Rais Magufuli si rafiki wa vyombo vya habari

Umetumia vigezo gani kuwateua hawa mawaziri nalo ni swali? Ni bora angeuliza hivi "unatarajia nini kwa hawa mawaziri na manaibu uliowateua" au unawaeleza nini kuhusu matarajio ya Watanzania kwa serikali ya awamu ya 5. Samahani lakini. Ila waandishi wa habari tafuteni namna nzuri ya kuframe maswali ili majibu yatolewe kutokana na matakwa ya swali.
Swali zuri sana hilo; ukimuuliza swali hilo mtu kama Obama, Clinton au Tonny Blaire utawapa uwanja wa kujizolea marks nyingi sana. Unatakiwa ujibu 3 key points na kueleza kwa ufupi vigezo ambavyo ni general kama weledi,n.k.

Kiujumla rais anatakiwa kuwa mtu eloquent mwenye kuwapa watu matumaini wakati wowote sio kwenye kampeni tu.
 
Waandishi wanajikomba kwa magu
Magufuli ni
MJIVUNI ANAJIONA YEYE NDO ANA AKILI KUSHINDA WATANZANIA WOTE
Hakuna rais aliyependwa sana na watanzania kama mh kikwete..na alichaguliwa kwa landslide victory...lakini Leo hii mmmh hata mheshiwa jk anaona haya kujitokeza kwa wananchi kwa maneno machafu na kejeli anazopewa. Bado Nina wasiwasi kwa mahaba ya watanzania waliyonayo kwa mh magufuli. Naamini matumaini makubwa waliyonayo kwa huyu rais yatayeyuka na kubaki maombolezo.Ningependa watanzania tumuache afanye kazi bila kumjaza misifa isipokuwa na kichwa wala miguu ambayo matokeo yake anapata kiburi,jeuri,na kujiona yeye ndo yeye...akashindwa kufanya kazi ipasavyo na hata kutupilia mbali ushauri wa wataalam wingine wa ikulu.Sitopenda kuona mh Magufuli akimaliza muda wake kwa kujuta kuwa rais...pale watanzania watakapo mchukia kupita kiasi ..na hata mengine wadiliki kusema "afadhali ya kikwete".Let's take it simple kwa hayo anayoyafanya ni sehemu ya majukumu take.Waandishi wa habari tuandike na vitu vingine vingi vilivyopo kwenye jamii. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kiongozi with due respect unakumbuka ulituambia nini humu JF mwaka 2010 watanzania tunahitaji kiongozi wa aina gani, kama umesahau hebu tujikumbushe ulichoandika hapo chini:-

Ben Saanane 12:15 3rd March 2010
JK nimegundua ni mfuasi mkubwa wa 48 laws of power alizoandika Robert Greene.Na hasa law namba7,ya let people work for you,take credit always
Pia Magufuli ni mchapakazi sana.Nadhani pia ukaribu wake na Urafiki8 wake mkubwa na Raila Amolo Odinga wa kenya umechangia mfanano wao wa kiutendaji
Nakumbuka ile kashfa ya kumuuzia nyumba kimada,sijui ni kweli au ilitengenezwa na mtandao ktk harakati zao?
Huyu akiwa Rais Tanzania basi tutakua tumepiga hatua maanake ana kaudikteta flani hivi ambako watanzania wanakahitaji ili wafanye kazi

Watu mnajua kupekua hansard balaaa duuh..!!!
 
Mimi nadhani na anayeuliza swali alipime kwanza hajalitoa. Maswali yanayoulizwa wakati mwingine hata sisi wasikilizaji tunashangaa!! Pia sio lazima kila mahali uulize swali hata Kama umeruhusiwa. We angalia kilichokupeleka, Pima upepo, jikung'ute baada ya kumaliza endelea na safari yako.

Mhe. Rais Leo alikuwa kikazi zaidi (#HapaKaziTu)

Queen Esther

Yaani mwandishi apime upepo?

Hilo swali la "vigezo vilivyotumika katika uteuzi" huoni msingi wake? Daah!!hebu kuwa serious kidogo
 
Waulize wakenya uzuri wa katiba yetu, wansema wao na katiba yao ya kidmokrarsia imemnyima rais mamlaka, amebaki bila maamuzi.katiba yetu inamfaa sana rais magufuli.kwa katiba hii nchi za afrika mashariki zimeingiwa kiwewe, wanajua fika kuwa magufuli anawawashia indicator, ktk nishati, miundombinu, kwa ujumla sasa watajuta kuifahamu Tz
Akiondoka Magufuli (kwa namna yoyote ile) atakuja kutuongoza tena Magufuli? Au alipotutoka Sokoine, tulimpata Sokoine tena?
Kwa wenzako ameondoka Clinton, ameondoka Bush na sasa anaondoka Obama bado nchi ni SUPER POWER, ni kwa sababu ya mfumo, sio mtu.
 
