Rais Samia aagiza Mashirika ya Umma kuajiri Watumishi moja kwa moja

Phobia

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,156
1,819
MASHIRIKA RUKSA KUAJIRI

“Kuna mashirika ambayo wenyewe wangehitaji ajira za harakaharaka lakini unaambiwa subiri Tume ya Utumishi ikae, subiri sijui utumishi ifanyeje mwaka mzima taasisi kwa mfano TRA inataka watu wakakusanye mapato mwaka mzima watu hawajapatikana, vivyo hivyo TANESCO, REA wanataka watu utumishi paka izunguke iseme ifanye mikutano ifanye semina, hapana hatuendi hivyo.

Kama wanataka wafanyakazi mishahara ya kulipa wanayo haitoki hazina wanataka wafanyakazi kwa ajili ya mradi au kazi fulani wapewe ruhusa wafanye. Wapewe ruhusa wafanye sabahu ajira hizi wala nyingine sio za kudumu mradi ukimalizika na ajira imekwenda. Kwa hiyo wapewe ruhusa waajiri ili miradi ikatekelezwe kwa haraka.”

Rais Samia Suluhu Hassan
 
Katika hili nampongeza sana Rais Samia kwa uwezo na ubunifu wake wa kutatua matatizo. Utumishi inakera lakini ni muhimu kuendelea kutumika kwenye ajira.

Mamlaka na taasisi zisipewe mamlaka ya kujiajiri bila mchakato wa ndani kuratibiwa na kusimamiwa na utumishi. Taasisi zipewe jukumu la kutangaza ajira na tarehe za usaili lakini jukumu la kusimamia mchakato mzima wa ajira wasipewe wao.
 
Wazo zuri sana...
 
Back
Top Bottom