Rais Magufuli awaapisha wajumbe wa Kamati Maalum ya kuchunguza sakata la mchanga wa migodini

Hivi kwani huo "mchanga" wa awamu zilizopita na hii ya sasa una utofauti!!!
 
Mimi nashauri kamati teule kumwaga makontena yote chini ili kujiridhisha na kilichokuwemo isije kuwa vipande vya dhahabu vimechanganywa na mchanga ili kuvisafirisha kwa udanganyifu.Bora kuingia gharama ili ukweli ujulikane.
 
Soma TEITA Act 2015, mikataba (MDAs/PSAs) yote ni subject to disclosure. muwe mnasoma kabla ya ku-comment. Businessas usual is nowhere accepted in Tanzania as of now.
hata kama unaipenda sana ccm ficha upumbavu wako. ccm mmetuingiza mkenge,
 
Cheezeeni wote sio wazungu,hata chupi tunaagiza nje,halafu tunahangaika na mchanga huyu kiongozi anatupoteza ,hayo madini yenyewe hata kuyatumia hatuwezi,Sera ya viwanda imemshinda,katumbua wote wameisha,sasa kahamia kwa wazungu wa madini
 
Mkataba ambao watangulizi wake waliingia na hayo makampuni unasemaje? Hata kama ni mkataba wa kutuibia madini yetu, lakini unasemaje?

Ukishajiuliza hayo maswali utagundua kwamba approach anayotumia mkuu siyo sahihi. Angeenda kwenye mkataba kisha akakaa nao mezani na kuona namna ya kubadili mkataba
Aende mezani atapataje kiki ( umaarufu) huyu mkuu wetu anapenda sifa kutoka kwa wananchi. Yani kama hivi alivyotangaza mchanga unaenda kukaguliwa anajua mambumbumbu yatalipuka kwa furaha rais ndo huyu. Bila kuwaza terms za msingi katika huo uchimbaji wa madini.
 
Serikali ya Magufuli sio serikali ya kujadiliana na wakwepa kodi....hilo labda mgelifanya ninyi wazungusha mikono ambao kiongozi wenu ni mmoja wa wakwepa kodi wakubwa nchini.[HASHTAG]#HApaKazitu[/HASHTAG]
Si tupo.unawaita wakwepa kodi .subiri mkuu tutapata majibu hapa hapa na serikali itaaibika.
 
Tatizo lingine kubwa ninaloliona kwenye hii tume ni presha watakayokuwa kuwa nayo kutokana na mategemeo ya Magufuli kwao. Inavyoonekana tayari rais ana majibu yake ambayo anayataka kutoka kwa hiyo tume.nimemsikiliza vizuri sana akiongea baada ya kuwaapisha. Kazi kwao . hii haina tofauti na lile agizo alilowapa majaji kuwa wakitaka awape pesa wafunge mafisadi.
 
Ndugu wewe ndio hujaelewa...
Mpaka hapo hajavunja mkataba Bali amesitisha usafirishaji wa huo mchanga on grounds that,Wazungu wamekuwa wakitudanganya kuhusu kiwango cha Dhahabu kilichomo kwenye mchanga huo. Hiyo tume imeundwa sio kuangalia mkataba isipokuwa kupima kiwango cha dhahabu.
Kwa karibu miaka ishirini wamekuwa wakidai wanasafirisha Shaba na fedha na kiwango kidogo sana cha Dhahabu 0.02-0.05g/t ya mchanga baada ya kuwa wamechimba.
Ukisoma taarifa ya ACACIA ndio utashtuka sana.
Leo ndio wanatangaza kuwa 30% ya mapato ya kampuni wanapata kwenye usafirishaji.
Kumbuka wamesema ktk madini wanayochimba 95% ni dhahabu na 5% ndio Shaba na fedha na kadhalika. Sasa jiulize iweje 5% ya madini wanayochimba ichangie 30% ya mapato!??
Kuna Maelezo kwamba 70% ktk ile 95% yavDhahabu hupatikana mgodini na 25% hupatikana baada ya kusafirisha mchanga
Sasa jiulize 25% ndio 0.02-0.05gm/t.
Kama haitoshi wanadai kupoteza $1,000,000/= kwa siku ambayo ni sawa na billion 2.2/day!!!!
Hata wakilipa kodi ya 3% ni zaidi ya 66million kwa siku kwa mchanga pekee. Kwa mwaka ni kiasi gani?
Ndugu huu mchanga kabla ya kusafirishwa nje wataalamu wetu hapa nchini wanapitia vipimo vya kilichomo ndani au huwa unapita free tu pale bandarini bila kufanyiwa ukaguzi?
 
