- Feb 10, 2006
- 4,235
- 13,439
Wakuu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.
Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.
Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.
Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu