Rais hasemwi bungeni,ila kwa kumpongeza

Na hapo hakuna cha mno kilichofanyika kwa karibu miaka 55, yan kama tunafanya analysis ya mafanikio gan yenye tija tumepata tangu wakoloni waondoke ni hasara tupu kwa viongozi wote wanne waliopita. Je ingekuwa Tanzania ni kama Botswana, Namibia, South A au hata Ethiopia tungewaiteje viongoz wetu, si Miungu kabisa.
Sisemi kwamba swala la utii kwa viongozi sio muhimu, ila la kulazimisha, let the nature find its own path, yan kama unawafundisha watoto wako vizuri bila hila, wakikua wanasoma historia ya miaka iliyopita kwa nchi zote, wanaangalia maisha yao kwa wakati huo walipo wanalinganisha na maisha ya wananchi ktka nchi nyingine. Amini nakwambia watakwenda kulia kwenye Makaburi ya mababu zao wenyewe bila hata kushawishiwa na mtu tena kwa uchungu mkubwa. Sababu wanajua kumbe hapa tulipo kuna watu walisuffer kutufikisha hapa. Sasa hapa kwetu watu wanataka wasujudiwe wakati wameuza kila kitu vijana wamegeuka wauza machinga tu, hiz akili matope.
 
Msigwa na lema kwa kula matapishi yao, wanamtetea nani bungeni??
Mipango mizuri ni ile inayokuwezesha kubadili mipango ya awali, kwa maana mipango sio kitabu Kitakatifu kisichobadilika.
Awamu ya nne Msigwa na Lema walikuwa wanawapigania Watz kupata japo milo miwili wakati ule wakipata mlo mmoja kwa siku lakini sasa inaonekana wanaelekea kwenye kupata nusu mlo (refer sukari) hivyo kumuona huyo aliyekuwa analeta walau mlo mmoja kuwa bora.
 
Ni katika kukumbushana tu
Mwenye sera na mamlaka ya kuuza/aliyeuza nyumba za serikali kwa sasa mko naye KAMATI KUU YENU CHADOMO...ni muda muafaka kumuuliza alifanyaje kupitisha hiyo sera....mumuvue nguo hukohuko sisi hatuna shida naye kwa sasa
tutaelewana tu taraatiibuu.
Mbona akina Nape hawalipigii kelele kama walivyomsukumia zigo lowasa.
 
Ubaya wa Nyumbu wanahubiri Magufuli afuate kanuni na taratibu za nchi lakini wao chadema hawafuati kanuni wala utaratibu wowote wa bunge..

Ni kuzomea mwanzo mwisho.

Jaribuni kuwa watu wazima basi

Wewe Mwasita wewe, amka bhana unaongea nini bhana, aaaah you are making me down!!
 
Hapa ndipo tunapo kosea kumfanya raisi ni mtakatifu kuliko malaika angali yeye ni binadamu kuna sehemu anafanya vizuri na kunasehemu anateleza kumwambia ukweli ili ajirekebishe ni jambo la msingi kwani kufanikiwa kwake ni kufanikiwa kwetu sote.

Ndipo Lema na Msigwa wanaposema kwa namna moja au nyingine wanammiss Kikwete.Ni kwamba hawakufafanua tu wanamkumbuka kwa yapi ila wote tunaelewa wanamkumbuka kwa kuruhusu uhuru wa habari na kutoa maoni.Ni kweli hayupo hadi sasa raisi aliesemwa kwa mazuri na mabaya kama raisi Kikwete na sio kwamba hakuyasikia ila aliheshimu sana uhuru wa habari ikiwa ni pamoja na kutoingilia mamlaka ya bunge.Sasa shangaa kiongozi yule yule Zungu aliewahi kuwa m/kiti wa bunge lililopita chini ya spika Makinda ndiye huyu huyu anaedai kutoruhusiwa raisi kusemwa bungeni labda kama ni kumsifia tu.Hivi kuna kanuni yoyote ya bunge iliyorekebishwa na upinzani usiyajue marekebisho hayo?Sasa leo inakuwaje kiongozi aliekuwepo juzi na leo kuendesha bunge lile lile kwa double standards?Hivi ni kweli spika wetu mama Makinda na naibu wake na sasa ndiye spika wetu Ndugai hawakuielewa hiyo kanuni au walikuwa wanawapendelea wapinzani?Mbona mzee Zungu ni msomi mzuri tu tena wa elimu bora ya miaka hiyo kuna maagizo kapewa na chama chake kuhusu michango ya upinzani bungeni au ana hofu na ukali wa raisi wetu?Ameshasahau kura zilizomshindisha mh.Zungu sio za wana ccm tu zipo na za wapinzani ambao nao wanatakiwa kutendewa haki?Kwa kuwa nao wapo wengi humu wanipe hiyo sheria/kanuni mpya kwa bunge hili.
 
