Q-NET Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?

Mbona ofisi zao zimejificha sana,haziko wazi kiasi kwamba huwezi jua kinachofanyika.Halafu unaoseminishwa unaambiwa usimwambie yyote hata awe mmeo/mkeo,why?
 
Mwenye swali lolote aulize kuhusu Qnet aende website au njoo inbox ntajibu.watu wanabadirisha maisha yao, wewe unabaki unatoa macho oh DECI...
Matapeli sana lugha zao,mimi kuna rafiki yagu aliniambia twende kwenye semina za UN nikashangaaa UN kienyeji enyeji tu kumbe ndo wanavyofundishwa kudanganya watu ili mtu ashtukie kaingizwa mkenge.
 
Tusidharau sana lbd waje watu waliofanikiwa kupitia Qnet watupe ushuhuda ili watu wawaamini.
Hakuna hata mmoja zaidi ya kutafuta watu na kuwajaza ujinga then na yeye atafundisha kujaza mwingine utumbo.....
The line and story continues......
 
Mimi nilibahatika kufika ofisi yao siku moja na kupewa lecture zao. Kwanza nilishangazwa sana na namna wanavyosalimiana kwa kusema kila muda goodmorning!

Pili wale watoa lecture wanatumia nguvu sana kulinda hoja kwamba QNet ni tofauti na pyramids nyingine zilizoliza watu.

Tatu hawataki kabisa upate elimu ya QNet kutoka kwa watu ambao siyo wahusika na mwisho nikaona kama uninga fulani yaani mnaimba na kuhamasishana as If ni imani ya kidini. Kifupi ni kama inafifisha matumizi ya akili katika kuamua na kujikuta unaishi kwa matumaini hewa.
 
Habarini ndugu zangu naimani wote mpo salama. Kama kichwa cha habari kinavyo sema. Kuna binadam kanifuata na kuniambia kuna fursa ya pesa fasta twende, mimi nami si nina taka nifanikiwe haraka!

Sikusita nika ongozana nae hadi mahali fulani kuna jengo kubwa sana nikakutana na watu kibao kila mtu yupo na afsa wake wana fundishwa jinsi ya kujiungaa na kampuni inaitwa Qnet.

Hawa jamaa wanasema, ili ufanikiwe au ili uwe mwana chama lazima ununue bighaa yao moja pili upeleke wanachama wawili kusudi nao wajiunge nahao pia wapeleke wao hivyo hivyo. Kwa hiyo nikipeleka mtu mmoja napata Doler 200.

Yani ndo utaratibu sasa sikuweza kuafiki moja kwa moja nikaona ngoja nilete hapa jukwaani kama kuna yeyote ambaye amesha fanya nao biashara atujuze hii fursa
.

 
qnet wazee wa good morning hata kama ni usiku..................
kimbia mkuu,usiangalie nyuma kimbia kama usain bolt........
 
Kuna hawa wanajiita bf suma nao sio jamii ya hawa network marketing kweli hawa
 
Wadau naomba kujua kiundan kuhusu qnet kama kuna yeyote yuko huko na kuna mabadiliko au ametajirika kuptia hyo ktu a share na mimi ktu maana dah ndugu yangu anaamin asilimia mia yan hatak hata nitafte kazi niwe qnet
 
Wadau naomba kujua kiundan kuhusu qnet kama kuna yeyote yuko huko na kuna mabadiliko au ametajirika kuptia hyo ktu a share na mimi ktu maana dah ndugu yangu anaamin asilimia mia yan hatak hata nitafte kazi niwe qnet
Ndugu hao ni matapeli tu! Bora hata ukauzemaandazi mtaaniutapata hela halali kuliko QNET
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…