
 
Back
Top Bottom