Hizi ni mbinu za chama tawala kutaka kuua nguvu ya upinzani maana wameona vyama vya upinzani vinashamiri sana na kutishia uhai wa chama tawala.
Lakini mbinu wanazotumia sio sahihi kwasababu katiba inaipanguvu chama tawala kuwa raisi hatikiwi kuguswa hata kama ameharibu sasa hizi kasoro za kikatiba ni hatari kwa uhai wa demikrasia.
 
Jibu hoja au kama unatetea jenga hoja sio unaleta msutano hapa,kwani hao Chadema wapi wamekataa kuongelewa mabaya yao ............... tunambiwa bungeni si mahali pa kumuongelea vibaya rais ila kama unamtaja kwa mazuri ni ruksa je wewe unaonaje ............ toa maoni yako hutaki pita kimya.
Kuna watu wana shida sana duniani
 
Rasimu ya Mzee warioba ilikuwa poa sana, lkn wengi walishinda wachache wasepa, tutafka IPO cku
 
Ama kweli bunge limevamiwa awamu hii, kuna jitihada la kuligeuza kuwa baraza la mawaziri badala ja chombo cha kusimamia na kuisema serikali. Unaambiwa kanuni haziruhusu kumsema Rais pale bungeni, labda kama unataka kumpongeza ''Rais mwema''.

Kule Brazil na hata ndugu zetu wa South Africa wabunge wao walifikia hatua ya kumwajibisha rais kwa makosa ya kutumia madaraka vibaya.

Sasa hapa Bongo ''Tanzania ya Magufuli'' tunawezaje kumdhibiti rais asitumie madaraka vibaya kama wawakilishi wetu kina G.Lema wanakatazwa rais asisemwe vibaya?

Mwenye picha ya Lugumi atuwekee, wengine hatumfahamu!!!!!!!!
Picha gani tena ? Lugumi siyo mtu mjomba , Lugumi ni TAASISI KUBWA SANA , kwa mfano unawezaje kuniwekea picha ya TRA hapa ?
 
Ubaya wa Nyumbu wanahubiri Magufuli afuate kanuni na taratibu za nchi lakini wao chadema hawafuati kanuni wala utaratibu wowote wa bunge..

Ni kuzomea mwanzo mwisho.

Jaribuni kuwa watu wazima basi
Nilivyoona tu jina lako sikushtuka
 
Rais anataka kujenga " himaya " yake .na wabunge wameshindwa kuelewa majukumu yao.
 
Ni katika kukumbushana tu
Mwenye sera na mamlaka ya kuuza/aliyeuza nyumba za serikali kwa sasa mko naye KAMATI KUU YENU CHADOMO...ni muda muafaka kumuuliza alifanyaje kupitisha hiyo sera....mumuvue nguo hukohuko sisi hatuna shida naye kwa sasa

naona mnatafuta pakutokea, arudishe nyumba walimu wanateseka mno
 
pamoja na mabaya yake lakini RAISI HUYU MWEMA kisha unendelea kukosoa kwa kuzunguka zunguka huo ndo utawala wa afrika viongoz wa na watumish wa umma ni malaika mobos wao ( raia) waliofanikisha mpango wa wao kuwa pale ni takataka.
 
Back
Top Bottom