Ngoja sasa,uone vita kati ya JF Diaspora,na JF home,Tanzania.....
Some popcorn,lol,
Kaka
Wahamiaji hua hawatafuti kazi serikalini, fanya research yako kote duniani. Hua wanatafuta private na ku create zao.
Hapo ndo wana make differences, wahamiaji.
Mfano, tuna ziwa victoria, nyasa, tanganyika, eyasi. Mto rufiji, kagera, malagalasi nk mbunga na mashamba yako wazi. Na bado tunalilia serikali ijiandae na njaa kuhudumia na ikishindwa itakiona cha mtema kuni, sababu mvua hakuna.
Wahamiaji would have closed this gap, amini nakwambia.
Wapi niliposema wageni wanatafuta kazi serikalini? Ukweli ni kiwa Tanzania hakuna kazi, na kazi zilizopo zimawatosha Watanzania
Wahamiaji wana create more jobs. Maana watasafiri watakula, watalipa kodi za nyumba na creativity nyingine ambayo mzawa anaishi kado kado za ziwa victoria anasema hakuna mvua.
Kupinga dual citizenship ni ulofa na ubinafsi tu.
Dakika chache nimetoka kuongea na ndugu yangu yupo Odense DK sasa mwaka wa 10. Japo anapata haki kama raia wengine wa Denmark lakini anashindwa kuji-commit kwenye mambo mengi kwasababu bado tu anajua yeye si raia. Sasa hapa nashangaa kwanini dual citizenship isiruhusiwe tu? Inamaana akitaka kuwa raia wa DK basi anapoteza uraia wa Tz. Na hapa nyumbani ameacha ndugu. Serikali iache ubinafsi.......kukataa dual citizenship ni ulofa tu.
Waamiaji hawawezi kucreat kazi, kazi zinaletwa na investors,
Kwani ninaposema wahamiaji unaelewa nini, kaka?
Mimi sina maana ya wakimbizi. Wahamiaji wa kiuchumi wanaotafuta "green pasture"
Kaka unajichanganya na maelezo yako, kwenye hoja yako ya kwanza unazungumzia ruhusa kwa Immigrants waingie na wafanye kazi bila vibali, hao ni tofauti na investors ambao wanakuja na capitals kuwekeza kwa ajili ya kupata faida,
Hao investors hakuna mtu anayewanyima Permit wala usumbufu Dangote, BP, Backlays, Barrick, FNB, nk wewe unazungumzia wafanyakazi watoke kwao waje kugombea kazi na wazawa, watu wasio na capital zozote zaidi ya vyeti vya shule tu labda na experience
Impact of Immigration on UK Economy
Tejvan Pettinger July 19, 2016 economics
In the past two decades, the UK has experienced a steady flow of net migrants into the economy. Net migration is a significant factor in the growth of the UK population. But, does this net migration help or hinder the UK economy?
Impact of Immigration on UK Economy | Economics Help
Mkuu creativity inatokana na kujiamini (High self esteem).Ni kweli kwa muda mrefu sisi watanzania tulikuwa na LOW self esteem. Kila kitu KIZURI tunajifananisha na nchi JIRANI.Hata kwetu sasa kuna Creativity/Ubunifu!Regulated process ipi? wewe ukiwa na kampuni unaitisha interview anayeweza ndo unamchukua.
Wahamiaji ni creative kutokana na ukweli kuwa anakuwa hayupo nyumbani na anatumia uwezo wa ziada ili ku survive, hapo ndo creativity inapokuja.
Nilishakwambia usilinganishe hayo mambo ya ulaya na Tanzania, huwezi kupata uhalisia hata kidogo, ulaya kazi ya Bar au Hotel ni kazi ya Heshima sana na ina mifumo yake, Tanzania hizo ni kazi za kishenzi/kihuni, yaani unakuta mtu ana Bar na wafanyakazi zaidi ya kumi anawalaza geto,
kaka elewa kuwa Tanzania hakuna kazi, watanzania wenyewe wenye level mbalimbali za elimu na uzoefu wanaangaika kutafuta kazi sembuse Wageni?
Hatujafikia hiyo stage ya kuwaleta wageni kuja kufanya kazi bila vibali, Dangote kaleta gari 600 kulikuwa na Madereva zaidi ya 4000 walienda kusololea kazi,
Mkuu creativity inatokana na kujiamini (High self esteem).Ni kweli kwa muda mrefu sisi watanzania tulikuwa na LOW self esteem. Kila kitu KIZURI tunajifananisha na nchi JIRANI.Hata kwetu sasa kuna Creativity/Ubunifu!
Rais magufuli akitaka kufanikiwa awamu hii fanya hivi
Ruhusu immigrants waje wafanye kazi Tanzania bila working permit, kwa sababu.Wahamiaji huwa ni creative
Tanzania hakuna kazi sababu yakuweka ngome, wote wanabaki na mawazo ya aina moja yasiyokuwa creative na mwisho wake wote wanataka kazi kutoka serikalini kwa sababu hawawezi ku create kazi wamejifunga kwenye box la uzawa.
Serikali ikitaka kutoka humo na iachane na pressure kutoka kwa wananchi kwamba imezuia ajira nk, yapaswa kuruhusu immigrants waje wawafundishe wazawa namna yakutengeneza kazi. Itakuwa kama ulaya hivyo hivyo, ndugu yangu.
Tatizo la ajira Tanzania ni mindset iliyojikita ktk uzawa na kuzuia immigrants. Uchumi una dictate ku create demands, the moment utakapokuwa na immigrants opportunities zinaji open zenyewe.
Hizi sera za nchi yetu kujifungia zitatucheleweshea maendeleo tu. Wanzetu wanatafuta namna yakujichanganya zaidi na dunia sisi tunaangalia namna tutakavyojifungia ndani tusionekane wala kuzoeleka. Nashangaa tunachoofohia ni nini?Kukataa Dual citizenship. Nikithibitisho kingine hatuna wataalamu.
Dual citizenship ni by design lazima ilihusiwe. Na Elimu tuliyo nayo kwa kujifungia sababu hatutaki dual citizenship hatutatoka hapo tulipo hata ashuke nani.
Ok, topic nzuri. Ila wahamiaji wachukuliwe wenye skills. UK inachukua kutoka India wale trading brokers, Drs, na Software engineer. Tanzania haihataji wsukuma mikokoteni, inahitaji creative skills people.
DUAL citizenship THUMBS UP. Mimi mmoja wapo tunaopata tabu kuja nyumbani. Unataka kufanya miradi 100 lakini huna njia because I feel I am outsider now. Miradi ndio maendeleo ya nchi, miradi inaleta ajira za wananchi. Ikiwa serekali itaendelea na single citizenship, ni upumbavu. Hakuna sababu yoyote wa Tanzania waliokua nje wasipewe Passport.