Rais Kikwete atimiza ahadi yake ya kununua kivuko mto malagalasi- Kigoma

Kama mpaka muda huu hujagundua kosa lako basi kweli mimi nimerogwa halafu wewe ndo ukadata. Angalia haraka zako, eti unaogea, sema unaongea.

hata ufanyeje fimbo unazo umeoga bila sabuni eeeeeee,nyota ya jk hata msipowasha yenyewe inawaka mtazidi kununa hamtapata mnalotaka.
 
Safi sana mkuu, hao wanaokatalia hongera tulishawazoea, wanaona kama hatma yao kwenye majukwaa ya siasa inafikia kikomo, hawatakuwa na cha kuwadanganya watanzania.

mkuu hawa watu hata kama ukiwanunulia gauni na vilembe bado hawatakupa ahsante wala hongera.
 
Tuambieni ametimiza zipi na zipi bado kati ya zile zote alizoahidi mwaka 2010.
[h=2]Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015[/h]
AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Hii ahadi iliyotekelezwa nafikiri ni ya wakati wa kampeni za 2005 kwani kwa hizi za 2010 hii haipo
 
jk ni mzalendo ,mwana maendeleo na mwana demokrasia aliyebobea,amesimamia na kuitekeleza iani ya CCM iliyomuweka madarakani,amemaliza kazi,naam akitoka madarakani tutamkumbuka kama mwanamaendeleo ni si kingine
 
Ametekeleza ahadi ya kivuko huko kigoma, akaweka lami barabara kadhaa za kuunganisha mkoa wa kigoma na mikoa mingine, daraja la kigamboni linaendelea kujengwa, barabara za jiji la dsm zinapanualiwa na kuboreshwa, ikiwa ni pamoja na bus ziendazo kasi, yamejengwa madaraja makubwa sana hapa nchini, vyuo vikuu kibao kila kona, hospitali za mikoa zimepandishwa hadhi na kuwa za rufaa,nk nk nk

2010 aliahidi zaidi ya 100 (zimo humu JF), zipitie tena na utuambie amefikia % ngapi
 
jk ni mzalendo ,mwana maendeleo na mwana demokrasia aliyebobea,amesimamia na kuitekeleza iani ya CCM iliyomuweka madarakani,amemaliza kazi,naam akitoka madarakani tutamkumbuka kama mwanamaendeleo ni si kingine

Wenzako wana CCM wa ukweli wanadai kuwa JK anatekeleza Ilani ya CDM, kama vile kujenga Chuo Kikuu Dom na Katiba mpya. Unasemaje hapo?
 
JK amejitahidi sana japo si rais kutimiza yote ila nia anayo ya kutimiza yote mungu anamlipa kwa kujali watu wake. CDM waliahidi elimu bure wananchi wakawapa baadhi ya halmashauri lakini mpaka leo hakuna hata halmashauri moja iliyo chini ya CDM inatoa elimu bure. Jamani hakuna hata tawi moja la CDM inapata fungu la ruzuku kutoka makao makuu hivi tukiwapa nchi hawa si tutakufa sie
 
Wajibu wa Serikali ni kuwatumikia wananchi kwavile imechaguliwa kwa kura zao(imepewa ajira).Baada ya kupewa ajira wananchi wanalipa kodi ili serikali ifanye kile wanacho kihitaji. Kwahiyo serikali haifanyi FADHILA KWA WANANCHI BALI NI JUKUMU NA WAJIBU WAKE! Hamna haja ya kumsifia mtu wakati aliomba kuajiriwa na kupewa nyenzo za utendaji!
 
umeongea vyema ila natofautiana na wewe kidogo pale uliposema wanaomchukia JK wanamlaza macho kufikiria jinsi ya kutimiza wajibu kwake kwa vile wanaumia sana kuona ahadi zikitekelezwa jambo ambalo linahatarisha kula yao 2015 kwa vile hawatakuwa na jipya la kuwaeleza wananchi tena. JK atakuwa amemaliza kazi.
Narudia tena 'hiyo ni dhana yako'. Watu wanapiga kelele sio kutafuta madaraka tu ila wanataka utawala bora. Demokrasia ikiwa barabara inatoa fulsa kwa wananchi kubadili uongozi wakipenda, na ni jambo jema kuhakikisha utawala bora.
 
Huwa sipendi kuwekewa maneno. Wapi nimemshukuru JK? Mtoa mada vizuri uweke rejea. Wapi JK aliahidi kwenye kampeni kwamba ataleta kivuko?

CCM mnaweweseka sana na Kigoma kusini. Ni wajibu wa serikali kuleta maendeleo na sio hisani; na huo ndio msimamo wangu siku zote.

JK hajawahi kuahidi kivuko wala hakufika kata ya ilagala kwenye tatizo husika.
 
Nimekua nikisisitiza kuwa ni wajibu wa serikali kuleta maendeleo kwa wananchi kwakua inatoza kodi wananchi na utajiri wa nchi yao. Na ni kwa msingi huo inapotekeleza mradi wowote haipaswi kujiona inafanya muujiza au hisani.

Mtoa mada mmoja kwa jina la kalamu kaandika upotoshaji wake kwa maslahi anauoyajua yeye kwamba mimi nimemshukuru kikwete kwa kuleta kivuko alichoahidi wakati wa kampeni 2010. Ukweli JK hakuwahi kuahidi kivuko popote katika kampeni ndani ya mkoa wa Kigoma. Hata kata husika ya kivuko Ilagala hakufika.

CCM acheni kuweweseka na jimbo la Kigoma Kusini. Wananchi wanajua mabadiliko makubwa waliyoyapata baada ya mimi kuingia bungeni. JK alikuwepo hata kabla ya Kafulila kuwa mbunge na hakuna kilichofanyika chochote Kigoma Kusini. Kigoma inawaelewa na Tanzania inawaelewa. Wanatambua kiasi cha maendeleo kilichopo hakiakisi utajiri wa taifa lao. Tumecheleweshwa sana.

Nashauri mtu akiweka mada ya kiongozi fulani kusema anukuu au kuweka source badala ya kujiandikia tu hata kupotosha..
 
Ni kweli mkuu Magamba wanapenda kutuona sote hamnazo.
Watieni adabu nje na ndani ya bunge.
 
Back
Top Bottom