Radio nyingine za Dini zifutwe kuitwa za dini-Ona hii

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,385
10,659
Siku moja nilitembelea Ifakara katika harakati zangu za kusaka noti. Sasa usiku wa saa nne nikawasha radio ya simu yangu nikakuta inakamata frequency za local radio, nikakuta wako na kipindi cha HURUMA YA MUNGU. Nikahubirika haswa!

Sasa kipindi hiki kiliisha majira ya saa 5. Hapo mtangazaji aliyejitambulisha kwa jina la Isdori alisikika akisema, " msikilizaji nakuacha na mrembo Zamaradi (kama sijasahau) akuletee kipindi cha mahaba...." acha sasa huyo Zamaradi aanze kusasambua matumizi ya shanga mwanaume na mwanamke wawapo kitandani!!! Mbaya zaidi aliyamwamwagula madude bila aibu mpaka nikaamua kuzima radio, maana upako wa huruma ya Mungu ulianza kunitoka na kuona mashetani ya ngono yakivamia chumba changu, mweeee!!

Jamani, radio za dini jitahidini basi kumtangaza huyo Mungu zaidi kuliko hayo malimwengu. Utakuta kipindi cha dini kinafuatiwa na nyimbo za taarabu za Mzee Yusufu, hivi hapo upako utabaki? Halafu watangazaji wenyewe adabu hakuna, lugha mnayoongea utadhani wanywa viroba, full kiswahili mbofu,mbofu. Igeni basi mfano wa Radio Maria ya Dar au Safina, na ile ya Sauti ya Injili.

Huyu Mungu hapendi michanganyo jamani. Utakuta radio asilimia 80 ni malimwenguuuuu, mambo ya dini kidogo tu. Hivi dini ni masikini kiasi hicho? Eti radio inakuwa na top 10 ya bongo fleva, manyimbo ya kusifia uzinifu tuuu ndo mnatupigia!!!hee, kwani Clouds, EFm na wengine hawatoshi? Mtadai eti inatafuta namna ya kujiendesha, hivi Mungu ni masikini kiasi hicho? Mbona wenzenu wanaweza?

Radio ya dini inayopiga taarabu HAIFAI KUITWA YA KIKRISTO!!!
 
Sasa Hili swala laki nimeliookea kwa masikikitiko makubwa Sana, naahid ntalishughulikia haraka sana
 
Dini na dunia kaka wengine hamu watoshelezi wake/waume zenu lazima mfundishe jinsi ya kuwapa raha na wao.
 
Hiyo redio Inaitwaje? Haina jina?

Maana redio za kidunia nyingi siku hizi zina vipindi vya dini, na wakimaliza wanaendelea na ratiba zingine.
 
Mi nilidhani Zamaladi kaongea udini..!! Hivi unadhani...'nyie wenye huruma ya Mungu'.. hamuhitaji tendo la ndoa kamilifu..!?
 
Ilikuwa ni usiku? Maandiko yanasema, nilipokuwa mtoto, naliongea kama mtoto. Ina maana mtu unapokuwa mtu mzima alafu ukawa unaongea mambo ya kitoto, lazima watu wakushangae. Hiyo inaitwa big talk. Inawafaa watu wenye mahusiano yao... Kama hakuhamasisha ngono bt alikuwa anawapa tuition wanandoa waweze kufurahia tunda, sidhani kama ni jambo baya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…