Kada Mzalendo
Member
- Oct 9, 2024
- 87
- 59
Mnamo tarehe 19 Novemba 2015, katibu mkuu mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na aliyekuwa mgombea urais, Dk. Willibrod Slaa, alitoa kauli kwamba “Chadema wanatekana,” akifichua siri nyingi kuhusu chama hicho.
Kauli ya Dk. Slaa inahusiana moja kwa moja na madai ya kutekwa kwa Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Aisha Machano, ambaye ameripotiwa kupigwa huko Kibiti.
Hata hivyo, tukio hilo limekuja katika mazingira yanayotia shaka, ikionesha hali ya vurugu na kuashiria uwezekano wa njama za kuibua taswira ya ukosefu wa usalama nchini.
Ni muhimu kujiuliza: Je, tunaweza kuamini kila jambo linalodaiwa na Chadema au kuna mchezo wa kisiasa wa kuipaka matope serikali yetu?
Madai haya yanazua maswali mengi sana, ikiwemo majukumu gani hasa aliyokuwa akiyatekeleza Aisha Machano Kibiti.
Hakuna maelezo ya wazi yanayoeleza sababu za uwepo wake eneo hilo, jambo linaloibua hisia kwamba kuna njama za kisiasa za kuhalalisha madai yao.
Soma Pia: Aisha Machano, Katibu mwenezi BAWACHA Taifa, alitekwa na kupigwa sana, ameokotwa porini akiwa na hali mbaya
Ndani ya Chadema, migogoro ya mara kwa mara imedhihirisha namna viongozi wanavyoshambuliana hadharani na kutoleana lugha za vitisho, ikiwemo vitisho vya kuuana na wakati mwingine kutekana kama alivyowahi kufichua Dk. Slaa.
Je, tunaweza kuwaamini Chadema wanapoishutumu serikali kwa kutekwa, wakati wao wenyewe wameshawahi kujihusisha na tuhuma hizo hadharani?
Tukio hili la kutekwa kwa Aisha limejiri siku tatu tu baada ya Bunge la Marekani kuidhinisha ufadhili kwa Tanzania, jambo linaloweza kuashiria kutoridhishwa kwa Chadema na mafanikio haya.
Hivyo basi, kwa kuzingatia yote haya, inawezekana hili ni jaribio jingine la kuchafua juhudi za serikali inayojitahidi kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na mahusiano ya kimataifa.
Ni muhimu kwa kila Mtanzania kuendelea kuungana, kulinda amani na kuhakikisha tunasonga mbele kama taifa imara, bila kuyumbishwa na michezo ya kisiasa isiyo na tija.