Franco Zetta
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 1,661
- 843
Aha! Rafiki yangu Mawazo kumbe uko kikazi zaidi ni vizuri kero nyingine mkimalizia huku huku, vilio ni vingi kila mahali kuhusu umeme kama humu nchini ndio hivi nadhani wazo la kuuza Kenya na Zambia lingekuwa Shelved kwanza Waswahili wana kuambia ukichomwa na miiba mmoja mguuni na mmoja kwenye kalio toa kwanza wa kwenye kalio ili uweze kukaa utoe wa mguuni, kwetu huku mbezi beach umeme kukatika tumesha zoea mwezi wa pili sasa imekuwa sawa na mshumaa ulio washiwa baharini,anyway niwatakie heri ktk juhudi zenu mafanikio yenu ndio furaha yetu,ina eleweka bila umeme hakuna maendeleo.mpaka sasa makao makuu yote ya mikoa 24 ya Tanzania yameshaunganishwa umeme na makao makuu ya wilaya zote 130 kati ya wilaya 133 yameshaunganishwa umeme kasoro wilaya 3 tuu ambazo ni mpya zilizogawanywa hivi karibuni.
katika miradi ya umeme vijijini mpaka kufikia katikati ya mwaka huu tayari vijiji 2000 vitakuwa vimeunganishwa na umeme wa Tanesco nchi nzima, sasa UNAWEZAJE KUSEMA TANESCO IMESHINDWA KUPELEKA UMEME VIJIJINI NDUGU? acha kupotosha wanajamvi humu