Ndugu Mfuasi wa CHADEMA huu ni wakati wa kusikia sauti ya viongozi wetu tu. Kile kinachosemwa na viongozi wetu wa chama ndicho sahihi, Viongozi wetu hawajavunja Katiba wala sheria yoyote ndio maana CCM wanahaha na kushindwa kupumua sawasawa. Kwasasa wameamua kutoa matusi,kukejeli na kuwadharua Watanzania wanaotaka demokrasia hai.
Mtanzania/Mfuasi na mwana CHADEMA mpenda demokrasia na haki usisumbuliwe na maigizo ya CCM, hayo tumeyazowea tangia uhuru hadi sasa. Kaa ukijua muda huu ndio vyama pinzani uchwara vilivyo olewa na CCM vitajitokeza kuitetea CCM ili waingize mkono kinywani, msiwashangae hiyo ndio ajira yao. Usishange kumwona kiongozi wa chama kingine cha upinzani akipinga CHADEMA na kuitetea CCM hiyo ndio kazi waliyopewa kufanya ndani ya Nchi, hao ni wanafiki na wasaliti.
Tuwasikilize viongozi wetu na kuwatii,ili tujenge chama na demokrasia Tanzania. Kuna asasi na makundi mbalimbali vitajitokeza kupinga na kulaani msimamo wa CHADEMA katika operesheni UKUTA, msishangae wala kutetereka hao ni wale wale wa CCM sare ndio wanavaa tofauti na hizo ndizo kazi walizopangiwa na CCM.
Tuzidi kuwaamini viongozi wetu na kuwapuuza watu wenye maneno ya uwoga ya kutia watu hofu,haki haiombwi kwa maneno tu bali kwa vitendo kama UKUTA. Kuna vyombo vya habari vipo kwa ajili ya CCM sio kwa ajili ya Tanzania mvipuuze na mkae tayari tarehe 01/09/2016 ni mikutano na maandamano ya nchi nzima.
Kuna mtindo wa Polisi kujidai kwamba wanapata taarifa za kitaalam za kiintelijensia kuhusu usalama,hasa kwenye mikutano ya wapinzani na kushindwa kupata taarifa hizo kwenye matukio ya kihalifu yanayotokea nchini kila kukicha. Tunaiomba polisi pale watakapo pata taarifa za kiintelijensia waje kwa wingi watulinde ili tufanye mikutano vizuri sio kuvuruga taratibu za CHADEMA na kuwapiga Watanzania. Nchi za wenzetu siku hizi matukio yanatokea kwasababu wanakoswa taarifa za kiintelijensia mapema, lakini kwa kuwa Tanzania tumejaliwa kupata taarifa hizo hasa kuhusu mikutano ya upinzani tunawaomba ulinzi wa kutosha.
HAPA KAZI TU imekuwa chungu zaidi ya shubiri,badala ya kufanya kazi sasa hivi ni maneno mengiiiiii ya kuwatukana wapinzani,watanzania na kuwadharau wanyonge ndio imekuwa kazi yao. Wanyonge wali ahidiwa mengi walichoambulia ni T-sheti na kofia huku maisha yakizidi kuwa magumu zaidi na zaidi. CCM ni waigizaji wanaopenda kuwa abudu watu wachache ndani ya chama. Wapuuzeni maana hata bei elekezi tu ya sukari hadi leo imewashinda kusimamia sasa wamebakia kutoa ahadi kila kukicha.Hakuna kazi wanayofanya inayosababisha wazue mikutano ya kisiasa na hawana sababu za misingi hata kidogo.
Jiandaeni kwa nguvu zote, simameni imara na msiogope chochote kile, hao mabwenyenye,maafidhina na walamba nyayo za wenzao achaneni nao. Taarifa za kupinga CHADEMA zitazidi kutolewa lakini pia mzidi kuwapuuza na mwendelee kusimamia kauli za viongozi wetu.
By Afixa
UKUTA