Rais Magufuli iokoe Tanganyika kwa mateso, sisi sio Wazanzibar

nakupa salamu, natumai umzima wa afya.
mh Magufuli ulipigiwa na kura na watanganyika wengi na wazanzibar wachache (source NEC) uchaguzi kwa mujib wa waangalizi wa ndani na nje kwa asilimia kubwa wamesema ulikuwa huru na haki. sasa mh Magufuliunajua bajeti yetu karibia asilimia 40 tunapewa na marekani, pamoja na jumuia ya ulaya sasa wote hawa wanatuangalia kwa jicho la jazba. MCC imezuiliwa, ambapo sisi wavijijini lilikuwa tumaini letu kupata umeme, sasa tutakaa kizani kwasababu ya wazanzibari?
mh Magufuli kwanini tuitese Tanganyika kwa makosa ya wazanzibari.

Mh raisi chukua hatua, kuwa juu ya chama, agiza viongozi wa Zec wakamatwe, omba Umoja wa mataifa usimamie mazungumzo kisha isimamie uchaguzi mpya ujao wallah utakumbukwa milele

kama ushauri huu utapuuzwa, kweli CCM watashinda 100%, kisha serikali ya umoja wa kitaifa itakufa then mtanadili katiba ili kurudisha muundo wa zamani, basi hapo hatma ya zanziba itakuwa inaelekea kuzimu, chuki, ibaguzi, utazidi sana.
Ni hayo tu mh.
shukran.
Acheni UJINGA hakuna cha mazungumzo MAALIM SEIF atangazwe mshindi tu....Yaani uniibie halafu unasema tuzungumze nini....!!! miaka yote CUF waliwashinda lkn walionyesha uungwana wakiamini iko siku mtawahwshimu....Kumbe walikosea mnawaona maBWEGE nw hawakubalia tena...mpeni MAALIM ushindi wake maisha yaendelee
 
Kwani umeambiwa kuwa Rais Magufuli anategemea kuendesha serikali yake kwa misaada ya wahisani? Ameshakuambia kuwa Tanzania tutakuwa wafadhili wa nchi nyingine
Duh wewe kubwa LA minyumbu uchumi gani wa kujitegemea kuendesha TBC tu unakushinda yaani bora usiandike uharo kunuka dah ccm kuwa na watu kama nyinyi hasara
 
mm sio mzanzibari sasa Tanganyika tunaumizwaje? mwenye haki yake apewe
mkuu ni kweli wewe na rais wako sio wazanzibari lakini sielewi kwa nini mnakua na kimbelembele juu ya maswala ya Zanzibar..
eti rais wa Zanzibar lazima akubalike dodoma kabla ya kua rais..
mapato ya foreign exchange,utalii,bandari kutoka zanzibar jioni yahesabiwe na kuhakikiwa na TRA bara..
mabilioni ya hela za Zanzibar kwenye benki ya East Africa,kabla ya EAC kuvunjwa,yameyeyukia BOT..
Wazanzibar mliwafata kuforce Muungano..
na wakinyanyua kauli ya kutaka muungano uvunjwe nyinyi ndio mnalaani..
mkuu mmeyataka wenyewe..
 
Siku zote mlikuwa mnatamani Rais super kama Magufuli. Mmempata na sasa mnatamani mlikotoka. Kweli mmekuwa kama wafuasi wa Musa vile!
Si kutamani tuliko toka bali anakumbushwa atimize wajibu wake kwa manufaa ya wa Tanganyika.Kwa kuwa iwe kwa haki au batili yeye sasa ni Raisi wetu, anapaswa kulinda maslahi yetu kwa namna yoyote.
 
kwa hali ya zanzibar ilivyo maghufuli hawezi tatua huo mgogoro kamwe...
Si kweli kuwa hawezi, inaonekana Magu anatanguliza mbele masilahi ya Chama chake, CCM na sio kumtanguliza mbele Mungu wake kama anavyotuasa sisi wadanganyika. Au kutanguliza masilahi ya Taifa.

