Profesa Maghembe, Sasa imetosha tuwape wanyama silaha wajilinde wenyewe

Mkuu unaongea point sana tatizo kubwa la nchi yetu mambo kupekeka kisiasa ile operation ilikua ina maana sana ila watu wakataka umaarufu wa kisiasa na Jeshi haliwezi kufanya kazi na wanasiasa Dawa ni moja tu tuwaruhusu Wanajeshi watulindie Mbuga zetu baas!
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%..Idara ya wanyamapori iwe chini ya Wizara ya Ulinzi.Raia wameshindwa kazi.
 
you-get1.jpg

Tumeshuhudia siku chache zilizopita mauaji ya kinyama ya rubani Capt. Roger yaliyofanywa na majangili .Ujangili nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla badala ya kupungua ndio kwanza unashika kasi,na kufikia hatua ya kutungua hata vyombo vya anga.
Raven-II-for-sale.jpg

Kitu kibaya zaidi majangili wameungana na magaidi.Ushauri wangu kwa Mh. Maghembe..kama tumeshindwa Kupambana na majangili basi ni wakati muafaka Tanzania ianze kuwapa mafunzo wanyama pori ,wajilinde wenyewe. Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kufundisha wanyama .Wengi tunaufahamu mradi wa panya wa kutegua mabomu.Mradi huu umesaidia sana katika nchi zilizo tumbukia katika vita na kubaki na maelfu ya mabomu ardhini.
Kama inavyoonekana katika picha ya nyani hapo juu aliepewa mafunzo ya kuwalinda nyani wenzie pamoja na faru dhidi ya maadui .. hususan binadamu..Tunaweza tukaanza na battalion moja ya nyani wenye IQ ya kushika mafunzo...kama nyani huyu wa South Africa aliepewa kazi ya kulinda faru na kampuni iliyompa mafunzo na kumuajiri... na sasa kampuni hii inalipwa fedha nyingi.
Yanabahati hayo majangili sio UKAWA, tungeyapelekea majeshi yote
 
kama soko la pembe za ndovu lataendelea kuwepo basi ujangiri hautaisha leo wala kesho.
Soko la pembe lilikuwepo toka enzi ya utumwa. Sasa limeongezeka. Wa China wamekuwa matajiri ..wananunua kila kitu. mpaka viongozi.
 
Naona mleta mada wakutrain wewe kwanza na wakupatie silaha. Una akili sana trust me utaweza tu
 
Njia ni moja tu hii wizara ikopewe kwenye wizara ya Ulinzi na JKT kwa mda alafu hawa jamaa waweke Deti huko Mbugani tuone kama kutakua na ujangili.
Ulishawahi kusikia habari ya ile gari ya jeshi iliyowahi kukamatwa na meno ya tembo?
 
Naona mleta mada wakutrain wewe kwanza na wakupatie silaha. Una akili sana trust me utaweza tu
Mi nilishakuwa trained mkuu. Usipime.
namuongelea huyu nyani.Kwa wale walio pass-out wakimuona jinsi huyu nyani alivyolala na kuji-position..na anavyoilenga na kui-ingiza target kwenye ''cross hairs'' watakuambia..huyu nyani ni hatari.
images
 
Wafuge na kuzalisha mbwa mwitu wingi kwani ni askari wazuri.
Mbwa mwitu wanashida moja..wana uchu sana na ni rahisi sana kunasa kwenye mitego .Wamasai wanajua.
na wanakinga dhaifu sana dhidi ya kichaa cha mbwa.
 
Basi ni kuwa lipo gari la jeshi Arusha lilikamatwa na shehena ya meno ya tembo nadhani ni mwaka jana au juzi. Hivyo kusema Wanajeshi walinde mbuga zetu bado litakuwa sio suluhisho labda kuwe na mkakati wa kidhamira wa ukweli
 
JW muda mwingi hawana kazi. Kiundwe kikosi maalum cha JW kwa ajili hiyo. Inakuwa kama vile hatuna askari? Shida
 
Basi ni kuwa lipo gari la jeshi Arusha lilikamatwa na shehena ya meno ya tembo nadhani ni mwaka jana au juzi. Hivyo kusema Wanajeshi walinde mbuga zetu bado litakuwa sio suluhisho labda kuwe na mkakati wa kidhamira wa ukweli
Kasoro hazikosekana popote pale. Ila jeshi litakapokabidhiwa jukumu hili rasmi..naamini hakanyagi mtu mbugani. Hifadhi zitapata ulinzi kama wa kambi za jeshi. Waulize wanaoikumbuka operesheni kipepeo.
 
Mkuu usidanganyike, kule DRC misitu ilipoonekana inateketea lilikabidhiwa jeshi lilinde rasilimali hiyo ili kutunza mazingira lakini hapo ndio biashara hiyo ikashamiri. Jeshi sio suluhisho, maana kwanza wale askari wanyamapori ndio wajuzi sana wa mambo ya porini kiasi kuwa wanaweza hata kumsoma mnyama mwenye hofu baada ya kukoswa koswa na jangiri na wakafuatilia. Kuwa mwanajeshi sio kujua mbinu za mbugani.
 
''Mkuu usidanganyike, kule DRC misitu ilipoonekana inateketea lilikabidhiwa jeshi lilinde rasilimali hiyo ili kutunza mazingira lakini hapo ndio biashara hiyo ikashamiri''

Mkuu DRC hakuna jeshi.Tolea mfano wa jeshi makini..please !
 
Back
Top Bottom