Rais Magufuli, kauli yako inaenda kuizika elimu ya juu

Dogo, kabla ya mfumo wa udahili wa TCU online kulikua na udahili kupitia vyuoni,na baadhi ya vyuo vilikua havikudahili hadi ufanyr mtihani wao kama chuo, vingine havikua na huo mfumo.Na elim ndo hyo hyo.Mfumo wa TCU online ndo uloleta VILADHA ambao wamenyofolewa baadhi ya vyuo.Na mfumo wa TCU baadhi ya vyuo havikuupenda like UDSM so ndo wangefanyaje wakaukubali.MUM waliukataa na hawajawah kuutumia.

Labda kwa usomi wako njoo na takwimu hapa kabla ya TCU online elim ilikuwaje?Ilipokuja TCU online ikawaje?

Kisha ndo uje na hitimisho.

Halafu kuhusu ada ya maombi mbona ilikuwepo hata siku za nyuma huko?

Mfano hata kwa level ya Masters ada ya maombi hutozwa kwa kila kozi unayoomba kwa chuo husika.Kama unaomba kozi tatu na ada ya maombi ni 20,000/- bas itakutoka 60,000/-.

Tatizo hayo mambo yalikuwepo ww ukiwa bado unasoma msingi, hata TCU hukuwa unaijua na nenda kasome kazi za TCU,kazi za TCU ni kusimamia vyuo vikuu kwa mujibu wa sheria za nchi,kudahili ni kazi ya CHUO,
TCU walipora majukumu ya chuo
Umekurupuka mwenzio kaongelea bei ya sh elfu 50 ni kubwa wewe unaaongelea mambo ya zamani mfano akichukua fomu vyuo viwili ni laki moja ni kubwa sana halafu ukose nafasi wewe huoni kama ni tatizo
 
Asikudanganye MTU wengi waliopelekwa st Joseph walishindwa competition kwenye vyuo vya serikali kama udsm etc!
Nimesoma st Joseph kabla ya kuhama wengi waliopo pale tulikuwa na division three kwa upande wa science!
Sijui upande huo mwingine!
Unaweza kuwa na div 3 na ukawa upo vizur tu usikariri.Nimeshuhudia hilo kwa mtu wa karibu tu,alipata udahili State Owned University na sasa ni mwajiriwa na anafanya kazi vizur hukohuko serikalini,japo aliomba vyuo vingi ila ni hicho chuo tu KILIMDAHILI na wakat huo haikua system ya TCU,aliomba moja kwa moja ilikua kozi ya sayansi.

Pia yupo mwingine alikuwa na III ya arts aliomba kupitia TCU chuo kikuu cha serikali kikamdahili kupitia TCU na ameshamaliza shahada yake
 
Kuhusu hiyo elfu 50 ni rahisi tu; vyuo vipunguze gharama za fomu. Kama enzi za TCU ilikuwa elfu 50 then unaomba vyuo vitano; then kwa utarataibu huu "mpya" (sio mpya ndivyo ilivyokuwa zamani hizo) gharama ya fomu iwe 10,000/=; as simple as that.
Hili ndilo la muhimu, wizara ya elimu ivitake vyuo vishushe gharama ya fomu!
 
Arron Kama wewe ni mwanafunzi kweli Kama unavyosema, lazima utakubali kwamba 'no research no right to speak'

Sasa nije kwenye mjadala wako ambao umelenga upande wa uchaguzi wa chuo tuu. Lakini umesahau kwamba ulikua unachagua chuo na course unayoenda kusoma.

Hawa, TCU, walikuwa ni genge la watu waliokuwa wanadumisha malengo ya mwanafunzi, tazama, ulipo maliza la Saba ulichaguliwa ukasome nini ukamaliza form 4 ukachaguliwa ukasome nn katika combination ulizojaza, pia, ukamaliza six tena ukapangiwa ukasome nn chuo kikuu, sasa wewe utapangiwa mpaka lini?

TCU lilikua genge la wahuni wakudumaza maono tazama, kuna vijana kibao mwaka jana waliomba kusoma udaktari katika mapendekezo yao hawa TCU wakawapeleka kusomea ualimu walipotaka kubadili wakaambiwa procedure ni kubwa Sana ikafaa waache waendelee na kozi ambazo hawakuzitaka.

Kuhusu swala la gharama naomba vyuo viangalie.
 
poleni sana wadogo zangu . Yaani ni shida sijui Kama
Mh ameshauriwa vya kutosha. Sina uhakika Kama
Waziri wa elimu anatafuta ushauri wa kitaalam AMA anaongozwa na personal attitudes
Habari zenu wanajukwaa.
Hili andiko ilibidi nilipeleke jukwaa la elimu ila ni vyema lijadiliwe hapa kwa kuwa huyu anayeivuruga elimu ni mwana siasa.

