Rais Magufuli waite wapinzani wako ujue wanachotaka

Naona mmeanza kuzimisi juice!
Zile zama zakupiga juice zimeisha,Lipumba mlimuona siku ile alivyoenda kwa Magu inaonekana sio juice tu hata AC ilizimwa kubana matumizi mwisho wa siku shati ndio kama vile.
Kukomesha kabisa mambo ya ndani katia kitasa kingine(Mwigulu).Bungeni Tulia uraiani Mwigilu lazima mkae!
 
Tangu raisi ameingia madarakani, ameshakutana na kada za watu tofauti na ameongea nao isipokuwa kwa upande wa wanasiasa bado.

Najua si lazima lakini kibusara kidogo angewaita akasikia maoni yao, nafikiri wana fikra nzuri tu ya kuisogeza nchi mbele ila wanapata hasira unapowapuuza. Labda tatizo vyombo vya habari vimekuwa ni wapinzani kuliko wapinzani wenyewe.

Mpaka sasa mazuri mengi umefanya ila kubwa ni hilo, kama ulivyokwishasema wewe ni raisi wa vyama vyote, basi waite hawa mabwana sidhani kama watakataa wito.
Mnatamani kwenda ikulu?
Hiyo opportunity inaweza isiwepo!
Raisi haendi kwa watu, na wala hatàki wageni kwake!
Poleni sana!
Just a joke!
Nadhani ni ushauri mwema!
Kikwete alipunguza some resistance alipokaa na kina Lisu!
Nadhani raisi anaweza akaimarisha utendaji wake kwa angalau kupokea maoni ya upinzani!
 
Hahahahahaha!!! Akili yako inaonyesha "we nataka sitaki". Hujiulizi kwa nini umejibu?

"Uchaguzi huu hatutachukuwa makapi ya CCM", tumefikiri kuwa Lowassa ndo awe mgobea wetu wa Urais!!!!!!

Kama wanavyosema ''mbecile trova un atro mbecile'' kwenye hoja hii Lowassa ameingaje? Kwani ukiwa mwana ccm ndo kujitoa ufahamu? Manake unarukia hoja ambazo hazina muungano kabisa! Pole sana!
 
Ushasema "wapinzani", kuna nini zaidi cha kujuwa na wao kazi yao kupinga tu.

Hao ikitokea siku, mchana kweupe, Magufuli akiwaambia "sasa hivi ni mchana kweupe" basi wao watakataa, watasema 'aah si kweupe, tunaona kuna mawingu ya blue"!

Hiyo ndiyo kazi yao, bila kupinga hawali.
 
Kama wanavyosema ''mbecile trova un atro mbecile'' kwenye hoja hii Lowassa ameingaje? Kwani ukiwa mwana ccm ndo kujitoa ufahamu? Manake unarukia hoja ambazo hazina muungano kabisa! Pole sana!
Naweka mifano ya aina ya watu kama wewe. Walianza akina Mbowe na kundi lake. mwisho wakamkumbatia kama koti.
 
Kwa nini wapinzani wasiombe kumwona Rais? Na sio kumweleza wanataka nini, bali wampe suggestions zao rais azipime.
 
Ushasema "wapinzani", kuna nini zaidi cha kujuwa na wao kazi yao kupinga tu.

Hao ikitokea siku, mchana kweupe, Magufuli akiwaambia "sasa hivi ni mchana kweupe" basi wao watakataa, watasema 'aah si kweupe, tunaona kuna mawingu ya blue"!

Hiyo ndiyo kazi yao, bila kupinga hawali.
Kukutana si ndio kunaleta maelewano
 
Hakuna haja ya kuwaita wapinzani bali Rais anatakiwa kutenda haki kwenye mambo ya msingi wapinzani wanayoyalalamikia
 
Naona mmeanza kuzimisi juice!
Zile zama zakupiga juice zimeisha,Lipumba mlimuona siku ile alivyoenda kwa Magu inaonekana sio juice tu hata AC ilizimwa kubana matumizi mwisho wa siku shati ndio kama vile.
Kukomesha kabisa mambo ya ndani katia kitasa kingine(Mwigulu).Bungeni Tulia uraiani Mwigilu lazima mkae!
Hahahahahaaa watamkumbuka jk! Kuna kitu hawakijui wapinzani walishaaambiwa kwamba huyu jpm si mwanasiasa ni mtendaji nadhani hawakuelewa somo
 
Tangu raisi ameingia madarakani, ameshakutana na kada za watu tofauti na ameongea nao isipokuwa kwa upande wa wanasiasa bado.

Najua si lazima lakini kibusara kidogo angewaita akasikia maoni yao, nafikiri wana fikra nzuri tu ya kuisogeza nchi mbele ila wanapata hasira unapowapuuza. Labda tatizo vyombo vya habari vimekuwa ni wapinzani kuliko wapinzani wenyewe.

Mpaka sasa mazuri mengi umefanya ila kubwa ni hilo, kama ulivyokwishasema wewe ni raisi wa vyama vyote, basi waite hawa mabwana sidhani kama watakataa wito.
Kwamba ANAWAPUUZA???????
LINI WAO WALIMHESHIMU NA KUKIRI KUWA NI RAIS WAO????? Hayo makundi anayoyaita yanamtambua yeye kama Rais wao hata kama baadhi hawakumpigia kura..ila heshima kwake ipo na INAONEKANA. .Wao wanaye RAIS WA MIOYON MWAO WAKAKAE NAYE TU WANYWE CHAI HUKO...Hakuna cha kuitwa had wakiri waziwazi kuwa ni RAIS wao
 
Hana muda wala budget ya juice...
JK aliyekuwa anawaita deile walimzawadia nini kama si maneno ya kejeli...????!!!
Ikulu ni mahali patakatifu...
Si mahali pa kupiga soga...ni kazi na kasi tu...
JPM yuko busy anasoma budget, riports za CAG etc...muda wa vikao atoe wapi?
 
Si wamekwisha sema wanakumbuka utawala wa jk, hiyo haitoshi?
 
Itakuwa na mantiki zaidi yeye akiwaita kuliko wao kuomba,

Uhalisia Wapinzani waombe kumwona Rais, kwa nini wanapenda kubembezwa? Let them be proactive and take charge for the sake of those they represent. Guys, put your egos behind and get the work done!
 
hivi wapinzani kusikilizwa mpaka waalikwe ikulu wao si wanajifanya watu wa kususa wasuse hii sio kama awamu iliyopita ambayo iliwadekeza sasa hivi ni mwendo wa kazi na kutumbua majipu
 
Back
Top Bottom