Aliwahi kusikika akisema, "Dawa ya jipu ni kulitumbua, na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu. Najua kutumbua jipu kuna maumivu lakini bahati mbaya halina dawa nyingine. Hivyo ninaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote mniombee na muniunge mkono wakati natumbua majipu haya."
Pia Magu alisema yeyeatakuwa mkweli, atasema kweli, hapendi unafiki na hawapendi wanafiki, msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Baada ya miezi mitatu na ushee wa mkwamo, Magu ameashauri mchakato wa mazungumzo ya mkwamo yaendelee, Mazungumzo nayo yamekwama au yamekufa. Magu amekuwa bubu,.Magu haonekani ana nia na dhamira ya dhati ya kutenda haki ili kumaliza mkwamo.

Tunamuombea kwa Mungu lakini hili jipu la Jecha na unafiki wa CCM Zanzibar ameamua kuyafumbia macho ili asiyaone na anajaribu kuepuke kulitumbua jipu.

Tumkumbushe tu, Magufuli hawezi kujigeuza mbuni kuzika/kificha kichwa mchangani, wakati mwili wote uko nje unaonekana.

Kwa kupoteza muda zaidi bila kuwachukulia hatua JWTZ waliositisha utangazaji wa matokeo ya uchaguzi na kutengeneza mkwamo, anatufanya tuamini kuwa ameamua kuungana na wanafiki na wanaosema serikali haitolewi kwa vikaratasi.

CCM wanasherehekea miaka 39 ya ung'anganizi wa madaraka, miaka 20 ya ubakaji wa demokrasia Zanzibar na kuwaletea wadanganyika "maisha bora"(kuwagawia umasikini).

Link ZanziNews : Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Shein Azinduza Sherehe za Miaka 39 ya CCM Zanzibar.
 
Aondeshe jwtz mengine tutamaliza wenyewe. Lakini hata hili litamshinda.

Katika mambo ya muungano tulyokubaliana mojawapo ni JWTZ.Hilo ni jeshi la muungano kuliondoa Zanzibar ni kuvunja katiba halitoki ng`o.
Hilo swala la uchaguzi wa Zanzibar halimuhusu Magufuli kabisa sababu si jambo la muungano.Linaihusu nchi huru ya Zanzibar tu.Hana ubavu wa kuliingilia kati kwani yeye kwa maswala ya Zanzibar hilo halimhusu.Wazanzibari mkitaka pelekeni mswada wa kubadili katiba ili raisi wa muungano awe na uwezo wa kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar kama mnataka Magufuli aingilie kati na mmruhusu pia aingilie kati na yale mafuta ya pemba
 
Katika mambo ya muungano tulyokubaliana mojawapo ni JWTZ.Hilo ni jeshi la muungano kuliondoa Zanzibar ni kuvunja katiba halitoki ng`o.
Hilo swala la uchaguzi wa Zanzibar halimuhusu Magufuli kabisa sababu si jambo la muungano.Linaihusu nchi huru ya Zanzibar tu.Hana ubavu wa kuliingilia kati kwani yeye kwa maswala ya Zanzibar hilo halimhusu.Wazanzibari mkitaka pelekeni mswada wa kubadili katiba ili raisi wa muungano awe na uwezo wa kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar kama mnataka Magufuli aingilie kati na mmruhusu pia aingilie kati na yale mafuta ya pemba
Kwa nini JWTZ ilitumika kubaka demokrasia Zanzibar?


Link Msaada: Nini kitatokea iwapo CUF hawatashiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar?
 
Kwani umeambiwa kuwa Rais Magufuli anategemea kuendesha serikali yake kwa misaada ya wahisani? Ameshakuambia kuwa Tanzania tutakuwa wafadhili wa nchi nyingine
Sio rahisi hivyo, sasa hv kabla ya march mambo yatakuwa magumu take my note.
 
Yaani wakati mwengine mwanadamu ni zaidi ya mnyama.

Linapokuja suala la Zanzibar utaona maajabu mengi hapa TZ. Wasomi wanakuwa mbweha mla watu, wanasheria wanakuwa kuku kwa kusahau, na waliobaki wote hujitowa fahamu.

Yaani Jeshi la JMT litumike kupora haki ya uchaguzi kwa Wazanzibari lakini wakati huo huo, Amir Jeshi ashindwe kuwa sehemu ya utatuzi yaani aah?

Haya mambo tulisema zamani Zanzibar imetumika kama mtaji wa Bara kwea jina la Muungano na kuitumia kulinda Maslahi yake.