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu niliyeadiliwa kwa mfumo TCU online.

Juzi baada ya jpm kutoa kauli yake juu ya tcu kuwapangia vyuo wanafunzi wasio vitaka. Ila ukweli ni kwamba tcu haiwezi kumpangia mwanafunzi chuo ambacho hakuchagua na kikubwa zaidi inamsaidia mwafunzi aliyekosa ushindani kwa vyuo ulivyovichagua. Hili linaeleweka na waliodahiliwa kwa mfumo huu watanisaidia kuongezea hapa.

Sasa baada ya kauli ya rais wakati akifungua mabweni pale udsm. Tcu wameamua isiwe shida kila chuo kipokee maombi na kupeleka tcu baadae. Kwa jicho la haraka ni kwamba wanafunzi wengi watakosa vyuo na udahili huu utakuwa mgumu sana.mfano leo chuoni kwetu wametoa tangazo la kuanza kupokea maombi na ada ya maombi ni elfu 50.

Ina maana kama unataka kuomba vyuo zaidi ya kimoja ili kujiweka kwenye mazingira ya kutokosa chuo itabidi ulipie fomu ya kila chuo.. Wakati tcu online tulikuw tunalipia elfu 50 na kuomba vyuo vitano.

Sasa ili uombe vyuo vitano itabidi utumie 250000 hapo bado huna uhakika wa kupata nafasi kulingana na ushindani wakati tcu ulikuwa unalipia mara moja elfu 50.
Mapungufu ya mfumo huu ni mengi na hapa vyuo lazima vifanye udanganyifu na kuwadahili wanafunzi wasio na sifa. Yale ya miaka ya nyuma yanajirudi.

Serikali mjirudi na tcu waendelee kufanya udahili huu.. Na mapungufu yatakayojitokeza muwahukumu hawa tcu.
 
Wakuu samahani,naomba kuuliza kwa huu mfumo mpya wa udahili,je inabidi mtu kutoka nyumbani mpaka kwenye vyuo husika ili kudahiliwa au itakuwa ni online application kwa kila chuo
 
Wakuu samahani,naomba kuuliza kwa huu mfumo mpya wa udahili,je inabidi mtu kutoka nyumbani mpaka kwenye vyuo husika ili kudahiliwa au itakuwa ni online application kwa kila chuo
Vyuo vya serikali unaombea online kupitia CAS,,ila vya binafsi unaombea vyuoni moja kwa moja. Tembelea kwenye website za vyuo husika download application form,ijaze then nenda benki kawalipe application fee yao then unaituma chuoni form yako usubir then matokeo.
 
Hili wasipoliangalia litaumiza wengi sana!
Uchague mfano udsm upigwe chini hela imeenda!
Udom upigwe chini pesa imeenda!
Muhas upigwe chini pesa kwa heri!
Wanaorudi kuumia ni wale wale watoto wa masikini
Mkuu lakini kwa sisi tuliosoma zamani nakumbuka unapokwenda kuomba nafasi ya masomo, chuo hukuelekeza aina ya kozi ambazo unaweza kusoma kwenye chuo husika. Sasa kama utalazimisha kuchagua kozi yenye ushindani mkubwa hapa ndipo unaweza kukosa nafasi na kuliwa fedha zako. Mfumo wa CAS uliwapa nafasi TCU kuwadhulumu wanafunzi nafasi za masomo na kuwapangia kozi za kipumbavu ambazo hawakuomba. Mfumo huu wa anologia utasaidia kurejesha hadhi kwa wanafunzi iliyokuwa inaporwa na matutusa wa TCU.
 
Pamoja na Mapungufu yote hayo, ni njia nzuri zaidi kwani humpa mwanafunzi wigo mpana wa kuchagua Chuo cha hitajio lake. Hutumika sana nchi za Wenzetu huko Ughaibuni.

Ili kupunguza Swala la gharama zisizo na msingi, Nashauri yafuatayo yafanyike.
Moja, gharama za fomu za kuomba Udahili ziwe bure kabisa kwa kila chuo. Hii itasaidia wanafunzi kuepukana na gharama nyingi za kuomba udahili katika vyuo vingi. Badala yake, ada ya form Tsh 50,000 ilipwe na mwanafunzi ambaye amedahiliwa na kufanikiwa kusajiliwa katika chuo tajwa. Fedha hii ilipwe pindi wanafunzi waliodahiliwa kufika Chuoni wanapowasili kwa ajili ya Usajili.

