Rais Magufuli anaingia kwenye vita kali

Ujinga sa ya kwenda tu.washatupiga sana sasa inatosha.nilikuwa najiuliza hizi nchi za east africa kutupita kiuchumi ilhali cc tuna kila kitu...leo ndo napata jibu...dah nasema inatosha
 
Katika kitu ambacho mapebari hawana mchezo nacho ni maslahi yao. Ukitaka uone michezo yao haramu ingilia maslahi yao.

Angalia nchi kama Venezuela, South Sudan, Libya na nyinginezo.Kosa la viongozi wa nchi hizo walichofanya ni kusimamia haki.

Kiongozi akijifanya "anajua" kuliko wao,wanapambana nae kwa njia za ajabu.Unashangaa maisha ya wananchi yanakua magumu mno, export haziuziki, thamani ya hela inaporomoka, wananchi maksudi kwa kutojua wanafikiri kosa ni la rais wao kwa hiyo anaonekana hafai kabisa.

Anatengenezwa ''kiongozi" mwingine ambaye yeye anakua anasimamia maslahi ya mapebari mambo yanaendelea kama kawaida.

Mimi sitoshangaa kama Rais Magufuli atatawala awamu moja tu,yote itakua ni kulipa gharama ya kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi, kwa bahati mwenyewe analifahamu hili.

Rais komaa hapo hapo wananchi tuko nyuma yako.
sasa mbona kama haueleweki unaunga mkono kinamna gani??
 
Kwa nini tunawasingizia sana wazungu?! Kungekuwa na nia ya dhati ya kukomesha huu wizi kwanza tungeondoa zile kinga za kutoshitakiwa walizojiwekea mafisadi wakuu. Hatua zote zingeenda sambamba na kuwawajibisha vikali watanzania wote vibaraka walioshiriki na kufanikisha kuiuza nchi yetu. Na hapa namaanisha marais wote waliosimamia udhalimu huu, mawaziri husika, watendaji waliohusika, viongozi wa vyombo vya usalama walioacha kuilinda nchi yetu wakakomaa kuilinda ccm.... Hao walafi hawakutimiza wajibu wao, walizembea na kushiriki kuirarua nchi hii. Ajabu zaidi, bado taifa hili linawagharimia kwa kila kitu kwa lugha ya pensheni!!!
 
Katika kitu ambacho mapebari hawana mchezo nacho ni maslahi yao. Ukitaka uone michezo yao haramu ingilia maslahi yao.

Angalia nchi kama Venezuela, South Sudan, Libya na nyinginezo.Kosa la viongozi wa nchi hizo walichofanya ni kusimamia haki.

Kiongozi akijifanya "anajua" kuliko wao,wanapambana nae kwa njia za ajabu.Unashangaa maisha ya wananchi yanakua magumu mno, export haziuziki, thamani ya hela inaporomoka, wananchi maksudi kwa kutojua wanafikiri kosa ni la rais wao kwa hiyo anaonekana hafai kabisa.

Anatengenezwa ''kiongozi" mwingine ambaye yeye anakua anasimamia maslahi ya mapebari mambo yanaendelea kama kawaida.

Mimi sitoshangaa kama Rais Magufuli atatawala awamu moja tu,yote itakua ni kulipa gharama ya kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi, kwa bahati mwenyewe analifahamu hili.

Rais komaa hapo hapo wananchi tuko nyuma yako.
Rais Bush Jr alipokuja Tanzania alisema wanachukia viongozi wanaowaibia watu wao. Nasi tunasema tunachukia nchi tajiri zinazoibia nchi maskini. . Nina imani pesa chafu haiwezi kukubalika Norway na Sweden. Sasa mbona USeA, Canadua, Australies waliko hawa Barriki n miti hii fake ya Migunga Nk wanatuibia sisi nchi maskini
Katika kitu ambacho mapebari hawana mchezo nacho ni maslahi yao. Ukitaka uone michezo yao haramu ingilia maslahi yao.

Angalia nchi kama Venezuela, South Sudan, Libya na nyinginezo.Kosa la viongozi wa nchi hizo walichofanya ni kusimamia haki.

