Chakochangu
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 2,668
- 2,164
Mimi ni mwalimu katika shule moja morogoro wilaya ya mvomero,
Nilifungiwa mshahara wangu tangu mwezi wa tisa.
Kosa langu lilikua ni kutofika kazini kwa siku 20, lakini walinisamehe kwa kunionya na adhabu yangu ikaisha mwezi wa 12 mwaka jana,
Tangu mwezi wa 12 mshahara wangu sijaupata na sasa hivi mshahara wa mwezi wa pili sijapata,.
Nimefuatilia halmashauri mara nyingi napewa majibu mepesi ambayo hayaendani na maswali yangu.
Ambao mnauelewa kuhusu hili naombeni msaada wangu ili niweze pokea pesa zangu za miezi miwili,.Kwa maana nipitie njia gani niweze pata hela yangu kiwepesi.
Natanguliza shukrani kwa wanajamvi wote mtakao guswa na kuweza nisaidia kimawazo kuhusu hili.
Karibuni wanajamvi.
Vipi mkuu South Africa huendi siku hizi?