Radio Times FM yatanguliza mbele maslahi ya Taifa, yawakaribisha manguli kusaidia Taifa

"Ukitokea upande mmoja unaiba na kufanya udanganyifu hii ni cheating ... sakata la mchanga wa dhahabu ni Uzalendo wa hali ya juu na anapaswa kuungwa mkono".

Kwa kauli hii mkuu Mayalla you are being intellectually dishonest. ACACIA wamefanya cheating kwa ushahidi upi? Kwa ushahidi wa report ya tume ya Mruma? Unafahamu kwamba ile tume haikuwa tume huru. Pia unajua kwamba suala la mkataba ni suala la kisheria; ni mahakama ndo inapaswa kusema kama ACACIA wamedanganya ktk makubaliano yao ya kimkataba na serikali, siyo Mruma wala Magufuli.
Mkuu Ycam, somo nililofundisha ni UZALENDO. Uzalendo unaanzia kwenye utii. Kama rais wako ameunda tume ya wataalamu akakuambia tunaibiwa, then ni tunaibiwa!.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa ni uchunguzi wa kitaalamu tuu, baada ya kamati ya pili ikithibitisha tunaanza uchunguzi wa kijinai.

Hawa jamaa ni majizi!.

Paskali
 
Kwani hadidu rejea za kamati ya pili ni zipi kama ripoti yake ndio inasubiriwa ili kuanzisha uchunguzi wa kijinai? Na kama hawa "jamaa ni majizi" kuna haja gani ya kusubiri kamati tena wakati tayari uchunguzi umethibitisha kuwa ni majizi hawa jamaa? kichwa kinauma!
 
ycam:
Inashangaza kuona kuwa Brad Gordon CEO wa Acacia leo ameongea kwa adabu tofauti na tone yako. Umenikumbusha 'msomi' mmoja huko miaka ya nyuma, aliyemwajiri jirani na primary school mate wake kuangua kilio kwenye msiba wa mamake msomi. Huyo surrogate derivative alilia kweli kweli, 'mama yangu wee, mama yangu umeniacha, nani?....kwi kwi kwi,' ungedhani mama yake, ambaye wakati huo alikuwa bado hai, ndie likuwa amefariki. Kumbe wapi bwana, jamaa yuko kibaruani akimlilia mamake Dk professa tutor! Ninakwambia, kwa walioshuhudia tukio hilo na bado wako hai hawatakuja kusahau kituko hicho kilichotokea miaka 40 iliyopita, mara baada ya kifo na wakati wa matanga ya mamake msomi, Dk. professa tutor. ycam umeonesha kituko cha aina hiyo kwa Brad Gordon wa Acacia.
 
Mkuu Ycam, somo nililofundisha ni UZALENDO. Uzalendo unaanzia kwenye utii. Kama rais wako ameunda tume ya wataalamu akakuambia tunaibiwa, then ni tunaibiwa!.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa ni uchunguzi wa kitaalamu tuu, baada ya kamati ya pili ikithibitisha tunaanza uchunguzi wa kijinai.

Hawa jamaa ni majizi!.

Paskali
Mkuu kwenye marketing uko vizuri sana.
 
Kwani hadidu rejea za kamati ya pili ni zipi kama ripoti yake ndio inasubiriwa ili kuanzisha uchunguzi wa kijinai? Na kama hawa "jamaa ni majizi" kuna haja gani ya kusubiri kamati tena wakati tayari uchunguzi umethibitisha kuwa ni majizi hawa jamaa? kichwa kinauma!
kamati ya kwanza ni uchunguzi wa kitaalamu tuu. Kamati ya pili uchunguzi wa kiuchumi na kisheria.

Mtaalamu geologist anaweza kuona dhahabu ni nyingi kumbe kiuchumi sio economic viable kuuchenjua na kinachopatikana sio kingi kivile kama wataalamu walivyoeleza.

When we are well informed kuhusu kila kitu, tutakuwa kwenye a good position to decide na sio hizo peace meals.

Paskali
 
Mmmh kumbe kuwaalika watangazaji,ma dj na wasanii wa zamani kwenda Times fm kutoa uzoefu wa enzi zao ina maslahi kwa taifa?. Nilikuwa sijui mkuu asante kwa kunijuza,hongera ziende kwa times fm.
 
Wanabodi

Tanzania tuna vituo vingi vya redio, kila kituo kina mambo yake na mchango wake kwa Taifa.

Miongoni mwa vituo hivyo ni kituo cha Radio Times FM inayopatikana 100.5 ambacho pamoja na mambo mengine, kimejibainisha ni moja ya vituo vimavyotanguliza mbele Maslahi ya Taifa kwa kutangaza live mambo yenye Maslahi kwa taifa.

