Rais Magufuli amsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa DART

ningefurahi sana kama muhongo angesimamishwa kuwa waziri wa nishati...

Weeeeee acha hizo bana, yaani jembe hili lisimamishwe??!! you are not serious!! kakubania kwenye vitalu vya gesi nini, au kule kwenye madini!!
 
Hii nyinine ya 2012, Raia Mwema - Bosi wa Mabasi ya Kasi Dar ang’oka


Ni baada ya shaka ya matumizi ya mabilioni
OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi jijini Dar es Salaam (DART), Cosmas Takule, aliyekuwa akisimamia mradi wa ujenzi wa barabara za Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi bilioni 240.9, ameondolewa katika wadhifa huo, Raia Mwema, limethibitishiwa.
Hatua hiyo inajitokeza miezi miwili baada ya Rais Jakaya Kikwete kutilia shaka matumizi ya shilingi bilioni mbili zilizoombwa serikalini kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha muda, eneo la Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Rais Kikwete alisema kutumia Sh. bilioni mbili kujenga kituo cha muda cha mradi huo Chuo Kikuu, halafu baada ya miaka miwili kipatikane cha kudumu, si maarifa sahihi, kwani yanachangia kupoteza fedha za serikali.

Rais Kikwete alitia shaka hiyo alipozindua mradi huo Septemba 19, mwaka huu na kusema; "Jawabu lenu la kujenga kituo cha muda Chuo Kikuu siliafiki. Hakuna kujenga cha muda. Ujenge cha muda leo, miaka miwili ijayo unapoteza fedha za Serikali. Fanya uamuzi wa kudumu sasa.

"Wiki ijayo, kwa kuwa wewe ni Mwenyekiti (Mkuu wa Mkoa), mwite Mkurugenzi wa DART. Kama akikataa mwambie sawa, lakini mimi ni Mkuu wa Mkoa. Mkurugenzi wa DART, Tanroads na wewe mkae, mzungumze. Wiki inayofuata mniletee majibu, mmekubaliana nini, " alisema Kikwete.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia uamuzi huo wa kumng'oa ofisa huyo mkuu unahusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi ambazo hata hivyo, yeye amezikana, akisisitiza amekuwa akifanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa.

Mbali na tuhuma za ufisadi, Takule anadaiwa kufanya kazi kwa kupuuza ushauri wa maofisa wenzake katika mradi huo na hivyo kuondoa dhana ya uwajibikaji wa pamoja.
Mmoja wa maofisa wa DART ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini anamzungumzia Takule akisema; "….baadhi ya wageni walikuwa wakifukuzwa kama mbwa, hakutaka ushauri, watumishi ni kama walilala wakiwa wamefungwa minyororo , hivi hapa ni kama tunajipanga upya (baada ya kuondolewa Takule)."
Lakini katika maelezo yake kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwake, Takule anasema; "Agosti mwaka huu niliandika barua kwa ofisi ya Waziri Mkuu kuarifu kumalizika kwa mkataba wangu Novemba 8, mwaka huu, barua ambayo haikujibiwa.

"Nimekabidhi ofisi baada ya mkataba wangu wa miaka mitano kwisha. Mwaka 1979 hadi 2004. Nimetekeleza miradi mikubwa hapa nchini tukianzia na mradi wa Uimarishaji wa Huduma Mijini (USRP), uliojenga miundombinu ya barabara, majitaka katika miji yote mikubwa Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro , Moshi, Iringa, Tanga, Tabora na Dar es Salaam."

Kwa mujibu wa maelezo yake miradi yote ambayo amekuwa akiisimamia imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa na hapakuwa na ufisadi wa aina yoyote.
"Sijawahi kukumbwa na kashfa yoyote maishani mwangu,"alisema Takule.
Kutokana na kuondoka madarakani, Novemba 9 mwaka huu, Takule alikabidhi ofisi kwa Asteria Mlambo, anayekaimu wadhifa huo wa Ofisa Mtendaji Mkuu.

Asteria ambaye kabla ya kukaimu nafasi hiyo alikuwa Mkurugenzi wa Usafirishaji na Maendeleo DART, anasema hatua iliyochukuliwa ni uamuzi wa kawaida.
"Kilichofanyika ni utaratibu wa kawaida, ni muda gani nitakaimu nafasi kwangu si tatizo, ninachozingatia ni namna gani shughuli zinafanyika.

"Kwa nafasi hii niliyopewa kwangu ni heshima, mtu ambaye nilipuuzwa kipindi chote, ninayo matumani makubwa kwamba serikali imeniamini. Naamini sana kwenye utendaji wa pamoja ndani na nje ya DART. "Hakuna kitu kibaya unakaa kwenye taasisi kipindi chote na hakuna kinachofanyika. Mradi unahitaji mazingira ya uwazi ili watu waweze kuelewa yanayotendeka, hiyo itawasaidia wadau wengine kuelewa namna watakavyoweza kushiriki kwenye mradi husika," alisema katika mahojiano na Raia Mwema, ofisini kwake.
Kuhusu kauli ya Kikwete kuhoji matumizi ya shilingi bilioni mbili anasema; "Lile agizo na maelezo ya Rais yametusaidia sana. Tumejenga fikra mpya za pamoja. Wengine walidai kuwa Rais alishauriwa vibaya, si kweli kuwa alishauriwa vibaya bali sisi wenyewe tulikuwa na upeo mdogo katika ubunifu wetu kiasi cha kujijengea taswira ya ubadhirifu."

