Rais Magufuli,tunakuwa sugu. Urais wako 'hautanoga' tena!

BAK mpaka Watanzania wengi tulitambue hili labda atabadili kauli zake. Kama wapo watu wanashangilia kwa kejeli na dharau zake basi ni vigumu kujitambua. Credibility yake imekwisha sio kupungua ndani na nje ya Tz. 2020 utakuwa wakati mgumu sana.
Ahsante Mkuu lakini hii inawezekana tu chini ya katiba/tume ya uchaguzi nyingine.
 
Utamu wa Urais ni kuheshimiwa,kusikilizwa na kuungwa mkono. Urais haupaswi kuogopwa kama ukoma. Urais unapaswa kupendwa,kulindwa na kujivunia. Na Rais anapaswa kuendana na hayo.

Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM,umejipambanua na hulka yako ya kusema ukweli. Unatuambia ukweli toka moyoni mwako na vile unavyoamini. Lakini,ukweli wako unavuka mipaka ya kusikilizika. Ukweli wako hujaa vitisho,'utani',ubabe na ahadi za kikampeni wakati wanasiasa wengine umewaweka pembeni hadi 2020.

Ukweli wako unatufanya tuwe sugu. Tunakuwa sugu na mikwara yako ya kufuta au kuondoa;mikwara yako ya kuzuia au kubomoa. Tunakuwa sugu na kauli zako za kuchoma bila huruma na kushona. Tunakuwa sugu na kusikia kilekile kutoka kwa yuleyule. Urais wako utapoteza ladha.

Tutakuzoea kwa matendo na maneno yako. Tutakuona wa kawaida. Rais hapaswi kuwa kama wengine. Wewe ni mtu wa kipekee,ndiye mboni na alama yetu. Usitufanye tuwe sugu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Nyumbu wewe
 
Mtapiga kelele nyingi za Kike kike
Huyu hajui Majungu,Porojo wala hizo ngonjera zenu.
Lori linakwenda
Kila kukicha mna umua ngonjera mpya hata kabla ya jana haija Futika kweli Wapuuzi awamu hii mnakazi
Huyo mwana lumumba mwenzako
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mtapiga kelele nyingi za Kike kike
Huyu hajui Majungu,Porojo wala hizo ngonjera zenu.
Lori linakwenda
Kila kukicha mna umua ngonjera mpya hata kabla ya jana haija Futika kweli Wapuuzi awamu hii mnakazi
Dawa ni kunyamaza tu maana kele zenu ndo zinamwongezea nguvu ya kufanya vizuri zaidi
 
Mm na 2020 nampa kura yangu maana huko kajamba nani bado sijaona anayefaa hata kupewa ukuu wa mkoa
 
Mtapiga kelele nyingi za Kike kike
Huyu hajui Majungu,Porojo wala hizo ngonjera zenu.
Lori linakwenda
Kila kukicha mna umua ngonjera mpya hata kabla ya jana haija Futika kweli Wapuuzi awamu hii mnakazi
UMEZALIWA NA WAKIUME TUU!!??? WATAKE RADHI WAKIKE!!
 
Muongo mwingine huyu hapa. Niwe na ID mbili hapa ili iweje!? Sifanyi huo upumbavu mie.

Mkuu unajua wewe ni mjenga hoja mzuri sana, na mwelewa wa mambo. Sasa nashangaa kwa nini siku hizi hizi tunu zako unazifuta. Pia haukuwa mtu wa kujibu hoja kwa lugha za kuudhi, mkuu. Ama siyo wewe wa awali uliyekuwa una miliki ID hii?
==============
Mimi nimehoji tu credibility na reputation za viongozi wa wale wanaohoji credibility na reputation za utawala wa awamu ya tano. Sikuhoji credibility yako! hapo mwanzo ila kwa namna fulani nimeihoji kwenye post hii.

Naomba unihakikishe kuwa wewe ndiye mmiliki halali wa ID hii toka mwanzo ili niweze kuweka sawa kumbukumbu zangu.
 
Ni sawa na mtoto,ukimchapa kila wakati,ukamtukana kila wakati,anaiona hiyo si njia ya yeye kujifunza,unamchapa halii tena,unamtukana anacheka na kulichukua tusi na yeye kuanzia kutokana wenzake.

Baada ya hapo anakuwa hakamatiki,shuleni watapiga fimbo,alishazoea,watakemea,alishakuwa sugu,
 
Sauti ya Magufuli imekua kerokubwa sana kwenye TV,kilasiku sauti ya MAGUFULI he!mara anazindua mwendo kasi anautubia,dodoma,udzm,kilimanjaro,he!kwenye ukifungua tv yeye tu,kwe nye u tube yeye sauti yenyewe mbaya kama sura yake uwiiiiii.Magufuli kanisa zote umeshikilia hadi kkkt?wewe si mroma?natarajia kukusikia mwisho wa mwezi nilivozoea kwa RAIS wote waliopita.
Makanisa yamekuwa "Viwanja vya siasa"
 
Utamu wa Urais ni kuheshimiwa,kusikilizwa na kuungwa mkono. Urais haupaswi kuogopwa kama ukoma. Urais unapaswa kupendwa,kulindwa na kujivunia. Na Rais anapaswa kuendana na hayo.

Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM,umejipambanua na hulka yako ya kusema ukweli. Unatuambia ukweli toka moyoni mwako na vile unavyoamini. Lakini,ukweli wako unavuka mipaka ya kusikilizika. Ukweli wako hujaa vitisho,'utani',ubabe na ahadi za kikampeni wakati wanasiasa wengine umewaweka pembeni hadi 2020.

Ukweli wako unatufanya tuwe sugu. Tunakuwa sugu na mikwara yako ya kufuta au kuondoa;mikwara yako ya kuzuia au kubomoa. Tunakuwa sugu na kauli zako za kuchoma bila huruma na kushona. Tunakuwa sugu na kusikia kilekile kutoka kwa yuleyule. Urais wako utapoteza ladha.

Tutakuzoea kwa matendo na maneno yako. Tutakuona wa kawaida. Rais hapaswi kuwa kama wengine. Wewe ni mtu wa kipekee,ndiye mboni na alama yetu. Usitufanye tuwe sugu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Wewe kuwa Sugu au uwe nunda utajijuwa mwenyewe.

Rais haitaji kupendwa au kuchezewa kwa kuvunja sheria.

Wewe kama unaona uraisi wake haina maana kaka pembeni.

Kama unaona huwezi kusikiliza speech yake badili channel hujazuiliwa.

Rais Magufuli hawezi kubadili na kuvunja taratibu za nchi ili wewe au Mimi tuvunje sheria kwa lengo kujinufaisha hiyo sahau kabisa.

Kama unataka kuhama nchi hama kama unataka kukaa nchini fuata sheria za nchi na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom