Rais amekosea kumteua Amon Mpanju. Angeteua mlemavu ambaye ni neutral

Anaunda serikali kwa ajili ya wanaccm au wananchi wote?
Kwani wanaCCM sio wananchi? Rais anaunda serikali na watu ambao anawaamini na anaweza kufanya nao kazi. Haya maneno yenu ni kujipotezea muda tu...bora mngeenda kumsaidia mzee wa machooni (Lowassa Kujinyea) kuchunga Ng'ombe kule Monduli.
 
Mijitu mingine inapenda kulazimisha mambo.kama una chuki binafsi na mpanju sawa.unataka kujifanya unajua kuliko rais? Mpanju amekula kiapo cha uaminifu kwa jamhuri,pia ameapa kufuata maadili,acha ahukumiwe kwa kazi yake badala ya kuchafuana humu
 
..ktk post yangu ya kwanza nimejieleza kwa kirefu.

..huyu bwana angeteuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri nisingekuwa na tatizo.

..tatizo langu ni kuingizwa ktk CIVIL SERVICE. hapo ndiyo naona pana makosa.
Acha upimbi wewe...ni nani unaemjua wewe (mtu mzito) kwenye civil service ambae sio mwana CCM...Mtaje hapa.

Wakurugenzi wa halmashauri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa mashirika ya umma na taasisi za serikali...makamishna...wote hawa ni wana CCM.

Waraka wa utumishi wa umma haukatazi hizo nafasi kushikiliwa na wanachama wa chama cha siasa....na ndio maana ya ukisikia serikali ya CCM...usifikiri ni rais na mawaziri tu...ujue ni serikali kwa ujumla wake.
 
..nijatihidi kuwa-ignore.

..Raisi amekosea kumteua mlemavu mkereketwa wa ccm kama Mpanju.

..nina hakika wako walemavu wengi tu ambao wangeweza kuteuliwa ktk nafasi hiyo.

..Mpanju anafaa zaidi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM, kwenye utumishi wa umma hafai.
Umekomaa na Mpanju balaa lakin kumbuka kila zimwi na mbuyu wake Rais n binadamu kama wewe so hawez kutenda akamridhisha kila mtu. So upendeleo kwa mwanadamu n kawaida sana mkuu usihof kuhusu hilo na nna kusihi acha kulalamika sana malalamiko hayaleti maendeleo kilichobaki n kumuombea afanye kaz kwa weled
 
rais anamteua mtu kwa kuangalia ulemavu wake badala ya utashi wake na akili yake? hili siliungi mkono
 
..nilitaka ateue mlemavu ambaye ni NEUTRAL.

..Mpanju ni mkereketwa na mpiga debe wa CCM.

..ushahidi upo kwa mwenendo wake wakati wa bunge la katiba.

..zaidi ushiriki wake ktk kampeni za CCM.

..Nina wasiwasi kama Mpanju ataweka mbele maslahi ya taifa, au maslahi ya ccm.
Unachoongea ni kweli tupu ba ni kitu sahihi kabisa bahati mbaya watajaribu kujifanya hawakuelewi! Ndio Tanzania inavyoteketea hivyo
 
Mtoa mada umeteleza kidogo. Rais hakuteua wajumbe wa NGO, ameteua makatibu wakuu ambao ni sehemu ya chama kwa maslahi ya serikali yake. Tuwe makini katika kuanzisha uzi na ujenzi wa hoja.
 
Amemteua ili sheria ivunjwe kwa haki.Nadhani kuna wengine Mungu huwapa mapigo ya ulemavi ili kuepusha usumbufu kwa jamii baadaeA.mpanju angekuwa na macho sighted!! Mmmhhhh
 
Kama Mpanju kala shavu,Diallo,Polepole na Bulembo wakae mkao wa kula maana walikipigania sana chama.
 
Umeusoma waraka wa watumishi wa umma au ulimsikiliza Mbowe AKA Kengeza akisema kuwa watumishi wa umma hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama cha siasa?

Unyumbu ni kitu kibaya sana...ingia google na upakue waraka wa utumishi wa umma na usome..ndio njia pekee ya kujua ukweli wa mambo.

Kwa kukusaidia...watumishi wote wa umma wanaruhusiwa kushiriki siasa ikiwemo kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa...isipokuwa wanajeshi, jeshi la polisi, majaji na mawakili wa serikali.
Nakushukuru kwa kunipa mwangaza japo umeingiza na utu wako, nakusamehe bure.

Kwamba sasa kanuni zinaruhusu au la, ndio lilikuwa swali langu, na hivi karibuni Dk. Tulia alipogombea u Spika wa Bunge, swali kuwa ilikuwaje wakati akiwa Deputy AG awe na kadi ya uanachama wa CCM liliibuka kwa kuwa awali sheria na kanuni ya utumishi wa umma ilikuwa haimruhusu. Kwa hiyo kuuliza si ajabu, ni suala la updates badala ya ushabiki wa kijinga.

Vv
 
Mimi sijui kwa nini marais wa tanzania wanakuwaga viziwi yamemwa sana alipoteua baraza nikajua atajitekebisha sijui kalitoa wapi tena hilo jitu mnanalolijadili
 
Magufuli mwenyewe alikuwa kundi moja na mpanju wakati wa bunge LA katiba. Mi sioni shida kabisa huo ni mtazamo wako
 
Mimi sijui kwa nini marais wa tanzania wanakuwaga viziwi yamemwa sana alipoteua baraza nikajua atajitekebisha sijui kalitoa wapi tena hilo jitu mnanalolijadili
J JPM HANA HAJA YA KUPATA USHAURI TOKA BAVICHA
 
Back
Top Bottom