Radio Times FM ndani vipindi vyake mbalimbali, imeanzisha segment mpya iitwayo, "Zaidi ya Kawaida". Kwenye segment hiyo, wanawaalika Watangazaji, ma dj au wasanii wa zamani kwenda kutoa uzoefu wa enzi zao kwa kilinganisha na sasa, kisha wanawapa fursa za kutoa somo lolote kuhusu uzoefu wao.

Leo mimi ni miongoni mwa waalikwa wa leo na nikaanza kwa kujikumbusha enzi zangu za utangazaji wa redio ambao nilianzia RTD miaka ya 90s, nikapigiwa miziki ya zamani ukiwemo wimbo wa Georgina wa Marijani Rajabu na bendi ya Safari Trippers, nikapagawa na kujikuta ghafla nimerudia utangazaji wa redio na kulipuka. ..
Kwenye kutoa somo nimetoa somo linaloitwa Uzalendo na Rasilimali Zetu.

Nikasisitiza hatua alizochukua rais Magufuli kwenye sakata la mchanga wa dhahabu ni Uzalendo wa hali ya juu na anapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mzalendo wa kweli.

Japo Tanzania tumeingia mikataba na wawekezaji hao lakini mikataba yote huingiwa kwa hiyari na utekelezaji mkataba huo hutegemewa kutekelezwa kwa kitu kinachoitwa goodwill na good faith. Ukitokea upande mmoja unaiba na kufanya udanganyifu hii ni cheating, sio goodwill na haina goodfaith hivyo mkataba anaweza kuvunjwa na Tanzania kudai kulipwa fidia.

Unaweza kufuatilia hiyo mada hapa

Leo katika maisha Mseto ni zaidi ya Kawaida
LEO KATIKA MAISHA MSETO NI ZAIDI YA KAWAIDA
Created by ADAM KEFA on Fri, 06/02/2017
no comments
DBSxvVzUAAALEYD-559x520.jpg

kupitia vipindi mbalimbali leo katika redio ya 100.5 Times Fm utapata vitu tofauti tofauti ikiwemo kuwasikiliza watu mbalimbali ambao watakupa fursa mbalimbali katika kutambua mambo mengi .

maisha-800x450.jpg

Picha ya Pamoja ya watangazaji wa Times fm wakiwa na mtangazaji mkongwe wa zamani Pasca Mayala (katikati), wa kwanza kushoto ni Stanslaus Lambat,wa pili kushoto ni Dj-DSlash,wa kwanza kulia ni Dkt. Kumbuka na wapili kulia ni Fredrick mabula.

Leo katika kipindi cha [HASHTAG]#MaishaMseto[/HASHTAG] tumeungana na Mtangazaji mkongwe wa zamani Pasco Mayala ambaye ameweza kutujuza mengi licha ya kuwa na watangazaji wa kawaida wa 100.5 Times Fm Stanslaus Lambat na Dkt.Kumbuka.

Times Fm TZ - [HASHTAG]#ZaidiYaKawaida[/HASHTAG] hewani Pascal Mayalla ndani...

Paskali
Pascal Mayalla moja ya manguli.Nakumbuka ulivyokuwa ukikukuruka kule external service,na enzi zile ukitangaza kwa ung'eng'e unaonekana babu kubwa mjini
 
Mmmh kumbe kuwaalika watangazaji,ma dj na wasanii wa zamani kwenda Times fm kutoa uzoefu wa enzi zao ina maslahi kwa taifa?. Nilikuwa sijui mkuu asante kwa kunijuza,hongera ziende kwa times fm.
History is the study of the past in relations to the present, to determine the future.

Hivyo kuwaita ma nguli wa zamani just to share the experience, inakupa picha nzuri ya tulikotoka na kulinganisha na hapa tulipo ili kujua kule tuendako.

Paskali
 
Wew jamaa ungekuwa msukuma safi ungekuwa mkuu wa wilaya au mkoa...maana sio kwa kujipendekeza huko
 
Wanabodi

Tanzania tuna vituo vingi vya redio, kila kituo kina mambo yake na mchango wake kwa Taifa.

Miongoni mwa vituo hivyo ni kituo cha Radio Times FM inayopatikana 100.5 ambacho pamoja na mambo mengine, kimejibainisha ni moja ya vituo vimavyotanguliza mbele Maslahi ya Taifa kwa kutangaza live mambo yenye Maslahi kwa taifa.