Kwenye Mfumo wa Utawala Ulio makini huhitaji Tume wala Kamati. Wizara husika ingekuwa tasked kuleta majibu ya Maswali yaliyopo na Mapendekezo kwa Mheshimiwa Raisi.
Ukisikia taasisi inaunda Kamati Ujue Watu wameshindwa Kuwajibika kwenye majukumu yao. Chini ya Wizara ya Madini na Nishati, kama hakuna majibu ya kile kinachotafutwa, Hakuna sababu ya Wizara kuwepo,na pesa za walipa kodi wanazolipwa zitakuwa zinapotea.
Mkuu unadhani professor Muhongo hana majibu? Anajua kila kinachoendelea na ndio maana hata alipokatazwa mchanga usitoke kule mtwara alipuuzia rais kashikwa na hasira akamfukuza Katibu mkuu kazi.
Magufuli anachotaka yeye ni kuambiwa kuwa mchanga wetu unaibiwa na madini mengi ili apate umaarufu kwa wananchi hivi bado hujamjua huyu babu kipara anavyopenda sifa?
Hiyo tume imepewa maelekezo ya kufanya na ni mategemeo ya Magufuli majibu yake kwamba tunaibiwa ili spate cha kusema.
Mikataba mibovu wanashindwa kushughulikia wanahangaika na mchanga.
 
Mkataba ambao watangulizi wake waliingia na hayo makampuni unasemaje? Hata kama ni mkataba wa kutuibia madini yetu, lakini unasemaje?

Ukishajiuliza hayo maswali utagundua kwamba approach anayotumia mkuu siyo sahihi. Angeenda kwenye mkataba kisha akakaa nao mezani na kuona namna ya kubadili mkataba
Kwa hiyo tu3ndelee kuibiwa tu


Nahis wengine humu ni waarabu au watanzin wa kihindi sio bure
 
Rais Magufuli awaapisha wajumbe wa Kamati Maalum

Hongera Rais, tunasubiri majibu ya tume yako na ile ya bunge japo nadhani mnayochunguza yaweza pishana kidogo.
Mkimaliza hili msisahau tunasubiri kwa hamu sana ya miaka tele kujua mikataba yetu ya madini inasemaje, hata usipotupa kusoma utwambie tu mkuu.
Ila mwisho wa siku hata kama kamati ikigindua tunaibiwa madini mengine kwenye huo mchanga, mikataba would be the one to blame and not Accaccia or other miners. This implies, useme kweli kuwa serikali iliyopita na ya Mzee wa kubinafsisha anko Ben ndio waliosababisha haya na kupelekea wewe uunde hiyo kamati. Wewe ni msemakweli? Acha siasa kwenye hili usimung'unye maneno.

Labda niulize, Kwenye hotuba yake kwa kamati amesema pia, nanukuu, "tunataka tujue kama hatuibiwi hatujaibiwa kiasi gani". Mwisho wa kunukuu"
Hapa kiswahili chake ameniacha, why would the comittee waste time doing this?
 
Mkataba ambao watangulizi wake waliingia na hayo makampuni unasemaje? Hata kama ni mkataba wa kutuibia madini yetu, lakini unasemaje?

Ukishajiuliza hayo maswali utagundua kwamba approach anayotumia mkuu siyo sahihi. Angeenda kwenye mkataba kisha akakaa nao mezani na kuona namna ya kubadili mkataba
Hapa sijui kama mkulu wangu wa nchi yule wa awamu ya tatu atachomoa maana kwa kumbukumbu zangu hii issue ya mchanga ndio ilianza.
 
Back
Top Bottom