Rais Magufuli amdhalilisha Meya wa UKAWA Manispaa ya Ilala

Kosa lingine, ashuriwe vizuri. Mpaka sasa rais ametenda mazuri mengi mabaya ni kiduchu.
 
Thats why chiz Trump anaonekana kusema kweli kwenye upuuzi wake.... yaani chizi anasema upuuzi ambao unakuwa wa kweli kwa viongozi fulanifulani Africa...... sijui hawa binadamu wanasali makanisa gani yanayo wafundisha haya... ubaguzi ubaguzi ubaguzi.....
 
Tuliokuwa Kinyerezi tuliulizana sana,kwanini Rais ambaye husema atawaongoza watu wote bila kujali itikadi analeta ubaguzi wa viongozi mbele ya wananchi?Kauli ya kuwa hawezi kumpa chakula mtoto wa jirani wakati wake yupo ina maana gani kwa Watanzania waliochagua vyama pinzani?
Kwa kweli ile hatua ya kumruka yule Dada wa viti maalumu wa Chadema wakati alikuwepo jukwaani haikuwa nzuri...Lkn Meya alikuwa amekaa karibu kabisa na Mbunge Bonna Kaluwa,lkn Rais akamruka na kuanza kashfa....chuki za hivi sio nzuri kabisa...Kuanza kudhalilisha viongozi wengine kisa si wa chama chako inapunguza heshima fulani kwako wewe unayefanya tabia hiyo...Ndio tumekubali kasi yako,lkn UUNGWANA NI VITENDO SIO MANENO
 
Hivi hamumjui?? yule alimselema ni mr misifaa tuu! polee ila ni lazimaa uendee kwa faidaa yako! Moyo shupavu n kupambanaa na kushindaa ukisusaa itakusaidia nn?? ndo utazidi kuwapa mafisiemu nafasii
 
Kama kweli ameongea hayo,basi hatuna RAIS bali tuna Mwenyekiti wa CCM.

Huna sababu ya kususa,ukishamuelewa mtu ni rahisi kuishi naye.KUna siku atajishtukia kwamba anayofanya yanaulakini.

Issue ya Mwenye nyumba ni lazima afanye maana HULKA yake ni visasi kwa kwenda mbele.Cha msingi tumieni vizuri pesa mnazopata kwenye halmashauri na kupeleka kule ambako RAIS amesema hatapeleka misaada.

Ni maisha tu yawezekana huko asikopeleka hakuna wanachama wa CCM
 
Nimejuta kwenda huko na sitakaa niende tena kwenye ziara zake kwani huko ni kufuata maudhi badala ya kufurahia maendeleo ambayo ndiyo lengo la UKAWA.

Ndugu, USIJUTE kwenda huko. Vinginevyo tungepata vipi ENGO hii ya STORI?
Mytake: Namshauri Raisi (kwa heshima/Taadhima) AWATUMIKIE Wananchi WOTE. Waliomchagua na wale ambao hawakumchagua. Aache kinyongo. Siku zote anawaomba WOTE WAMWOMBEE. Mbona huko HABAGUI kwa kusema: "Mlionichagua nimbeeni". Ningependa kuona Raisi wangu asiyefanya kazi KiCCM (yaani UBAGUZI). Itifaki izingatiwe!

ni kweli Mh. Rais anatakiwa kuwatumikia waTZ wote pasipo ubaguzi lkn kuna kipindi hata mzazi huchoka kwa matendo ya mtt wake. nashauri pia wapinzan wasilete upinzan sehem isiyotaka upinzani. mathalani kwann wanamwandama huyo prof. Muhongo?au Makonda? na wengine NA WAKATI NI WAZI HAWA JAMAA ni wachapakazi tena sana tu. kama serikali inafanya mazuri wanatakiwa watoe mchango wao na si kusubiri pale kunapoteteleka ndio watie maneno zaid kupata popularity. kama raisi anataka kuishi kwa ndoto zake ni lazima awafanyie kazi wapinzani wake akicheka nao yatamkuta makubwa. for which hakuna mtu anayetaka hayo. God forbid
 
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA ALIVYODHALILISHWA NA SERIKALI YA MAGUFULI

Makamanda pipozzzzz! Jana nilipokea mwaliko wa maneno kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kupitia kwa Mkurugenzi wangu Manispaa ya Ilala wakinitaka niungane nao leo (jana) kwenye ziara ya Raisi Kinýerezi kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo kipya cha kufua umeme wa gesi na mvuke 240 MW (Kinyerezi II), mradi unaotarajiwa kukamilika 2018.

Nilipofika nilipokelewa na kiongozi mmoja wa protocal ambaye ananifahamu kwa kuwa tulikuwa tunasali pamoja zamani akanikabidhi kwa public relation manager wa Tanesco ambaye pia ananifahamu tangu akiwa mwandishi wa habari na mimi nikiwa mwanaharakati wa kupinga wawekezaji wa TTCL.