Alisema pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik , Meya wa Jiji hilo Dk. Didas Masaburi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda wanajipanga kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha mabasi ya mikoani.

Kwa mujibu wa maelezo yake, eneo hilo lipo Mbezi, barabara ya Morogoro ambako kama watafanikiwa kituo cha mabasi Ubungo kitahamishiwa Mbezi badala ya kujenga kituo cha muda cha mabasi eneo la Chuo Kikuu.
Mradi wa mabasi yaendayo haraka ambao unatarajiwa kubadili mandhari ya Jiji la Dar es Salaam utakuwa na mtandao wa barabara zenye urefu wa kilomita 137, unajengwa kwa awamu sita.
Awamu ya kwanza yenye urefu wa kilomita 20.9, inayohusisha barabara za Kimara – Kivukoni , Magomeni –Morocco na Fire –Kariakoo – Kivukoni. Mradi huo unagharamiwa na Benki ya Dunia kwa kiasi cha Sh bilioni 240.879, ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia kwa wenye maeneo yaliyokumbwa na mradi.
- See more at: Raia Mwema - Bosi wa Mabasi ya Kasi Dar ang’oka
 
Huo ni ushabiki wa kitoto tuu, siasa /management na kemia ni vitu viwili tofauti

Mwana sayansi yoyote yule ana uwezo mkubwa wa kiakili (IQ) na kutatua matatizo klk Mwanasiasa na mwandika makala magazetini kama Ulimwengu, hivyo analoliona Mkemia wetu mwandika makala magazetini kama Ulimwengu hawezi kuliona!
 
Nadhani sasa atangaze kuwa watebdaji wakuu wote hamna kazi aweke wengine.

Sasa hivi wale ambao hawajafikiwa ni wasiwasi na kazi haziendi.

Mzee Pombe hebu asome makala ya Ulimwengu katika gazeti la Raia Mwema Leo inaweza kumpa mwongozo

Kama tu pana ufujaji na uhuni wowote acha tu watumbuliwe ..
 
Nadhani sasa atangaze kuwa watebdaji wakuu wote hamna kazi aweke wengine.

Sasa hivi wale ambao hawajafikiwa ni wasiwasi na kazi haziendi.

Mzee Pombe hebu asome makala ya Ulimwengu katika gazeti la Raia Mwema Leo inaweza kumpa mwongozo

Siye hatutaki nadharia zake bana, sisi tunataka kuona kazi tu ikifanyika site
 
Kemia ya ubaoni au IPI?


attachment.php

 

Attachments

  • Mkemia.jpeg
    Mkemia.jpeg
    8.7 KB · Views: 1,944
Nadhani sasa atangaze kuwa watebdaji wakuu wote hamna kazi aweke wengine.

Sasa hivi wale ambao hawajafikiwa ni wasiwasi na kazi haziendi.

Mzee Pombe hebu asome makala ya Ulimwengu katika gazeti la Raia Mwema Leo inaweza kumpa mwongozo
Hilo gazeti na huyo mwandishi si ndio wana Chadema walisema gazeti la kufungia nyama,hatuwezi kumsikiliza Jenerali Ulimwengu kwani yeye bado ana mitizamo tofauti na Magufuli,ingekuwa busara azidi na kubaki kushauri gazeti lake ili ili lisiwe gazeti la ''kufungia nyama''na sio lazima kila wakati tufuate ushauri wa Jenerali Ulimwengu.
 
Wale wa machozi band watakuja na kukebehi...Mwaka huu hakuna huruma ni kutumbuliwa!

Na yule kichaa wao anaye jiita Ulimwengu ni wa kupuuzwa..!
 
Nadhani sasa atangaze kuwa watebdaji wakuu wote hamna kazi aweke wengine.

Sasa hivi wale ambao hawajafikiwa ni wasiwasi na kazi haziendi.

Mzee Pombe hebu asome makala ya Ulimwengu katika gazeti la Raia Mwema Leo inaweza kumpa mwongozo
Hamna muda wa kupoteza na porojo ni muda wa kazi tu tatizo la bongo much know ni wengi sana kila mtu anajifanya mtaalamu that dude can't tell magufuli shit sababu hayuko kwenye system hajui hali halisi ilivyo ndani ya system hii nchi inahitaji boosting kubwa ili ikae kwenye position nzuri ya kufuata trend ya uhakika kuelekea kwenye maendeleo ya haraka ukisema mtu aanze kudili na mfumo usiku utaingia sababu process ziko too complicative na huku maisha yanazidi kuwa magumu na uchumi unazidi kudorora anachofafanya Magufuli ni sahihi kabisa #HAPA KAZI TU#
 
Kwa kweli hii kasi ya Magufuli ni Noma, ametutaka Watanzania TUMWOMBEE!!!!!!!

Hiyo siyo kasi bhana. Hizo ni preparation za kasi. Kuondoa watu walioshindwa kudeliver bado siyo kasi stahiki. Tumpe muda ili atimize azma yake !
 
Kama tu pana ufujaji na uhuni wowote acha tu watumbuliwe ..

Hilo nalikubali kabisa ila tujiulize ni CEO gani katika mashirika ya umma ana nafuu? Kama wapo ni wachache sana. Sasa kuliko kusubiria mmoja mmoja awaondoe wote na kuweka wapya
 
Back
Top Bottom