Rais Magufuli amfukuza kazi katibu tawala wa mkoa wa Mwanza

Magufuli fukuza,fukuza kila mtu kisha weka watu wako wa kanda ya ziwa na wasukuma wenzio.dalili tumeziona zipo waaazi kabisa.
muda wa kusoma political game utafika tu.
 
Kwa kufuata hoja zilizotangulia inaonyesha kulikuwa na MAUMIVU YA MUDA MREFU,au NANI WA KUMFUNGA PAKA KENGELE,kutokana na hulka ya RC,kila mtu alikuwa fed,kiasi cha mtu mwenye taaluma yake anaona "to hell" for anything happen!kwa kuchoshwa kwa vitisho na kutaka kukaliwa kichwani kila uchao.(kwani mtu akiwa hata kama hana nguvu lakini mbabe kila siku akiwa anakanyaga au kumtonesha kidonda kwa makusudi iko siku atapata nguvu tu ya kumdhibiti mtemi wake na watu watashangaa)na mtu akiwa tempered kiasi hicho atafanya jambo ya kustaajabisha na kufedhehesha maana subira/busara yote hupotea,ndio maana tumesikia watu huua familia nzima baadae hujuta.Huyu Bwana mkubwa ni Mwonevu na Mchokozi na wa kwanza kushtaki akijua husikilizwa either ana tabia ya kuchonganisa kwa kupenda kutoa taarifa kwa mabwana wakubwa za kweli/uongo aonekane mwema(MNAFIKI),na Kipindi cha nyuma ukijikombakomba mara unaukwaa ukuu wa wilaya/mkoa kama bwana Mmoja alivyomchapa vibao waziri mkuu mstaafu hadharani na kwenda kulamba viatu kwa kumfuga kamba za viatu mtoto wa bwana mkubwa akaukwaa utwana!viongozi wa namna hii hujitahidi kwa utendaji wa kimajungu kuliko kiutendaji kukaa kwenye usukani,ni shida na janga ila all in all 'kwenye ukweli uongo ujitenga ila utachukua muda"na haki haipotei!
 
Kwa kufuata ethics za uongozi kwa kitendo cha kunyanyua kiti kwa dhamira ya kumdhuru boss wako au hata mfanyakazi w chini yako whether wewe ndio ulichokozwa au la! Ndani ya kikao cha kikazi.....Papo hapo unaondolewa na aliekuteua kwenye nafasi hiyo.

Kwa nini iwe hivyo? Maana yake uko pale kumwakilisha yeye....yaani RAS alikuwa anamwakilisha Rais, maana yake ni kwamba Rais alinyanyua kiti kwa dhamira ya Kumpiga RC

Tuanzie hap....

Baadae sasa ndio tutafute fact ili kuona Mulongo pia atachukuliwa hatua gani kwa kuwa chanzo cha RAS kupandwa jazba ili mteule mwingine Asije yeye kunyanyua meza kabisa kutaka kumdhuru RC.
Magu kukurupuka sana kumtimua huyo jamaa kama ni hivyo alitaka awaite awasikilize na atoe maamuzi maana haiwezekani mtu ayenyuke na kiti bila sababu aidha kuna chuki binafsi kati ya Magu na huyo RAS hiyo imetumika kama sababu.
 
Magufuli fukuza,fukuza kila mtu kisha weka watu wako wa kanda ya ziwa na wasukuma wenzio.dalili tumeziona zipo waaazi kabisa.
muda wa kusoma political game utafika tu.
Sasa hiyo gross misconduct ulikuwa unataka aachwe? Unamrushia boss wako kiti? Inaweza kuwa kweli Mulongo anamakosa ila Kuna more civilised ways to point out his weaknesses. Plus wasukuma na watu wa Kanda ya ziwa ni Watanzania, mbona haulalamiki ndio Kanda inayoongoza kwa kuchangia pato la taifa? Au umesahau mchango wa samaki, dhahabu, almasi? Regardless kabila la mtu wasukuma wanastahili pia kama watanzania wengine.
 
Tuache kushabikia maamuzi ya kijinga, jazba na kukurupuka ya Magufuli, kwa sababu Tanzania ni nchi inayopaswa kuongozwa kwa SHERIA, KANUNI na TARATIBU. Hatupaswi kuongozwa kwa Hisia, imani au Fikra za kimaamuzi za Magufuli.
Katika sakata hili dosari kuu ni hizi
1/Hakukuwa na Nature Justice yoyote(Mtuhumiwa hakupewa nafasi yoyote ya kusikilizwa)

2/Hakuna ripoti yoyote ya wazi au Usawa iliyotolewa kuhusu Tukio hilo la Kikao.
3/Hakuna uchunguzi wowote huru kuhusu tukio hilo.
 
Kwa kufuata ethics za uongozi kwa kitendo cha kunyanyua kiti kwa dhamira ya kumdhuru boss wako au hata mfanyakazi w chini yako whether wewe ndio ulichokozwa au la! Ndani ya kikao cha kikazi.....Papo hapo unaondolewa na aliekuteua kwenye nafasi hiyo.

Kwa nini iwe hivyo? Maana yake uko pale kumwakilisha yeye....yaani RAS alikuwa anamwakilisha Rais, maana yake ni kwamba Rais alinyanyua kiti kwa dhamira ya Kumpiga RC

Tuanzie hap....

Baadae sasa ndio tutafute fact ili kuona Mulongo pia atachukuliwa hatua gani kwa kuwa chanzo cha RAS kupandwa jazba ili mteule mwingine Asije yeye kunyanyua meza kabisa kutaka kumdhuru RC.
Yeye mulongo ndiyo alianza kumpiga kwa chupa ya maji na mwenzake akajibu mapigo kwa kuchukua kiti
 
Hii nchi ina vyeo vingi mno. Vipunguzwe.

Kuna sababu gani ya kuwa na RAS au DAS kwani hao ma-DC na ma-RC wana kazi zipi ngumu.
 
Kwa kipengele kile kile Mulongo nae uteuzi wake unapaswa kusitishwa mara moja...hafai kuwa kiongozi maana hana leadership ethics wala skills. Nadhani baada ya investigation kukamilika na fact kama hizi (kumrushia chupa ya maji) kuthibitika Rais hatasita kumwajibisha asipowajibika mwenyewe.

Nimefanya kazi serikalini kabla kuingia kwenye international organisations kuna tofauti kubwa sana ya utekelezaji wa kanuni za maadili kwa watendaji wa Serikali....ingawa kanuni zote zinakaribia kufanana sana maana zote ni zao la ILO.

Yeye mulongo ndiyo alianza kumpiga kwa chupa ya maji na mwenzake akajibu mapigo kwa kuchukua kiti
 
IKU1.jpg

Hakuna Ubaguzi uliofanyika kwenye kikao cha KUU Mwanza ,soma Taarifa ya KUU Mwanza
 
Attachments

  • Taarifa kwa umma KUU Mwanza.pdf
    25.3 KB · Views: 103
Back
Top Bottom