Hii ni nzuri kwani itaepusha gharama zisizo na msingi kwa wanafunzi na walezi wao. Pia, vyuo vingi vinaweza kupokea fedha nyingi kwa mgongo wa fomu ya Udahili ilihali haina uwezo wa kuwadahili wanafunzi wote hao.

Pili, kila chuo kiwe na system yake ya Udahili online. Mfano, UDOM walitengeneza system ya kudahili mwaka jana. Vyuo vyote vitengeneze website ambayo itaweza kupokea taarifa pamoja na nyaraka mbalimbali za wanafunzi wanaoomba Udahili. Hii itasaidia kupunguza gharama za nauli pamoja na matumizi mengine kwa wanafunzi. Hii itamuwia ugumu sana Mwanafunzi kutoka Kigoma mwenye nia ya kusoma vyuo vya Dar es Salaam kutoka huko mpaka huku kwa ajili ya kuomba usahili. Gharama za usafiri pamoja na malazi ni kubwa sana. Ingelikuwa rahisi kama kila chuo kitakuwa na System yake.

Nawasilisha.
Central Admission System (CAS ) Haina ubabaishaji. Kama kuliluwa na vyuo vilivyokuwa vinakapumgufu km Miundo mbinu, Waalimu nk, vijiiongeze na TCU ivikague kabla ya kupeleka Wanafunzi. Hili la Kila Chuo kudahili ndipo tulipotoka. Upendeleo na kujuana kutarudi pale pale. Mtoto wa Mkulima atadahiliwa mwishoni au kukosa maana mtoto wa Kigogo fuani lazima apate nafasi Kwanza . Huko tulitoka why go back
 
k
Pamoja na Mapungufu yote hayo, ni njia nzuri zaidi kwani humpa mwanafunzi wigo mpana wa kuchagua Chuo cha hitajio lake. Hutumika sana nchi za Wenzetu huko Ughaibuni.

Ili kupunguza Swala la gharama zisizo na msingi, Nashauri yafuatayo yafanyike.
Moja, gharama za fomu za kuomba Udahili ziwe bure kabisa kwa kila chuo. Hii itasaidia wanafunzi kuepukana na gharama nyingi za kuomba udahili katika vyuo vingi. Badala yake, ada ya form Tsh 50,000 ilipwe na mwanafunzi ambaye amedahiliwa na kufanikiwa kusajiliwa katika chuo tajwa. Fedha hii ilipwe pindi wanafunzi waliodahiliwa kufika Chuoni wanapowasili kwa ajili ya Usajili.

Hii ni nzuri kwani itaepusha gharama zisizo na msingi kwa wanafunzi na walezi wao. Pia, vyuo vingi vinaweza kupokea fedha nyingi kwa mgongo wa fomu ya Udahili ilihali haina uwezo wa kuwadahili wanafunzi wote hao.

Pili, kila chuo kiwe na system yake ya Udahili online. Mfano, UDOM walitengeneza system ya kudahili mwaka jana. Vyuo vyote vitengeneze website ambayo itaweza kupokea taarifa pamoja na nyaraka mbalimbali za wanafunzi wanaoomba Udahili. Hii itasaidia kupunguza gharama za nauli pamoja na matumizi mengine kwa wanafunzi. Hii itamuwia ugumu sana Mwanafunzi kutoka Kigoma mwenye nia ya kusoma vyuo vya Dar es Salaam kutoka huko mpaka huku kwa ajili ya kuomba usahili. Gharama za usafiri pamoja na malazi ni kubwa sana. Ingelikuwa rahisi kama kila chuo kitakuwa na System yake.

Nawasilisha.
kaka hata zamani waombaji wa vyuo kwa njia ya tcu, walikuwa wanapewa option ya kuomba chuo zaid ya kimoja, na system ilikuwa nzuri tu, ukiwa hauna sifa za kuingia chuo fulani, basi unapelekwa chaguo lako la pili, ukikosa vigezo cha pili, wanakupeleka chaguo lingine
 
Wakuu samahani,naomba kuuliza kwa huu mfumo mpya wa udahili,je inabidi mtu kutoka nyumbani mpaka kwenye vyuo husika ili kudahiliwa au itakuwa ni online application kwa kila chuo
Vyuo vingi vina website.. So cha kufanya nenda kwenye website ya chuo. Chukua fomu ya maombi jaza na uambatanishe malipo ya fomu then tuma kwa EMS itakuwa rahisi badala ya kwenda chuo
 
