Rais Magufuli azungumzia Umeya wa jiji la Dar

Namuona Emmanuel Buhohela pale kapiga suti kwenye team ya Waandishi wa Habari wa Ikulu...Safi sana kijana kwa kutumia fursa,hii ndio kusema hata yule bwana mdogo Spencer Lameck kama Mzee wa Monduli angeshinda basi dogo angekuwa Magogoni anakula upepo..Mshahara wa Mzee Machache ndio basi tena

Kuhusu suala la Umeya Dsm:Tunarudia tena kusema...Demokrasia na maendeleo huenda sambamba,huwezi kuhubiri kasi ya maendeleo bila kuzingatia demokrasia.Nchi zote zilizoendelea zilienda pamoja na vitu hivi;yaani maendeleo na Demokrasia.Ni muhimu viongozi wa Afrika wakaheshimu uwepo wa "Political Pluralism"

CCM waheshimu maamuzi ya wana Dsm,Tunajuwa kuwa moja ya sababu ya uchaguzi kuwekwa kesho ni kufifisha swala la mazingaombwe na uchaguzi wa Znz,lkn tunajuwa jinsi Masaburi na mafia wenzake toka South Africa wanavyohakikisha Meyor hatoki UKAWA ili kulinda ufisadi wa UDA,DART na viwanja vya wazi ufukweni na mitaani.Baada ya uchaguzi kupita Rais atatangaza Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni,na UKAWA watapokwa Wilaya ya Kinondoni na umeya wao utaaenda Wilaya mpya ya Ubungo,na baada ya hapo hesabu zao za kuficha maovu ya Kinondoni utakuwa umepona.CCM huwa hawafanyi jambo bila mahesabu
Tunarudi pale pale, aibu hii ipo chini ya Tamisemi, ofisi iliyoko chini ya Rais. Hayakujaulikana yote haya hadi leo?

Hizi ni siasa za ajabu sana, baada ya mazingaombwe ya ZNZ sasa wanarudi kutuambia ni aibu. Hawatuambii nani kasababisha aibu hii. Hata Umeya hatuwezi kufanya!

Kwakweli aibu hii ipo chini ya ofisi yake, hakuna namna ya kuieleza bali kusema ukweli
 
Alikuwa wapi muda wote huo bila kuzungumzia chochote kuhusu hili suala la Umeya wa JIJI,ni vizuri kama angetueleza zichukuliwe hatua kwa yule Mkurugenzi na Mwanasheria wa JIJI ambao walijitoa ufahamu na kutoa zuio feki la Mahakama.
Anakomaa taratibu. Kauli yake ya kuheshimu demokrasia ichukue mkondo wake imenipa matumaini kuwa anaanza kukua. Heri nusu ya shari kuliko shari kamili! Sikuwa ninafikiria JPM anaweza kuzungumza lugha kama hii!!
 
Polisi MTU asichezee na silaha yako.....marufuku kumsogelea askari akiwa na silaha.....
 
Mkuu wa nchi viongozi wa CCM ndio hawataki Demokrasia kila uchaguzi wanakimbilia mahakamani mpaka wanagushi mazuio Feki polisi Na pccb wamekaa kimya
 
Akizungumza mara baada ya kukamailisha zoezi la uhakiki wa silaha zake.

Rais amesema suala la umeya wa Dar ni aibu kila siku kuahirishwa na kusisitiza ni lazima demokarsia iaachwe ichukue mkondo wake kama ni CCM basi iachwe ishinda na kama ni CHADEMA nayo iachwe ishinde..

Unaweza kubofya hapa chini kuona yote Rais aliyoyasema


propaganda at its best!ila ana onekana anaweza kucheza na miguu ya kuku
Alikuwa wapi muda wote huo bila kuzungumzia chochote kuhusu hili suala la Umeya wa JIJI,ni vizuri kama angetueleza zichukuliwe hatua kwa yule Mkurugenzi na Mwanasheria wa JIJI ambao walijitoa ufahamu na kutoa zuio feki la Mahakama.
ukiona hivyo ujue maji yamezidi unga
Hapa Magufuli kaonyesha Uzalendo Wa Kisiasa...Hata Zenji angefanya Hivii Hakika Mungu angempa pepo ya milele
dhubutuu yake!ukiona hvyo ujue mpango ushapangwa wakupindua matokeo ya umeya,tangu lini simba akamwoa huruma salwa?
 
Anakomaa taratibu. Kauli yake ya kuheshimu demokrasia ichukue mkondo wake imenipa matumaini kuwa anaanza kukua. Heri nusu ya shari kuliko shari kamili! Sikuwa ninafikiria JPM anaweza kuzungumza lugha kama hii!!
Lakini inabidi uchukue tahadhari sana. Mimi nadhani bado kuna kitu kipo nyuma ya pazia ambacho kimepangwa. Kwanini? Kwa sababu hili ni suala linalojulikana na rais kwa muda mrefu. Na anajua ukweli. Na anajua hata uchaguzi ungefanyika leo kwa uhuru ni nani angeshinda. Lakini matokeo yake tuliona mpaka mawaziri wake wenye heshima zao kama mzee Mahiga wakibebwa kwenda kupiga kura ya umeya na wakakubali kupelekwa kama mafurushi. Ina maana rais alijua kwa undani ni nini walitaka kufanya. Leo ghafla amegeuka na kusema eti demokrasia ichukue mkondo wake. Alikuwa wapi siku zote? Au ni malaika Gabriel amemtokea leo?
 
Unafk ukiisha Tanzania nchi itasonga... Na hatuwez kusonga kwa ccm kuendelea kubaki madarakani
Sidhani kama shida ni CCM kutoka madarakani. Shida ni kuacha demokrasia halisi ifanye kazi yake. Maendeleo yataletwa na watanzania wote - CCM, CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF, ACT WAZALENDO na hata wale wasio na chama.
 
Back
Top Bottom