Rais Magufuli hana sera yoyote ya kukuza uchumi, yupo yupo tu huku uchumi ukiteketea kwa kasi!


Uko sahihi kabisa mkuu. Watu wanajua kulalamika na kutoa negatives tu bila kutoa maoni mbadala. Sasa mtu kama huyo ataendeshaje biashara au kampuni wakati akipata kimsukosuko tu kidogo ananza kulalamika.
 
Hii inamaa auchumi tuliokuwa nao haukuwa halisi, kulikuwa kuna uwezekano wa kupata kipato pasipo kuzalisha au kutoa huduma, au kukwepa kodi,mianya hii inapozibwa lazima kutakuwa na mshtuko wa uchumi, ambao hauna madhara kihalisia, ila sasa tutakapo kaa sawa, kipato kitakuwa kinapatikana kwa njia zinazofahamika tu, either uzalishe, au utoe huduma, na utalipa kodi, hapo ndio tutakpoona ushindani wa kweli, na uchumi wetu utakuwa halisi.
 
It hurts but ain't working!
 
Ndo kishakuwa Rais, Pole sana kwa kutokuwa na kura ya veto ambayo ingekuwezesha kumzuia Kikwete kuwa Rais!
We mtu wa pwani mimi nimesema namzuia kuwa rais? mimi nimekanusha andiko lako kuwa tuta miss utawala wa kikwete, mimi nikakuambia madhaifu yake yaliyotufikisha hapa, taarab ya nini?
 
Aa
Tatizo la magu anajiona ana akili kuliko watu wote hivyo hawezi kukubali ushauri Wa mtu yeyote. Ukilshauri kinyume na mawazo yake unatumbuliwa
Na kweli kabisa ana akili na kama inamtosheleza yanini achanganye???????????????????????????????
 
Hoja haina mashiko. Watu waliokuwa wanafanya kazi na makampuni ya wasafirishaji makontena bila kulipia ushuru unadhani wataenda wapi?

Watu wamezoea njia za mikato, itachukuwa muda lakini kama taifa tuko kwenye mstari sahihi.
 
We mtu wa pwani mimi nimesema namzuia kuwa rais? mimi nimekanusha andiko lako kuwa tuta miss utawala wa kikwete, mimi nikakuambia madhaifu yake yaliyotufikisha hapa, taarab ya nini?

Wapi niliandika mtamiss?
 

Nakuona unaandika huku umekunja mdomo,unasndika kwa shinikizo la njaa tu,kwa sasa mnatumia mabaki ya akili za Dr.Slaa zikiisha mtaaibika.
 
Serikali au kiongozi yeyote duniani sifa kuu kwake ni uchumi imara baas!! Shida ni kwamba kwa muda mrefu tumekua tukiimba pambio za ufisadi na kuacha ajenda kuu ya uchumi!!

Magufuli naye kaingia madarakani kadaka agenda za majipu ambayo now yamerudishwa serikalini kinyume nyume huku kukiwa hakuna hatua madhubuti za kuokoa uchumi!!

Nchi zote duniani uchumi ndio ajenda kuu ya nchi kuliko chochote ila hapa tunakazana na mauzo na kutokelezea kwenye media!!

Uchumi nchi nyingi unaanguka!! Nigeria nimeona biashara zinaanguka uingereza viwanda vinaanguka so ni suala mtambuka ila hapa kwetu hakuna jitihada zozote zaidi ya mashairi tu kwamba majipu yakiisha uchumi utapaa!!!
 
Mkuu next time uje na facts and figures.
Sector binafsi wapo ambao wamefanya redundance baada ya kubanwa kodi so profit margin inashuka lazima ulayoff.Kuna jamaa zangu haya yamewasibu.
Kwa mbinyo uliopo wa serikali ya JPM ugumu wa maisha lazima uongezeke kwa sababu ela za magumashi hazipo tena kwa kiasi kikubwa.
Pia NIDA alitimua watu kazi hawa nao wanaongeza ugumu wa maisha mtaani maana watu kama 500 ila sababu kubwa ya kuwapunguza ni ufanisi kwa mujibu wa msemaji.
Kwa kifupi matumizi ya contractionist monetary policy in a short term impact zake ndo izo ila long term savings zikitumika vyema zikatumika kujenga viwanda vidogo vya kati na vikubwa in a long term mambo yatanyooka.
Cha msingi tulipe kodi tuu ili serikali ipate hela angalau kwa sasa nina imani kapu la hazina ela iko salama kwa kiasi kikubwa ata nami nimeanza rasmi kulipa kodi kwa imani iyo.
 
Elimu Elimu Elimu!!

Sera ya Ukawa kwenye uchumi ni ipi?
Wewe kweli jina lako linakufaa sana-JINGALAO! Huwezi kujenga Uchumi bila elimu bora. Mataifa yaliyoondelea yanaweka msisitizo katika elimu kwa sababu bila kuwa na advanced technology hakuna Uchumi. No education no technology and henceforth no economic growth. Do you understand?
 
Ulikuwa umezoea vya kufisadi sasa umekwama sio. Utasemaje uchumi umedoroa kwa kipindi kifupi hiki wakati sera ni zile zile. Wewe unazungumzia mzunguko wa fedha za madawa ya kulevya na ufisadi kama bandarini, wafanyakazi hewa, vikao na safari hewa nk.
 
Haya ndiyo mabadiliko ya kweli ya kimfumo wa ukusanyaji kodi. Hapa inadhihirisha kuwa hata kampuni yako nayo iliishi kijanjajanja maana isingeathirika. Kuwa mpole fuata sheria ya kodi tuinue uchumi.
Kwa uzoefu wetu hiki kilio cha maisha magumu huwa na matokeo chanya kwa wanaojibidisha katika kazi. Sasa hivi wale waliokuwa wakiishi kwa upambe wa wenye hela za wizi huwa wanalia kwa kelele kubwa sana Rais asisikie kilio chao aweke pamba masikioni.
 
Mkuu mpaka mfumo ukae sawa tutaumia kwa muda ujanja ujanja ulizidi mjini lakin pia ....
Mfumo ukae sawa lini? Ugiriki waliamini mfumo utakaa sawa mpaka Leo patupu!! Na tusichokijua njia/mbinu za uchumi za karne ile zinazotumika sasa zimefeli sehemu nyingi tu!!

Nigeria mzalishaji Mkubwa wa mafuta uchumi wake unayumba!! Nimeona viwanda vya vitenge vimegeuka machaka uzalishaji umekoma!!

Binafsi namsifu JK ukiacha makando kando mengine kwenye uchumi alijitahidi sana hasa kukuza uhimilivu!! Dunia ya Leo mbinu za kusimamia uchumi zinatakiwa kubadilika kulingana na wakati na mazingira kwa hilo JK alimudu!!

Kumbuka tunachofanya sasa ni pata potea!! Ukisema tutakaa sawa bila kujua lini ujue fursa zenu zinachukuliwa na wengine!!

Kadiri uchumi wa dunia unavyoyumba tukicheza zaidi hapa tutalia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…