Mpaka sasa kwa hili la Uchaguzi Wazungu wameliona hilo. Acha tufaidi MATUNDA YA MAPINDUZI. ACHA TUGAWANE FAIDA NA HASARA.
 
Hili la uchaguzi CCM imedekezwa mno. CCM Zanzibar na Tanzania inadekezwa na wasomi wetu na wanasheria, mahakama, vyombo vya dola, na makundi ya kijamii.

Kule Zanzibar katiba imevunjwa wazi, kwa makusudi kumetengenezwa mgogoro na hakuna anaenyoosha kidole. CCM wanahusika kwa asilimia 100%, ndio wameshika dola, hatima yake wanaleta ubaguzi, wanapiga watu, wanavunja sheria na katiba kwa wazi, wanafanya wanavyotaka hawaulizwi. Hakuna wa KUWAULIZA.

Acha Tanzania ionje machungu ya DEKO la mtoto wake CCM, CCM isiyo na makosa wala isiyoonywa. Na CCM wa Zanzibar amezidi DEKO. Tuendelee kumpa PIPI adeke zaidi.

Msilalamike pazeni sauti haki itendeke

Kwa hili angalau Hongera ,
Membe, Butiku, Salim na UKAWA.
c c

Warioba, UDSM, LHRC, Wanasheria nguli, Viongozi wa dini, Maraisi wastaafu na wengineo

"Kujitowa fahamu hakusaidii"
 
Nakupa salamu, natumai umzima wa afya Mh. Magufuli ulipigiwa na kura na watanganyika wengi na wazanzibar wachache (source NEC) uchaguzi kwa mujibu wa waangalizi wa ndani na nje kwa asilimia kubwa wamesema ulikuwa huru na haki.

Sasa Mh Magufuli unajua bajeti yetu karibia asilimia 40 tunapewa na marekani, pamoja na jumuiya ya Ulaya sasa wote hawa wanatuangalia kwa jicho la jazba. MCC imezuiliwa, ambapo sisi wavijijini lilikuwa tumaini letu kupata umeme, sasa tutakaa kizani kwasababu ya wazanzibari? Mh Magufuli kwanini tuitese Tanganyika kwa makosa ya wazanzibari.

Mh rais chukua hatua, kuwa juu ya chama, agiza viongozi wa ZEC wakamatwe, omba umoja wa mataifa usimamie mazungumzo kisha isimamie uchaguzi mpya ujao wallah utakumbukwa milele

Kama ushauri huu utapuuzwa, kweli CCM watashinda 100%, kisha serikali ya umoja wa kitaifa itakufa then mtanadili katiba ili kurudisha muundo wa zamani, basi hapo hatma ya zanziba itakuwa inaelekea kuzimu, chuki, ibaguzi, utazidi sana ni hayo tu mh.

Shukrani.
Mara hii watu mmeanza kujinasibu nyinyi Watanganyika wao Wazanzibar..Duh??!!
 
Kwani umeambiwa kuwa Rais Magufuli anategemea kuendesha serikali yake kwa misaada ya wahisani? Ameshakuambia kuwa Tanzania tutakuwa wafadhili wa nchi nyingine
Chini ya "UTAWALA" wa CCM kuwa wafadhili wa nchi nyingie hilo kamwe halitaweza tokea hata miaka 1000.
Chini ya "UONGOZI" wa vyama vingine,Tanzania inaweza kuwa "SUPER POWER" kwa miaka 30 tu.
 
Mkuu, unataka ushahidi gani zaidi ya upuuzi mwingi uliokuwa unaandika humu dhidi ya Rais Magufuli? Pitia mada zako za nyuma utaona ulivyo mpuuzi
We jamaa huna kazi aisee...mbn kila muda unaandika shit..! kubali kupokea mawazo tofauti na yako. Jukwaa hili linaharibiwa na nyinyi kwa kuendekeza uchama..Tanzania ni kubwa kuliko vyama vyenu. Nakubali maisha ni siasa but siyo kishabiki in that extent. Magufuli akiendeleza nchi faida kwa wote sio Ccm..na akiharibu ni kwa wote sio wapinzani. kuwa objective usiwe ambaye huna hoja unadharaulika humu
 
Back
Top Bottom