Rais Samia aagiza Mashirika ya Umma kuajiri Watumishi moja kwa moja

naona sakayosa zinaendelea.

Kinachoisumbua hii nchi ni wasimamizi wa mifumo na mianya kwenye mifumo yenyewe, mifumo ina matobo mengi kwa wapumbavu kuuishi upumbavu wao na kuulinda pia.

Unaruhusu mashirika kuajiri yenyewe huku hakuna vyombo madhubutu vya kusimamia usawa na ubora.
 
Watoto wa walalahoi ndio msahau kupata kazi katika hizo taasisi. Utumishi sifahamu makando kando yao mengine ila kwenye suala la ajira wako fair sana. Ni kupitia mfumo wao wa ajira nimeona vijana waliotokea familia za kawaida (akina sie watoto wa mama ntilie) wakipata kazi mashirika/vitengo nyeti Serikalini. Rais Mama Samia Usijaribu kuua mende kwa nyundo, fikiria tena kuhusu kauli/maamuzi yako, elewa tatizo lilipo kisha tatua ila sio kwa kuondoa mfumo rasmi uliopo. Kati ya Mashirika yaliyoongoza kwa vi Memo kabla ya mfumo wa ajira kuwepo ilikua ni TTCL na hapo TRA, ofisi nzima ilikua inaongozwa na familia.
 
Taasisi zinazojitegemea kibajeti, ni vema hata kupata wafanyakazi wake wahusike kuwaajiri chini ya bodi zao Wakurugezi. Na vivyo hivyo CEOs wao wapatikane kwa kuomba na kufanyiwa interviews. Atakayekidhi vigezo, jina lake lipelekwe kwenye mamlaka kwa vetting na uteuzi
 
Back
Top Bottom