Pre GE2025 Rais Samia afunguka ya Moyoni: Kuna waliosema tuna Rais wa kuambiwa afanye na mwenye maamuzi ya Kitchen Party, hatuna Rais tuna House girl…

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,947
5,297
Rais Samia afunguka ya Moyoni kuhusu kauli za Wahafidhina wa mfumo dume ambao hawakuwa na imani naye wakati anachukua nafasi ya Urais na waliothubutu kusema "Tuna Rais wakuambiwa afanye na mwenye maamuzi ya Kitchen Party" wakati akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika Uongozi katika Siasa.

Akishiriki Madhimisho ya Miaka 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es Salaam, leo tarehe 21 Februari,2025, Samia amesema;

"Hapa nataka kusema ya Moyoni, kwenye wahafidhina wa mfumo dume kwamba wakati ule hakukua na imani kabisa, hakukua na imani au kuamini kwamba yule mwanamke anaweza kufika hapa [hakukua..]"

"Kuna waliothubutu kusema tuna Rais wakuambiwa fanya tu na atafanya. Kuna waliothubutu kusema hatuna Rais tuna House girl. Kuna waliothubutu kusema maamuzi ya Kitchen Party, yale ambayo nilikuwa nafanya"

Soma, Pia: Rais Samia: Nafasi ya Uongozi unayoipata Mwanamke isiwe sababu ya kuharibu familia

Watanganyika mnachokitafuta mtakipata, kiko jikoni chungu chungu cha dawa na inawahusu hadi mpone maradhi mlonayo
 
Rais Samia afunguka ya Moyoni kuhusu kauli za Wahafidhina wa mfumo dume ambao hawakuwa na imani naye wakati anachukua nafasi ya Urais na waliothubutu kusema "Tuna Rais wakuambiwa afanye na mwenye maamuzi ya Kitchen Party" wakati akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika Uongozi katika Siasa.

Akishiriki Madhimisho ya Miaka 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es Salaam, leo tarehe 21 Februari,2025, Samia amesema;

"Hapa nataka kusema ya Moyoni, kwenye wahafidhina wa mfumo dume kwamba wakati ule hakukua na imani kabisa, hakukua na imani au kuamini kwamba yule mwanamke anaweza kufika hapa [hakukua..]"

"Kuna waliothubutu kusema tuna Rais wakuambiwa fanya tu na atafanya. Kuna waliothubutu kusema hatuna Rais tuna House girl. Kuna waliothubutu kusema maamuzi ya Kitchen Party, yale ambayo nilikuwa nafanya"

Soma, Pia: Rais Samia: Nafasi ya Uongozi unayoipata Mwanamke isiwe sababu ya kuharibu familia

Naomba msimdharau House Girl.Kuna mabint wanakaa watoto mpaka unaona awe tu familia.
Anapata mtaji anajiendeleza
 
Sasa kwani yeye huyo mwanamke si ni kwa dondokela tu akawa?! Ama lini alikuwa hapo alipo kwa uwezo wake?
pamoja na mambo mengine lakini bahati pia inasaidia kwenye maisha, mfano olivier giroud kubeba kombe la dunia ilhali ronaldo ambaye ni mchezaji aliyekamilika kushindwa kubeba kombe hilo.
 
Mimi nadhani angetangaza nia ya kugombea urais sasa kwa kuruhusu wengine wenye nia ya kugombea urais ndani ya chama chakavu, wachuane kwa hoja kisha wapitie mchakato wa chama uliopo kikatiba! ...kwa vyovyote kwa sifa anazopewa na mabango ya taswira yake nchi nzima, angewashinda wote kabla ya kupambana na Simba Tundu Lissu....

Aachane na mbeleko ya wazee waliojichokea, na wale wenye masilahi binafsi....Akishinda atawafunga midomo wote wanaoitwa mfumo dume na wengine wasiomuona kama anayefaa kuendelea kukalia kiti cha urais. 🤔
 
Back
Top Bottom