Baada ya pita pita huku na kule nimepata habari hii ya rais kuwazawadia wasindikizaji wa waziri mkuu wa ethiopia kwa kupewa sh million 20. je pesa hii ni hongo au ni ujira kwa wasindikizaji?? Kama ni ujira ina maana siku zote wasindikizaji hupewa pesa pesa na mimi kesho nikapange foleni niache kaz zangu. Kama sio ujira ni hongo ili na kesho waje wengi rais anatufundisha nini wananchi wake?? Je kila macho na masikio tuwe tunaulizia ratiba za wageni ili tukajipatie ujira?? Na kama siku hiyo ijayo hatawalipa wahudhuliaji wakidai pesa itakua kosa??
Pia kitendo cha kumpa mkuu wa mkoa ina maana wageni sahiz wanapitia kwa mkuu wa mkoa?? Je waziri wa mambo ya ndani ana nafasi gani hapo?? Au ndio kumpa kiki bashite aonekane anakubalika kwa kugawa pesa zilizo toka kwa rais?? Kwa sasa mkuu wa mkoa ndio mkono wa kuume wa rais wetu??
Watanzania wenzangu kwa sasa ni mwendo wa kuvizia wageni tukagawane hela za taifa kama njugu!!