Kama Meya nilipangiwa kukaa jukwaa kuu la Raisi kati ya matatu ambayo mengine yalikaliwa na waheshimiwa wabunge na wawekezaji, lingine likikaliwa na wakurugenzi na viongozi wengine.

Sasa kituko kikaanza, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco akaanza kutambulisha watu walio ktk jukwaa kuu akataja karibu wote pamoja na mbunge Bona aliyekaa pamoja na mimi kwa heshima ya mbunge mwenyeji akaniruka mimi japokuwa alikwishaambiwa uwepo wangu!

Baadae alimkaribisha Raisi aliyekuja na kituko cha mwaka. Aliendelea kutambulisha mabalozi na wawekezaji, mkewe, mbunge Zungu (Ilala), mbunge Kessy (Nkasi Kaskazini) akamruka Anatropia wa CDM, akamwita mbele mbunge Bona na kumsifia sana akisema kwamba wananchi wa Segerea walifanya vizuri kuchagua mbunge wa ccm kama na yeye alivyo wa ccm na kwamba kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwa sababu ati hawezi kumpa mtoto wa jirani chakula wakati wakwake yupo!

Kama hiyo haikutosha akampa nafasi ya kusalimia wananchi! Haikuishia hapo akasema amemchagua mkuu wa mkoa Makonda kwa vile ni mchapakazi na kwamba wengine walikuwa wakigombana naye na kujidai kukataa fedha za maendeleo sasa yeye kampa ukuu wa mkoa awe bosi wao sasa aone kitakachoendelea!

Kauli hii iliniacha hoi. Kama vile haitoshi akasema tena kwamba amemteua mchapakazi mwingine ambaye wasiopenda maendeleo wanampinga Mh. Muhongo. Ati naye atawakomesha wale waliokuwa wanapenda kukodishakodisha mitambo ya kufua umeme. Ati anampongeza kwa kuvunja bodi iliyokuwa inamshauri kukodishakodisha mitambo ya ajabuajabu.

Yote hiyo ni mipasho kwa wapinzani ambayo haikutakiwa kutoka kwenye kinywa cha Raisi. Ile ilikuwa ziara ya kiserikali siyo ya chama chake. Na madongo mengine mengi kawarushia wapinzani utafikiri akina mama wanaocharurana kwa mafumbo.

Nimejuta kwenda huko na sitakaa niende tena kwenye ziara zake kwani huko ni kufuata maudhi badala ya kufurahia maendeleo ambayo ndiyo lengo la UKAWA.
Hii habari imenisikitisha sana yani Rais anatamka maneno kama hayo ya kibaguzi . Nimeumia sana ila mungu yupo
 
Magu pamoja na PhD yake haijamsaidia kung'amua mambo upinzani sio uadui ndo mana kwenye teuzi anaogozwa na visasi. Hii ni aibu tupu hata haya aoni ila haishangazi ndo akili za ccm wao madaraka mbele na kubagua watu. Jk alikua mswahili ila hakufikia hyo level yake alijua kuongea na kila group kulingana na mazingira
 
Mh, kama ni kweli mh.raisi amefanya hivyo, it isn't this way.
BTW ndugu meya uache kulalamika na wewe, u need to be strong.
 
Magu pamoja na PhD yake haijamsaidia kung'amua mambo upinzani sio uadui ndo mana kwenye teuzi anaogozwa na visasi. Hii ni aibu tupu hata haya aoni ila haishangazi ndo akili za ccm wao madaraka mbele na kubagua watu. Jk alikua mswahili ila hakufikia hyo level yake alijua kuongea na kila group kulingana na mazingira
Ndio maana mlimuita DHAIFU. Sisi watu wa kanda ya Ziwa sio wanafiki. Tunanyoosha Kama ilivyo.
 
Kama kweli ameongea hayo,basi hatuna RAIS bali tuna Mwenyekiti wa CCM.

Huna sababu ya kususa,ukishamuelewa mtu ni rahisi kuishi naye.KUna siku atajishtukia kwamba anayofanya yanaulakini.

Issue ya Mwenye nyumba ni lazima afanye maana HULKA yake ni visasi kwa kwenda mbele.Cha msingi tumieni vizuri pesa mnazopata kwenye halmashauri na kupeleka kule ambako RAIS amesema hatapeleka misaada.

Ni maisha tu yawezekana huko asikopeleka hakuna wanachama wa CCM
Kwenye jimbo la professor j. Huko morogoro mbona wazir alionesha ushirikiano mzur tu .Hekima ni kitu kizur sana
 
Back
Top Bottom