Kiongozi akijifanya "anajua" kuliko wao,wanapambana nae kwa njia za ajabu.Unashangaa maisha ya wananchi yanakua magumu mno, export haziuziki, thamani ya hela inaporomoka, wananchi maksudi kwa kutojua wanafikiri kosa ni la rais wao kwa hiyo anaonekana hafai kabisa.

Anatengenezwa ''kiongozi" mwingine ambaye yeye anakua anasimamia maslahi ya mapebari mambo yanaendelea kama kawaida.

Mimi sitoshangaa kama Rais Magufuli atatawala awamu moja tu,yote itakua ni kulipa gharama ya kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi, kwa bahati mwenyewe analifahamu hili.

Rais komaa hapo hapo wananchi tuko nyuma yako.
 
Unajua kwa nini nchi Kama China ilitoa kauli kama "Atakayeigusa Tanzania tutamshughulikia" wakati manowari Yao ya Kijeshi ilipotembelea Tanzania!?
Duh, kwa hiyo Watanzania hatuna wasi wasi tena baada ya kumpata bwana mpyaaa...yaani ujeuri wote huu ni kwa sababu tunamtegemea Mchina kutuliwaza! Makubwa!
 
Katika kitu ambacho mapebari hawana mchezo nacho ni maslahi yao. Ukitaka uone michezo yao haramu ingilia maslahi yao.

Hii ni nusu kweli lakini si kweli kamili. Si mabepari tu wasiokuwa na mchezo na maslahi yao, hata wajamaa na wakomunisti kama kina Nyerere, Fidel Castro, Stalin, Mugabe n.k. hawana mchezo na maslahi yao.

Hivyo ni vizuri kusema watu wengi hawana mchezo na maslahi yao.

Angalia nchi kama Venezuela, South Sudan, Libya na nyinginezo.

Venezuela imefika hapo kwa sababu ya sera za kijamaa na utaifa (Nationalism) za Chavez ambazo na sisi tunaelekea huko (tulitoka huko kipindi cha Nyerere, leo tunarudi). Venezuela sasa raia wengine wameshaanza kuvunja sanamu za Chavez. Uchumi umekufa.

South Sudan tatizo si mabepari na tupende kuangalia kwenye kioo kabla ya kunyoosha vidole. Ukabila baina ya waDinka na waNeur haujaletwa na mabepari.

Libya tatizo ni mtu kujimilikisha nchi.

Kosa la viongozi wa nchi hizo walichofanya ni kusimamia haki.

Leo hii Maduro (dereva wa basi) anaua raia kutumia Collectivos (zao la Chavez). Hakuna haki anayosimamia.

Ghadafi kasaidia waasi wangapi hapa Afrika? Raia wake wangapi kawapoteza. Naelewa hapa Ghadafi anachukuliwa kama nusu mungu. Kaa na mlibya muulize kuhusu utawala wake kama ulikuwa wa haki au mabavu.

Salva Kiir huko Sudan sijui ni haki gani anasimamia.

Tusiseme kwa ujumla tu kwamba kiongozi akipambana na “mabepari” basi anasimamia haki. Si kweli. Kiongozi anaweza kupambana na “mabepari” na asisimamie haki. Mfano Mugabe hasimamii haki japokuwa anapambana na “mabepari” (wa kizungu, si wa kichina).

Kiongozi akijifanya "anajua" kuliko wao, wanapambana nae kwa njia za ajabu.

Dunia ya sasa kama kampuni ya kigeni inadanganya hapa hata huko kwao inashtakiwa na kulipishwa faini. Hivyo kama kampuni imedaganya hapa na kwao inabidi tupeleke mashtaka na wafikishwe kunakostahili.

Kuna wazungu wanaamini ubepari ni ushetani na kwa ishu kama hii wanaishikilia bango kuhakikisha kampuni inalipa fidia kwa mabaya yake.

Si mabepari hao hao wameleta chenji za rada? Si mabepari hao hao wametushtua skandali ya EGMA/BOT?

Vita yoyote ile ni kujipanga na kufanya vitu kwa akili na si hisia au mihemeko. Tatizo ni pale unapokuwa hujajipanga na/au silaha (ripoti) zako hazijitoshelezi kwa sababu unataka kusikia kile unachoamini.

Mwisho wa siku tunashindwa vita na tunalaumu wengine.

