Rais Magufuli akutana na Mabalozi wa Marekani na Italia

Nikikumbuka yale masusla ya "Tena Sukari yenyewe ni very inferior kutoka nje ukilinganisha na ya hapa kwetu" huwa napata hofu sana nikimuona amekaa na wazungu kama hivi
Kwa nini upate hofu kwa mtu ambaye hukumchagua kuwa Rais wa Tanzania kama siyo unachokifanya ni unafiki.

Badala upate hofu kuwa kwa sasa Lowassa na genge lake anaanza kutengeneza taasisi yake ndani ya taasisi ya CHADEMA.

Kwa akili yako unadhani wazungu wote wanatumia lugha ya kiingereza katika mawasiliano. Unachekesha kweli.
 
Wewe pacha wake Lowasa hakuna aliye wabembeleza na Rais husema wazi na aliwambia waige mfano wa China na sasa wameleta wenyewe!
Huyo kijana anashangaza sana.

Tatizo ni kuwa, watu wa aina ya huyu kijana walidhani nchi za Magharibi zitafanya kazi kwa faida ya fikra zao kwa manufaa yao.
 
On a serious note;Hivi si alikashifu misaada ya nje na kusema haiwezekani nchi tajiri kama hii itegemee misaada kutoka nje?

Hiyo kauli kuwa misaada ya Marekani ni muhimu ameitoaje tena?

Kumbe yale matusi yote dhidi ya MCC yalikuwa ni sizitaki mbichi hizi?

Kweli wazungu wanajua unafiki wa viongozi wetu na wanawapeleka hivyohivyo.Unafiki haujawahi kuleta afya.

I wanted to say the same

tena alikuwa mapumzikoni Geita
 
Magufuli afananisha misaada yenye masharti na mkate wa masimango Kuchapa


Rais Dk John Magufuli.

0 Comments

RAIS John Magufuli amefungua mdomo kuhusu misaada ya nchi wahisani inayoambatana na masharti, aliyoipa jina ‘mkate wa masimango’ na kusema kuliko kula mkate huo ni bora kushindia muhogo.

Alisema hivyo jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kwanza ya juu (Flyover), inayojengwa katika makutano ya Barabara za Mandela na Nyerere, kwenye eneo la Tazara. Barabara hizo zinajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuzungumzia misaada yenye masharti tangu Shirika la Changamoto ya Milenia (MCC) la Marekani, kusitisha msaada wa Dola za Marekani milioni 472.8 sawa na karibu Sh trilioni moja, zilizokuwa zitumike kuongeza kasi ya usambazaji umeme.

MCC ilisitisha msaada huo pamoja na uhusiano wake na Serikali ya Tanzania kwa madai kuwa Serikali haijachukua hatua za kuheshimu uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.

Bodi ya shirika hilo ilisema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar, ambao haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa Serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.

Akionesha kukerwa na misaada inayoambatana na masharti, Rais Magufuli aliisifu Japan kuwa ni rafiki wa kweli wa Tanzania, kwani imekuwa ikitoa misaada isiyo na masharti na kuongeza kuwa, nchi rafiki za aina hiyo ziko nyingi na zimejitokeza kutoa misaada isiyo na masharti.

Katika ujenzi wa barabara hizo, kwa mujibu wa Rais Magufuli, Japan imeshatoa fedha za walipakodi wake Sh bilioni 93.44 na Tanzania imeshatoa Sh bilioni 8.3 na kufanya mradi huo kugharimu zaidi ya Sh bilioni 100.

Rais Magufuli alisema, kwa kuwa fedha zipo na mkandarasi na mhandisi mshauri ni wazoefu wa ujenzi wa barabara za aina hiyo duniani, huenda zikakamilika kabla ya Oktoba 2018.

“Nawashukuru sana, (Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida), fikisha shukrani nyingi kwa Serikali ya Japan kwa jinsi wanavyotusaidia katika miradi mbalimbali kwani tunaposaidiwa na nchi tajiri, maana yake ni kuwa wamechukua fedha za walipakodi wao na kuamua kuleta Tanzania ambapo hatutaki kulipa kodi,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, kwa kuwa Japan imetumia fedha za walipa kodi wake kuisaidia Tanzania, Rais Magufuli alitoa mwito kwa Watanzania kuhamasishana kulipa kodi ili katika miradi mingi ya maendeleo, nchi ijihimili yenyewe. Alihakikishia nchi wahisani kwamba hakuna fedha ya misaada itakayopotea na kusisitiza kuwa Serikali yake imeamua kujisimamia yenyewe.
 
Kwanini siku hizi hawa mabalozi wa ulimwengu wa Kwanza wanapishana kila siku Ikulu??

Mara balozi wa China, mara wa Japan, mara wa Uingereza, mara wa Germany.

Kuna nini Mgogoni??

Siku hizi Ikulu wanagawa juice ya bure??

Au palipo na mzoga ndipo tai wengi hukusanyika.??
Kuna ulaji huko, maana wakichelea watakuta mChina amechukua kila kitu.
 
On a serious note;Hivi si alikashifu misaada ya nje na kusema haiwezekani nchi tajiri kama hii itegemee misaada kutoka nje?

Hiyo kauli kuwa misaada ya Marekani ni muhimu ameitoaje tena?

Kumbe yale matusi yote dhidi ya MCC yalikuwa ni sizitaki mbichi hizi?

Kweli wazungu wanajua unafiki wa viongozi wetu na wanawapeleka hivyohivyo.Unafiki haujawahi kuleta afya.