Radio Times FM ndani vipindi vyake mbalimbali, imeanzisha segment mpya iitwayo, "Zaidi ya Kawaida". Kwenye segment hiyo, wanawaalika Watangazaji, ma dj au wasanii wa zamani kwenda kutoa uzoefu wa enzi zao kwa kilinganisha na sasa, kisha wanawapa fursa za kutoa somo lolote kuhusu uzoefu wao.

Leo mimi ni miongoni mwa waalikwa wa leo na nikaanza kwa kujikumbusha enzi zangu za utangazaji wa redio ambao nilianzia RTD miaka ya 90s, nikapigiwa miziki ya zamani ukiwemo wimbo wa Georgina wa Marijani Rajabu na bendi ya Safari Trippers, nikapagawa na kujikuta ghafla nimerudia utangazaji wa redio na kulipuka. ..
Kwenye kutoa somo nimetoa somo linaloitwa Uzalendo na Rasilimali Zetu.

Nikasisitiza hatua alizochukua rais Magufuli kwenye sakata la mchanga wa dhahabu ni Uzalendo wa hali ya juu na anapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mzalendo wa kweli.

Japo Tanzania tumeingia mikataba na wawekezaji hao lakini mikataba yote huingiwa kwa hiyari na utekelezaji mkataba huo hutegemewa kutekelezwa kwa kitu kinachoitwa goodwill na good faith. Ukitokea upande mmoja unaiba na kufanya udanganyifu hii ni cheating, sio goodwill na haina goodfaith hivyo mkataba anaweza kuvunjwa na Tanzania kudai kulipwa fidia.

Unaweza kufuatilia hiyo mada hapa

Leo katika maisha Mseto ni zaidi ya Kawaida
LEO KATIKA MAISHA MSETO NI ZAIDI YA KAWAIDA
Created by ADAM KEFA on Fri, 06/02/2017
no comments
DBSxvVzUAAALEYD-559x520.jpg

kupitia vipindi mbalimbali leo katika redio ya 100.5 Times Fm utapata vitu tofauti tofauti ikiwemo kuwasikiliza watu mbalimbali ambao watakupa fursa mbalimbali katika kutambua mambo mengi .

maisha-800x450.jpg

Picha ya Pamoja ya watangazaji wa Times fm wakiwa na mtangazaji mkongwe wa zamani Pasca Mayala (katikati), wa kwanza kushoto ni Stanslaus Lambat,wa pili kushoto ni Dj-DSlash,wa kwanza kulia ni Dkt. Kumbuka na wapili kulia ni Fredrick mabula.

Leo katika kipindi cha [HASHTAG]#MaishaMseto[/HASHTAG] tumeungana na Mtangazaji mkongwe wa zamani Pasco Mayala ambaye ameweza kutujuza mengi licha ya kuwa na watangazaji wa kawaida wa 100.5 Times Fm Stanslaus Lambat na Dkt.Kumbuka.

Times Fm TZ - [HASHTAG]#ZaidiYaKawaida[/HASHTAG] hewani Pascal Mayalla ndani...

Paskali
Radio inayosikika Dsm pekee hua inanikera sana na automatically inajishushia thamani!
 
Radio inayosikika Dsm pekee hua inanikera sana na automatically inajishushia thamani!
Wala usikereke, FM ni masafa mafupi, Hata kusikika Dar pekee pia ni pakubwa. Kulipaswa kuwe na Dar FM, Kino FM, Lala FM, TMK FM, UDSM FM, Ari FM. KAWE FM, Mwenge FM, Mbezi FM etc.

Kila shule, Kila Chuo, Kila kanisa, kila wilaya zote zinapaswa kuwa na FM zao.
Tembea uone! .

Kil
 
Pascal, this is very funny! Ulipotaja "watangazaji wakongwe wa RTD" kwa haraka nilifikiri ni watangazaji kama akina S.S. Mkamba, Chama Omari Matata, Erasto Mbwana, Jim Ndoe, Abdul Baker, Godfrey Mgodo, Steven Mlatie na Enock Ngombale (wengi wa hawa bado wako hai). Kumbe unazungumzia "kijana" aliyeanza kazi ya utangazaji miaka ya 90!

Ama kweli neno "mkongwe" ni relative kulingana na unapeleka ujumbe kwa nani. Na utakuwa sahihi kujiita "mkongwe" kwa kuchukulia labda kuwa wengi wa watumiaji wa JF na watangazaji wa radio hapa nchini ni vijana wenye umri wa chini ya miaka 30.