Unashangaa maisha ya wananchi yanakua magumu mno, export haziuziki, thamani ya hela inaporomoka, wananchi maksudi kwa kutojua wanafikiri kosa ni la rais wao kwa hiyo anaonekana hafai kabisa.

Ningependa kutumia mfano wako huu na hii ishu ya sasa. Kwa kila maamuzi kuna mabaya na mazuri yake. Mazuri yanatakiwa kuwa makubwa kuliko mabaya hususani kwa kipindi kirefu. Tusipate faida kwa kipindi kifupi halafu hasara kwa kipindi kirefu.

Sasa unapokemea “wizi” (si mahakama imehukumu) na kabla hata ya kusikiliza upande wa pili (law of natural justice) tayari unatoa picha kwamba una upande umeegemea.

Mwekezaji (“mwizi”) ataogopa kuendelea kubaki hapa na kufunga kiwanda/kampuni. Watu watakosa kazi. Upande wako utashangilia huibiwi tena. Upande mwingine wananchi wamekosa kazi.

Je, hapo nani anafaidika? Je, kuna njia ya kuzuia wizi huu bila kiwanda/kampuni kufungwa na wananchi wako wasikose kazi? Je, wakikimbilia mahakama zao na kushinda kesi kisha kufunga kiwanda/kampuni si sisi tunaumia kwa kukosa kazi na kulipa fidia? Je, waki

Mwekezaji (“mwizi”) huyu ndiyo mojawapo ya pesa za kigeni. Leo hii ukimkimbiza bila kupata mwingine au kuwa na mbinu mbadala za kufidia pesa za kigeni tutakayopoteza, wakulaumiwa ni mwekezaji hapo?

Maswali kama hayo na mengine mengi inabidi tujiulize na kutengeneza ramani ya vita vizuri ili tusile matapishi yetu baadaye.

Mwisho wa siku unaweza kuwa unaamini unafanya sawa na kupata popularity kubwa lakini unashangaa uchumi unakufia. Mfano Nyerere.

Anatengenezwa ''kiongozi" mwingine ambaye yeye anakua anasimamia maslahi ya mapebari mambo yanaendelea kama kawaida.

Hii pia ni nusu kweli lakini si kweli kamili. Wapo wanaotengezwa na viongozi wengine wanaoamua kusimamia maslahi ya nchi pale wanapoona uchumi unakufa.

Hivyo hii ya kubandika watu vilemba kwamba huyu “kiongozi” kachongwa na mabepari haifai. Tusikilize hoja na tujadili, tusivishe watu vilemba. Tutajenga authoritarian regime mbaya.

Ubaya ni kwamba kwa sasa mwenye hoja tofauti na mkuu anaonekana analipwa na hawa mabepari na hivyo hapaswi kusikilizwa.

Mimi sitoshangaa kama Rais Magufuli atatawala awamu moja tu,yote itakua ni kulipa gharama ya kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi, kwa bahati mwenyewe analifahamu hili.

“Vita” hii ikisababisha maisha ya wananchi yawe magumu tusilaumu “mabepari”. Kama kiongozi anapaswa kujipanga na kujua apambane vipi ili faida iwe kwetu na si kwa “mabepari”.

Rais komaa hapo hapo wananchi tuko nyuma yako.

Mwisho wa siku tusijemchongea sanamu na kuivunja mbeleni.

Kwa sasa yoyote mwenye kuipinga hiyo ripoti ataambiwa amehongwa na si mzalendo.
 
Kwa hiyo Rais hajui kilichoko kwenye mikataba ama sijakuelewa?

Na washawasha!

Mi nadhani badala ya kusifia tuwe makini kufanya analysis kuwa Je maamuzi haya hata kama ni ya kizalendo Je yatatunufaisha au ndio kuchochea kuni zaidi za kujiteketeza wenyewe..
Mi naona ni bora ingefanyika anaysis tujue kwa kuchukua maamuzi haya ni kwa kiasi gan tuna-gain na ku- lose
Unajua bila kufanya hv tutajikuta kila kitu tunashangilia huku hatujui nin kipo kwenye mikataba na hata hatuna huo uezo wa kujiendesha wenyewe.. Mi nadhan hii mentality ya kuwaona waliotutangulia walikuwa wapigaji si sawa sana
 
Back
Top Bottom