Mkuu Saanane hapo kwenye red ndio huwa siwaelewi wanachadema. Unafiki mkuu ni nyie kumpokea Lowassa na kubadili gia angani.
 
On a serious note;Hivi si alikashifu misaada ya nje na kusema haiwezekani nchi tajiri kama hii itegemee misaada kutoka nje?

Hiyo kauli kuwa misaada ya Marekani ni muhimu ameitoaje tena?

Kumbe yale matusi yote dhidi ya MCC yalikuwa ni sizitaki mbichi hizi?

Kweli wazungu wanajua unafiki wa viongozi wetu na wanawapeleka hivyohivyo.Unafiki haujawahi kuleta afya.
Hiyo ni zawadi kwa ufanyaji kazi wa kutukuka wa Mh Magufuli na serikali yake kwani kila mahali ulimwenguni sifa zake zinavuma.

Msihadaike kwa neno MSAADA kutumiwa na Mh Rais bali pateni maana inayotolewa na muktadha.

Huyu balozi yeye ndiye kaenda kuzawadia hiyo pesa na serikali kwa niaba ya wananchi wa Tanzania itaipangia matumizi.
 
Sijakuelewa mkuu apo.
JPM huwa hape
On a serious note;Hivi si alikashifu misaada ya nje na kusema haiwezekani nchi tajiri kama hii itegemee misaada kutoka nje?

Hiyo kauli kuwa misaada ya Marekani ni muhimu ameitoaje tena?

Kumbe yale matusi yote dhidi ya MCC yalikuwa ni sizitaki mbichi hizi?

Kweli wazungu wanajua unafiki wa viongozi wetu na wanawapeleka hivyohivyo.Unafiki haujawahi kuleta afya.
ndi misaada yenye masimango.

MCC walipocjomoa UK na China wao walijitoa kuokoa jahazi na sasa US karudi kivingine huoni kuwa ni namna ya US kujibua.

Kwa jinsi nimjuavyo JPM lazima itakuwa uyu balozi ndo kaomba appointment na raisi sio JPM kuomba appointment na uyu Balozi.JPM ni maskini jeuri.

Wazungu misaada mingi watupayo wao hufaidika zaidi kuliko wapokeaji wa misaada iyo kupitia masharti yao.

So withdrwawal ya MCC fundi to some extent inakula kwa US pia ndp maana wameamua kurudi kivingine maana ata Symbioni kule vs Muhongo nako kimenuka.
 
wewe ulitaka aongee kingereza cha wapi wakati yeye ni msukuma?lugha sio issue sana kikubwa ni point unayozungumza kwa nini mzungu akishindwa kuongea kiswahili vizuri huwa hachekwi au kuonekana hajui??
 
mbona taa zinawaka walienda saa ngapi? naona walipewa na dinner kabisa, hongera jpm waje kukusalimia baada ya masaa ya kazi.
 
Mimi huwa siwaamini hawa watawala wa nchi za Magharibi.

Kwa sasa wamegundua kama Rais Magufuli haingiliki kwa njia waliyokuwa wamezoea na wananchokifanya kwa sasa ni kutumia njia nyingine katika kutimiza malengo yao.

We must take anything they say with a grain of salt!
Hapa siwaelewi Watanzania

Miezi michache baada ya US kuzuia pesa za MCC, viongozi walisema 'vimisaada' vinadhalilisha,hatuhitaji tutafanya wenyewe

'Wasomi'wakaandika magazetini kuhusu utegemezi,ni wakati wa kusimama wenyewe.

Wana mitandao na Msemajiukweli wakitetea hatua za kukataa misaada ya MCC.

Wengine tulisimama na kusema misaada si msingi wa maendeleo.

Lazima tukubali tunahitaji na kwamba MCC kuzuia msaada wake kwasababu ya fyongo zetu si sababu ya sisi kuanza kusema hovyo.

Kama tumekataa misaada iwe kwa , si suala la staki mbichi hizi kwa staili ya Sungura.

Nashangaa kiongozi wetu anasema 'msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo''

Kama ilikuwa ni hivyo kwanini tulisema MCC si muhimu na kwanini tukaachia pesa hizo?

Kwanini tulikubali kulinda watu wachache znz kwa gharama ya mamilioni ya Watanzania?

Tunawauliza walitetea 'Hatutaki vimisaada' imekuwaje 'mwenzenu' amewaruka kimanga ?

Tunawauliza akina Humphrey Polepole mtaandika nini magazetini kutetea huku ''kugeuka nyuma na kuwa jiwe''

Tunawauliza wasomi, mlitumia vipi bongo zenu na elimu zenu kutuambia misaada haina maana ikiwa kiongozi wetu anasema ni muhimu sana?

Mliotubeza, mtuombe radhi kwa ukurusa wa mbele wa ndimi zenu.

Ukweli ni kitu kizuri sana, kinamweka mja huru wakati wote.

Tulisema ukweli leo tupo huru, mliokwepa ukweli hamjui sura zenu mziweke wapi

Mag3 Nyani Ngabu The Boss Mzee Mwanakijiji Mchambuzi JokaKuu
Lizaboni
 
Tanzania haijaomba chochote isipokuwa USA wao wanasema wanataka kuleta hiyo US 800 ml. Hata Kiswahili kinakuwa kigumu kukielewa?
Kuna baadhi wanashindwa hata kutumia komoni sensi katika kuelewa alichokisema Rais Magufuli na kinachofanyika kwa sasa.
 
Back
Top Bottom