Profesa Ndakidemi aitaka serikali kununua bidhaa kutoka viwanda vya ndani

Ndagullachrles

Senior Member
Jun 20, 2023
123
135
MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini(ccm),Profesa Patrick Ndakidemi ameitaka serikali kutotumia mamilioni ya fedha kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi na badala yake wanunue bidhaa hizo kutoka kwenye vowanda vya hapa nchini.

Profesa Ndakidemi alikuwa akichangia kwenye bajeti ya wizara ya viwanda na biashara bungeni mjini Dodoma ambako wozara mbali mbali zinawasilisha bajeti zake kwa Mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema viwanda hivyo Vikiwamo vya bia,sementi,vioo,mabati vinatoa mchango mkubwa kwenye kuchangia Pato la Taifa hivyo serikali inaowajibu wa kuvisapoti kwa kununua bidhaa zake.

Profesa Ndakidemi alitoa mfano wa kiwanda cha kutengeneza dawa za kibaiolojia za viuadudu kilichopo Kibaha mkoani Pwani kilichojengwa kwa msaada wa serikali ya Cuba ambako serikali badala ya Kununua dawa kutoka kiwanda hicho imekuwa ikiangiza dawa za kuulia mbu kutoka nje ya nchi.

Alishauri seriikali kupitia wizara ya viwanda na biashara kuanzisha kongani za viwanda kwa kila kanda ili kurahisisha uchakataji wa mazao huku akitaka bajeti ya wizara hiyo kuongezwa zaidi.

"Mheshimiwa Naibu Spika nimpongeze sana mheshimiwa Rais kwa kuongeza bajeti ya wizara hii kutoka Bilioni 92.3 hadi Bilioni 110.3 lakini mheshimiwa bajeti hii bado ni ndogo,hii wizara inahitaji pesa nyingi siyo Bilioni 100 tu".

Alimpongeza Waziri mwenye dhamana na viwanda na biashara kwa kuanzisha jukwaa la kuzungumza na wafanyabiashara na kuzungumza nao na kusikiliza kero zao.

Alisema wafanyabiashara wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa kwenye masuala ya Kodi na ushuru ikiwamo ushuru wa bidhaa na ushuru na stika za stemp za kiielektroniki.

Profesa Ndakidemi pia aliitaka serikali kukiwezesha kifedha kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools (KMT)kilichopo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ili kiweze kujiendesha kwa ufanisi.

Alisema kiwanda hicho cha kutengeneza vyuma na ambacho kilitelekezwa kwa zaidi ya miaka 30 ,kinahitaji sh.Bilioni 3.46 kiasi ambacho alisema siyo kikubwa kama serikali ikiamua.

Alisema kiwanda hicho kilitoa msaada mkubwa kwa kiwanda cha sukari ya TPC baada ya mitambo yake kuungua ambako na kuokoa pesa nyingi baada kutengeneza vyuma kutoka kiwandani hapo.

Profesa Ndakidemi aliiomba serikali kukisaidia kiwanda cha kutengeneza MADAWA cha mjini Moshi pamoja na kiwanda cha kukoboa mpunga kilichopo Chekereni wilaya ya Moshi Vijijni kuvitafutia wawekezaji.
 
Hawa ndio viongozii wanaotakiwa ... pia ubora wa bidhaa za ndani wajitahidii uwe mzuri kwa bei rafiki asante
 
Back
Top Bottom