Rais Magufuli kwa hili umefanana na marehemu Mchonga

Huyo jamaa (freeland) yeye kazi yake ni kupinga tu hata ukweli, anataka kulazimisha mawazo yake ndiyo yawe pekee. Hata kama ametumwa basi akubali na kuelimishwa pia. Anakera sana!
Kaka nashukuru umeliona hilo. Issues nyingine mtu anaziona nonsense kwa sababu labda zinamzidi umri. Kuna watu wazima wengi tu wamenielewa kitu nilichokiandika na hawakutaka kuleta ujuaji wala dharau. Freeland ni aina ya watu ambao mawazo yao ndio sahihi na ya wengine sio sahihi.
 
Kaka nashukuru umeliona hilo. Issues nyingine mtu anaziona nonsense kwa sababu labda zinamzidi umri. Kuna watu wazima wengi tu wamenielewa kitu nilichokiandika na hawakutaka kuleta ujuaji wala dharau. Freeland ni aina ya watu ambao mawazo yao ndio sahihi na ya wengine sio sahihi.
Hata kama ni kutetea chama kwa namna hiyo haifai, awe flexible ajifunze pia.
 
Sifa moja mbaya aliyokuwa nayo mzee Mchonga (wenye umri fulani wanajua namuongelea nani), ni ule uwezo wa kumbana mtu chini kwa chini kwa kupitia lidubwana fulani hivi linaloitwa mfumo.

Mchonga alikuwa ana uwezo wa kumzuia mtu asitoke kijijini kwao, halafu anampa kazi mkuu wa wilaya kuhakikisha huyo mtu hatoki nje ya wilaya.

Mchonga akikukubali basi utaishi maisha yako yote meno 32 nje, lakini ukiingia "cha kike" halafu ukamtibua, basi tegemea kukutana na lile lidubwana la hatari.

Huyu mzee wa Chato namuona kama anayo hii tabia ya "kumminya mtu kende kimya kimya" mpaka anatoka huko alikokuwa amejificha akiwa ameweka silaha chini na mikono kichwani huku akitoa sauti kwa nguvu akisema "jamani nimeamua kwa hiyari yangu kujisalimisha"

Hii tabia ya kushughulika na adui kimya kimya haikuanza leo wala jana. Na namuona mzee wa Chato akiwa kama vile ni mtu anayezifahamu sana hulka za Mchonga, na yeye ameamua kupita mule mule.

Huyu aliyenyoosha mikono yake na kusalimu amri siku ya jana, ni kielelezo tu cha kufufuliwa kwa ile tabia ya Mchonga ya kushughulika na watu. Hatari kweli kweli.
kwanini mnamuita Mchonga?
 
Back
Top Bottom