Rais Samia aanza kutoa Fedha bilioni 75.98 kwa Vijana na Wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya. Hii ni Fursa, tuchangamkie

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,255
1,563
Tatizo la ajira kwa Vijana ni tatizo la dunia nzima kwa sasa, tatizo hili linachangiwa pia na hali ya uchumi wa dunia kwa sasa, licha ya jitihada za Serikali inayoongozwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhakikisha uchumi unaimarika bado tatizo la ajira ni changamoto ya dunia nzima.

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa fedha 2022/2023 amepanga kutoa mikopo isiyo na riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu jumla ya shilingi bilion 75.98 kupitia Halmashauri za Wilaya, fedha hizi zitasaidia saana Vijana kuazisha miradi ili kujikwamua na kuoongeza fursa mbalimbali, Vijana watakaopata fedha hizi wanaweza kuajiri vijana wenzao na kuchangia kwenye pato la nchi.

Fedha hizi za mikopo zimeshaanza kutolewa kwenyebHalmashauri zote kupitia Maafisa Maendeleo wa Halmashauri husika katika Ofisi za Wakurugenzi. Vijana twende tukapate mikopo hii isiyo na masharti magumu na haina riba. Vijana wenzangu tukipata mikopo hii tukumbuke kurejesha ili kuwezesha Vijana wenzetu pia waweze kunufaika na Mikopo hii.

Kwa mwaka wa fedha uliopita (2021/2022) Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa jumla ya shilingi bilioni 59,236,353,909.00 kama Mikopo isiyo na riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu,. Kupitia fedha hizo tumeshuhudia Vikundi vingi vikifanikiwa kuazisha miradi mbali mbali na kuweza kutoa ajira kwa vijana wenzao ikiwa ni pamoja na kuchangia katika pato la nchi,

Kuna kikundi cha vijana Dar Es Salaam kilipata mkopo na kufanikiwa kuazisha Kituo cha Afya/ Zahanati ambacho kwa sasa sio kinasaidia tu kutoa huduma kwa Watanzania bali kimetoa ajira kwa Vijana hao na wenzao.

Ukienda Wilaya ya Rufiji maeneo ya Ikwiriri kuna kikundi kilinufaika na mikopo hii kinajihusisha na uselemala, kimekuwa kikundi kikubwa kwa sasa, wanatengeneza fanicha kama pale keko, nimeshuhudia si mara moja Wafanyabiashara wa keko wa fanicha wakienda kuchukua vitanda na fanicha nyingine bora kabisa pale ikwiriri kutoka kwenye kikundi hiki, kikundi hiki kimeweza kutoa ajira kwa vijana wengi (sina takwimu halisi) lakini ukifika kwenye eneo la kazi yao utakuta zaidi ya vijana 100 wakiwa wamejiajiri kutoka na uwezeshwaji wa mikopo hii isiyo na riba.

Niliwahi kuona pia kikundi cha Vijana waliojiajiri na kilimo cha umwagiliaji hapo Rufiji, Vijana hao ni Wasomi kabisa na wanafanya vizuri, wamepata elimu nzuri kutoka kwa Watalaamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, sio rahisi kutaja vikundi vyote lakini ni wazi mikopo hii imekuwa mkombozi kwa Vijana wengi.

Kuna kijiji nilienda huko Rufiji kila kijana ana piki piki anayotumia kwa shughuli zake za kilimo na wengine wanatumia kwa shughuli za biashara, lakini nilipouliza nini kipo nyuma ya mafanikio haya nikaambiwa ni kutokana na uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wananchi unaofanywa na Serikali kupitia mikopo isiyo na riba, vijana wanamashamaba ya korosho na ufuta.

Huko kusini, kuna kikundi cha Mazingira kupitia mikopo hii Wameweza kununua mpaka gari (Scania) la zaidi ya milioni 120 kutokana na mikopo hii ya kuwezesha Wananchi kiuchumi.

Manufaa ya mikopo hii ni mengi, Vijana twende Halmashauri tukapate Elimu, Halmashauri zina Watalaamu wa kila nyanja, Halmashauri zinaweza saidia kupata vifaa kama vya kuazishia viwanda vya tofali etc..

Vijana tutoke kwenye mitandao kwenye kutukana watu na kukejeli, wale wanaokejeli na kupinga kila jitihada za Serikali msiwasikilize wana watu wanaowalipa kwa kazi hizo, Serikali iko macho, inaona.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Raisi wa Jamhuri wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan.
 
Kijana Execute uwe na Heshima, heshima ni kitu cha bure, mtu aliyestarabika ni yule anayeweza kuheshimu watu huku amejificha nyuma ya keyboard kama wewe, Nimesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
Kwahiyo ametoa huyo Samia au ni fedha za serikali zinazotolewa kwa kufuata bajeti iliyopitishwa na bunge?
 