Hata hivyo kilicho dhahiri ni kwamba kipindi cha kati ya miaka ya 90 hadi sasa kipo katika zama tunazoziita za mageuzi (kisiasa na kiuchumi) na matumizi internet. Na waliofikia utu uzima katika kipindi hiki kwa ujumla wao wanaitwa wa kizazi cha "dot.com" (millennials). Hiki ndicho kipindi kilichoshuhudia uanzishwaji wa vituo binafsi vya radio na tv nchini pamoja na kuanza kwa vipindi vipya vya talk/talk-back live shows na kwa kiasi kikubwa upigaji muziki wa nchi za Magharibi au wa staili na ladha ya hizo nchi.

Pia ukiangalia watangazaji wengi wa radio na tv kwa sasa ni hawa hawa vijana millennials; tena wa "age group" moja (kama picha inavyoonyesha) kitu ambacho chenyewe ni tatizo katika kukuza ubora wa utangazaji na hivyo kupanua soko la wasikilizaji (target market/audience). Kungepaswa kuwepo pia watangazaji "wakongwe" wa kuwaongoza hasa ikizingatiwa kuwa vituo binafsi vya utangazaji havina utaratibu wa kuwaendeleza kimasomo (kitaaluma na kiujuzi).

Kwa vile ni dhahiri vituo karibu vyote vya radio na tv nchini (ukiondoa vya dini na TBC) havina sera na mkakati wa kimasoko (wa kuhakikisha soko lote la wasikilizaji - audience - nchini linalengwa), vituo vyote hivi vinajikuta vinalenga sehemu moja tu ya soko (market segment) la wasikizaji: vijana chini umri wa miaka 35, tena wale wenye elimu ndogo na hivyo uwelewa mdogo wa mambo na pia uwezo mdogo wa kiuchambuzi. Hili ni tatizo kubwa linalotakiwa kushughulikiwa haraka.

Haishangazi vipindi vingi vya hizi radio ni vya majadiliano (talk shows) na vimejikita kwenye porojo za vijiweni zisizo na kichwa wala mguu; mipasho na vijembe. Taarifa za habari zinalenga tu katika kutukuza wanasiasa na hakuna uchambuzi wowote wa maana wa habari unaofanyika. Kwenye burudani vituo vyote vinapiga muziki wa aina mbili tu: hip hop (Bongo Flavour) na taarab (rusha roho), kama kwamba hizi ndizo ladha pekee za muziki wanazopendelea wasikilizaji wote hapa nchini. Kwa wapenzi wa muziki tuseme, aina wa Raggae, Rumba, Jazz, Country, Zouk nk (ambao hapa nchini wako mamilioni), hawana lao!

Kiufupi ni kwamba "wakongwe' wanatakiwa kuingilia kati na kuokoa jahazi.
Mkuu umemaliza kila kitu,sihitaji kusoma comments zingine,umesemea yote ambayo yapo kichwani kwangu na jamii iliyostaarabika kwa ujumla
 
Nginana umemaliza kila kitu. Watangazaji wa leo nivijana wahuni tu wachache sana wanaojisimamia, matangazo yao nikwaajili ya kinda gaten na hasa sisi tusiojitambua, taarifa ya habari nikwaajili ya kuwatukuza watawala na muziki ni bongo freva na taarabu. Ukweli mimi nikijana tu lakini huwa inanibidi kusikiliza RTD kupata vipindi vya kijamii ingawa kwenye ile habari ya u ccm huwa hawanipati, samahani siitambui TBC Taifa bado naitambua RTD na ishalah siku tukipata rais mzarendo jina hili litarudi
 
kamati ya kwanza ni uchunguzi wa kitaalamu tuu. Kamati ya pili uchunguzi wa kiuchumi na kisheria.

Mtaalamu geologist anaweza kuona dhahabu ni nyingi kumbe kiuchumi sio economic viable kuuchenjua na kinachopatikana sio kingi kivile kama wataalamu walivyoeleza.

When we are well informed kuhusu kila kitu, tutakuwa kwenye a good position to decide na sio hizo peace meals.

Paskali
Mkuu lakini tayari mmesema ni wezi wakubwa wale! Na kwanini tusingekuwa na kamati moja ambayo ingehusisha geologists, wachumi na wanasheria ili ripoti yao iwe na maana zaidi? Leo ripoti ya Prof. Mruma imewaita ACACIA ni wezi, na wewe mwenyewe baada ya taarifa hiyo umewaita na unaendelea kuwaita ACACIA kuwa ni wezi wakubwa, je, ripoti ya kamati ya pili ikija na hizo unazoziita "sio economic viable" mtawabatiza jina jingine ACACIA badala ya hilo la "wezi wakubwa"?
 
Kwa mujibu wa Press Conference ya Acacia ya jana kule Uingereza tayari imeishaonyesha kamati ya pili tayari imekuwa compromised!.

Paskali.
 
Back
Top Bottom