Mkuu lakini kwa sisi tuliosoma zamani nakumbuka unapokwenda kuomba nafasi ya masomo, chuo hukuelekeza aina ya kozi ambazo unaweza kusoma kwenye chuo husika. Sasa kama utalazimisha kuchagua kozi yenye ushindani mkubwa hapa ndipo unaweza kukosa nafasi na kuliwa fedha zako. Mfumo wa CAS uliwapa nafasi TCU kuwadhulumu wanafunzi nafasi za masomo na kuwapangia kozi za kipumbavu ambazo hawakuomba. Mfumo huu wa anologia utasaidia kurejesha hadhi kwa wanafunzi iliyokuwa inaporwa na matutusa wa TCU.
Ulichoongea ni kweli! Bahati nzuri mimi nimedahiliwa kupitia TCU!
Tuliomba wengi ukafanyika ushindani kupitia cutting point waliofanikiwa walipata nafasi!
Na ukweli vyuo ambavyo vilikuwa vinawahi kujaa kulingana na carrying capacity ya chuo ni vya serikali na vile vya private hasa kozi za afya!
Sasa TCU wanatoa majina ya vyuo vilivyobaki na kozi zilizobaki ambao hapa vingi huwa ni vya private!
Hapa sasa uchague mwenyewe mwaka upite au uangalie kozi yeye afadhali kati ya zilizobaki!
Nilikua muhanga wa hii kitu nililaumu sana ila tulipokutana na wenzangu st Joseph niligundua ufaulu wetu ulikua unaendana!
Fanya utafiti graduate wa st Joseph Nina uhakika na hili kwasababu nilipita pale kwa miezi kadhaa
 
Mkuu ameasema iwe na imekuwa. Debate ya ubora na ubovu wa maamuzi hayo yameandikwa sana (Jukwaa la Elimu na Siasa). Michango ya kufanyike nini ili vijana wengi wapate wanachotaka itasaidia. Na wale watakao kosa wanachotaka raundi ya kwanza wasaidiweje? Tangazo la NACTE halina raundi ya pili na sidhani kama TCU nao wameweka raundi ya pili. Watakao chaguliwa itabidi wahakikiwe na NACTE/TCU -sijui watatumia mfumo gani? Baada ya raundi ya kwanza 2016/17 waombaji zaidi ya 20000 walikosa-ni kiasi gani ya hawa walikosa kwa sababu ya "matatizo" ya TCU? Bila raundi ya pili ambayo siioni mwaka huu hawa 20000 wangekwenda wapi? Je raundi zaidi ya moja inawezekana nnje ya CAS? Wizara, TCU, NACTE na vyuo wanatakiwa wawe makini hapa vinginevyo kutawaka moto. Nawakilisha
 
Unaweza kuwa na div 3 na ukawa upo vizur tu usikariri.Nimeshuhudia hilo kwa mtu wa karibu tu,alipata udahili State Owned University na sasa ni mwajiriwa na anafanya kazi vizur hukohuko serikalini,japo aliomba vyuo vingi ila ni hicho chuo tu KILIMDAHILI na wakat huo haikua system ya TCU,aliomba moja kwa moja ilikua kozi ya sayansi.

Pia yupo mwingine alikuwa na III ya arts aliomba kupitia TCU chuo kikuu cha serikali kikamdahili kupitia TCU na ameshamaliza shahada yake
Ni kweli unaweza pata three ila ukawa vizuri kichwani!
Sasa TCU watajuaje wewe upo vizuri kichwani wamuache aliyepata division one wakuchukue wewe?
Kwa huyo wa three art kupata chuo cha serikali inategemeana na kozi aliyoomba + carrying capacity ya chuo husika!
Kama hakuna mwenye ufaulu wa juu kwenye kozi husika hata kama una three unachukuliw
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Umekurupuka mwenzio kaongelea bei ya sh elfu 50 ni kubwa wewe unaaongelea mambo ya zamani mfano akichukua fomu vyuo viwili ni laki moja ni kubwa sana halafu ukose nafasi wewe huoni kama ni tatizo
Bei ya TCU ni 50,ooo lakini bei ya maombi chuoni haitafika 50,000/- muda.
Nakupa mfano,USDM maombi ya Masters ni 20,000/- je unadhan ya UNDEGRAGUATE ITAFIKA 50,000/-.Subirini muda wa maombi ndo mtoe malalamiko,
Halaf bado elf 50 si nyingi mdau kwenye elimu,
 
division 3 mtoto wa kigogo atasoma udsm na mkopo atapewa 100% afu wewe division 1 mtoto wa baba kayumba utasoma kayumba university na mkopo utapewa 60%
Jamaa yangu katika familia anatoka familia maskini tu,alipata three na akadahiliwa chuo cha serikali na akapata mkopo 100% na sasa ameajiriwa serikalini,huyu alidahiliwa na mfumo wa chuo kabla ya TCU kuanza.
 
Back
Top Bottom