Watanzania tusimlaumu sana mh raisi, tuna safari ndefu na tukizingatia hii ni Afrika. Mabadiliko ndani ya Afrika ni ngumu. Tuna hitaji elimu, busara na mshikamano ili tuweze kusonga mbele. Asie jua ni vizuri kuuliza na hata kama watu wanatoa comments bila kufikikiria ni vizuri tukaelimishana. Tunahitaji sana elimi ili tuweze kuona masuala ya mbele yetu.
Mh raisi kweli amejibu mauali ya waandishi wa habari kiukali kodogo hapo inabidi tujiulize ni kwanini kafanya hivyo, na tena kuna hao mawaziri wa zamani wako ndani ya baraza la mawaziri na huku akiwa amechukua mda mrefu kuunda baraza sasa lazima tujiulize kuna nini humo ndani ya chama na serikali?
 
Mwandishi: Siku 7 zimepita, je kodi imelipwa?
Magufuli: Kamuulize commissioner wa kodi...


Kwani nani alotoa siku 7??????????????????????????????????????????????????
 
Leo nimemuona akijibu maswali ya waandishi baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri. Pamoja na kwamba aliitisha maswali ni wazi kwamba alikuwa akiwajibu kavu wale waliouliza pamoja na waulizaji kujitahidi kuuliza maswali ya msingi.

Mtu anauliza umetumia vigezo gani kuwateua hao kuwa mawaziri. Jibu lake ni kuwa kwani nilitumia vigezo gani kumteua Majaliwa kuwa waziri mkuu? Sisi tunajuaje? Toa ufafanuzi mkuu.

Kwa mwendo huu waandishi watasusia mambo ya msingi sana na kumwachia Msigwa kutoa habari zote za Magufuli..

Kama rais hakupaswa kutoa majibu ya namna ile huju akijua hatimaye nchi nzima ingeyafahamu. Tatizo kubwa ni hulka. Kauli zile hazikupaswa kutoka kwa rais. Hata kama alihisi maswali yalikuwa ya kuudhi abgetafuta diplomatic way ya kuyajibu. Kwa namna ile anatafuta kususiwa na vyombo vya habari jambo ambalo ni hatari kwa uongozi wake.
 
wanauliza maswali laini mno hata kama ni mimi nigewajibu kihuni huni tu.

hivi kuna mwandishi angeweza kumuuliza mwalimu maghufuli hivi!

"ndugu raisi, umemteua ndugu sospita muhongo kuwa waziri wakati ankabiliwa na tuhuma za rushwa ubadhrifu na uhujumu uchumi katika serikali iliyopita. na pia maazimio ya bunge liliopita yaliitaka serikali ichmchunguze na kumpeleka kwenye vyombo vya kisheria, je ndugu raisi mwalimu maghufuli hujakiuka sheria na kanuni za utrumishi, je kwa uteuzi huu unakinzana na mamlaka ya mihimili mingine ya dola??
 
Ni kweli Magufuli ni mwoga wa vyombo vya habari ,Kikeke hakukosea kabisa aliposema jamaa kamkimbia ..

Nakumbuka siku ya uchaguzi nlimuona alivyowajib waandish wa habari baada ya kupiga kura , Kile kipande cha ile clip nakumbuka kilionyeshwa ITV ilipokuwa live Chato , na baada ya hapo hakuna channel nyingine tena iliyoonyesha , kilikuwa ni kipande cha mwisho baada ya kuhojiwa , jamaa mmoja alimuuliza , " Akishindwa uraisi atafanyaje " na kuna swali lingine pia aliuliza sema silikumbuki, alimjib kwa kejeli sana , nafikiri vyombo vya habari baada ya pale vilikatazwa kurusha kile kipande cha ile lip , maana hata ITV nao walikikata kwenye taarifa yao ya habari.

JPM ajirekebisha kauli zake kwa waandish wa habari , akumbuke watanzania tumemjua kwa kupitia vyombo vya habari , akifanya makosa au akiendelea kutumia kauli mbaya , itakuja kumrudia puan , Maneno huumba
 
Sikutarajia waandishi kujibiwa kiufupi na kimkato mnaanza kumdiss, ndo hivyoo muanze kujipanga KUSOMA NAMBA! mlijua # inayozungumziwa ni mathematics? Na bado..na hivi hamna bahasha...
 
Leo nimemuona akijibu maswali ya waandishi baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri. Pamoja na kwamba aliitisha maswali ni wazi kwamba alikuwa akiwajibu kavu wale waliouliza pamoja na waulizaji kujitahidi kuuliza maswali ya msingi.

Mtu anauliza umetumia vigezo gani kuwateua hao kuwa mawaziri. Jibu lake ni kuwa kwani nilitumia vigezo gani kumteua Majaliwa kuwa waziri mkuu? Sisi tunajuaje? Toa ufafanuzi mkuu.

Kwa mwendo huu waandishi watasusia mambo ya msingi sana na kumwachia Msigwa kutoa habari zote za Magufuli..

namuheshimu magufuli ila pale jamaa kaniboa kweli yaani anajibu kwa majivuno na dharau kweli yani, ubabe wa kizamani na wa kipumbavu kweli watu wanaoheshimu demokrasia pia wana heshimu waandishi wa habari sio kuwajibu kwa kejeli na dharau kama vile
 
Pamoja na majibu yake ambayo yamenishangaza lakini nawapongeza waandishi hawakua na hofu waliendelea kuuliza maswali...ingekua wengine wangekua na hofu...waandishi hawaogopi wanaujasiri..

Nikweli Chaupimbi, hata mimi nliliona hilo.
 
Back
Top Bottom