fugees
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 2,868
- 883
Hata hoksa rusa kumvilia
Wandugu, rais Magufuli nimevulia kofia!, kumbe ni kweli amechinja mishahara hadi mshahara wa Gavana amefyeka!. Siku aliposema atapunguza mishahara isizidi TZS milioni 15, mimi ni miongoni mwa ma Tomaso wa humu, tulibisha na kubeza kuwa rais hawezi kupunguza mshahara wa mtu, kwa sababu hana mamlaka hayo.
Leo akihutubia jumuiya ya Chuo Kikuu, amethibitisha amefyeka mishahara ya peponi, na hakuna aliyeacha kazi kwa kupinga mishahara mipya ukiwemo mshahara wa Gavana ambao nao ameupiga panga, tena almanusura angeutaja, wastaarabu wakampooza kuwa ni kumdhalilisha gavana kusema anavuta ngapi, ila mshahara wake ameendelea kuutaja kuwa kuwa anavuta just TZS 9,000,000!.
Kuanzia sasa, namuaminia rais Magufuli, chochote atakachosema atafanya, kiukweli atafanya regardless katiba, sheria, taratibu na kanuni zinasemaje, the end justify the means, amesema, ametenda na ameweza.
Hongera rais Magufuli.
Paskali