Tatizo mfumo wa kuzipata ni mbovu, zinaishiwa kuliwa tuu huko juu au wakubwa wa halmashauri wanawapa Vijana wao. Wangekuwa na Nia njema, wangepitisha kampeni kwenye masoko ya machinga, sokoni, stend za mabasi na vyuoni, ndo hili kundi kubwa lipo huko. Idea nzuri Ila approach ni mbovu.
 
Ni fedha za asilimia kumi zitokanazo na makusanyo ya Halmashauri.
Hizo ziko miaka yote,badilisheni utaratibu wake..

Mwisho kuna Pesa za 30% za manunuzi yote Tzn yaani tenders ziko reserved kwa vijana na wanawake zaidi ya bil.900 hizo ndio zingewekewa mkazo..

Wa consult PPRA wanajua hili.👇
 

Attachments

  • IMG-20221018-WA0001.jpg
    IMG-20221018-WA0001.jpg
    58.3 KB · Views: 11
Tatizo mfumo wa kuzipata ni mbovu , zinaishiwa kuliwa tuu huko juu au wakubwa wa halmashauri wanawapa Vijana wao .... Wangekuwa na Nia njema , wangepitisha kampeni kwenye masoko ya machinga , sokoni , stend za mabasi na vyuoni , ndo hili kundi kubwa lipo huko... Idea nzuri Ila approach ni mbovu
Mkuu Slowly, Serikali ya awamu ya sitakupitia OR-TAMISEMI imejitahidi saana kuboresha na kusimamia mikopo hii, hakuna Mkubwa wala nani anayekula fedha hizi kwa sasa, mikopo yote sasa ni kupitia mfumo. Kwahiyo Washauri vijana waende Halmashauri wakapate mikopo hii haina upendeleo wowote.
 
Hizo ziko miaka yote,badilisheni utaratibu wake..

Mwisho kuna Pesa za 30% za manunuzi yote Tzn yaani tenders ziko reserved kwa vijana na wanawake zaidi ya bil.900 hizo ndio zingewekewa mkazo..

Wa consult PPRA wanajua hili.👇
Mkuuutaratibu umebadilika, kwa sasa kuna mfumo mpya wa utoaji mikopo hii, yote hii ni jitihada za Serikali kuona mikopo hii ina tija na kuwanufaisha walengwa. Hata hili la 30% za manunuzi ni jitihada za Serikali kuhakikisha Vijana wananufaika na kujikwamua, Elimu inaendelea kutolewa.
 
Hizi hadithi ukisikiliza hapa unaweza kwenda kufuata huo mkopo, sasa shuhudia usumbufu wake, na inabidi uwe na kadi ya ccm kabisa ili uweze kupewa. Achia mbali rushwa utakayombwa ili upate huo mkopo.
Mkuu Tindo amini kwamba mikopo hii haina usumbufu wowote kwa sasa Serikali imeazisha utaratibu mzuri kuhakikisha hakuna usumbufu wala upendelo wowote katika kutoa, Shauri vijana wenzetu twende kwenye ofisi za Wakurugenzi au hata ofisi za Kata kwa Maafisa Maendeleo Wajamii utapata elimu ya kuazisha kikundi na vijana wenzio na kuwezeshwa mikopo hii, maneno ya vijiweni kuwa kuna usumbufu sio kweli.
 
Kwani alikuwa hatoi?
Amina68 Kwa mwaka huu zinatolewa fedha nyingi kuliko miaka yote toka kluazishwa kwa mikopo hii, tena ni zaidi ya bilioni 100 zitatolewa, maana fedha nyingine zitatolewa kupitia fedha za marejesho, kikubwa kama una vijana unawajua wape elimu hii, Waende Halmashauri wakapate elimu na kupewa mikopo hii, no hate.
 
Anaetoa fedha ni samiah au serikali!?kwani ni zake!!?
Patriotic and visionary Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassan, ambaye niye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikubwa kama una vijana unawajua wape elimu hii, Waende Halmashauri wakapate elimu na kupewa mikopo hii, ili kuweza kuajiri Watanzania wenzao na kuchangia kwenye pato la nchi.
 
Kaka hapa cha msingi ni uelezee namna ya kuzipata
masai dada Mikopo hii inatolewa kupitia Halmashauri zote nchini, na unapitia kwa Mafisa Maendeleo waliopo katika kata na ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri, mikopo hii haina riba na inatolewa kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.

Fika ofisi ya Halmashauri ulipo au ofisi ya Kata uonane na Afisa Maendeleo wao ndio watakupa muongozo, Mikopo hii haina usumbufu na wala haina riba, Washauri Wanawake pamoja na Vijana wachangamkie fursa hii.
 
Tatizo urasimu mwingi sana. kupata hizo pesa ni kipengele kizito sana, zinaishiaga kwa wakubwa na wanao fahamiana huko juu
 
Back
Top Bottom