Profesa Kabudi jirekebishe udhaifu huu kabla haujafeli zaidi ya Mwakyembe

Kaazi kweli kweli.. Dawa ya Tundu lisu hiyo.. Huku Tulia huku Kabudi..Lisu anazikwa kabisa..lazima muanze kurusharusha vijembe vyenu.


Wanasiasa ndo wa kwanza kujigamba wakati hawana lolote..hata Muhongo walimfanyia figisu lakini awamu hii ya Magu ni hapa kazi tu.
Wakati ni jibu na mwalimu, IPO SIKU nyakati zitanena, huyu mnaempigia debe mala ameshaanza kutuambia tusidai dai katiba, bado kidogo tu atasema katiba haina maana, cheza na ulevi wewe?
 
huyu prof. huenda akajishushia heshima yake bungeni mbele ya lissu kwa hata ccm wenyewe wamechoooka mpaka basi pale bungeni kuendelea kuwa washangiliaji wa MADUDU YA AWAMU YA TANO!!!dawa ya palamagamba ni lissu kwani joh ******** alimpeleka tulia ili kumdhibiti Lissu lakini ameshindwa kapelekwa sasa Kabundi bila shaka haka kaprof kataomba poo kenyewe kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiquote misimamo yake kinzani juu ya utawala wa katiba na shera ambayo imekiukwa ktk awamo hii !!!
 
Ningependa kufahamu msimamo wake juu ya/kati ya katiba ya Warioba na ile Pendekezwa
 
Nilikua naskia tu kuhusu mtu kutokwa povu,kwa huyu prof.nimejionea yani anaonekana anapenda kuzogoana sanaaa
 
"We spoke when the law was law, and when the President was President." By Prof. Kabudi, 2017. Je, leo hii hatuna 'law' kwa maana yoyote ile? Je, leo hii hatuna 'president' kwa maana yoyote ile?

Ninaamini hii itaingia kwenye Hansard.
Hahaa..
Mkuu Prof alimaanisha wakati huo kulikuwa na sheria kali zifananazo na za mkoloni na sheria hata zile zisizo kali zilikuwa zinafanya kazi kwelikweli yaani zinafuatwa au zinatumiwa bila kusita, akatolea mfano sheria ya kuwekwa kizuizini. Kuhusu Raisi alimaanisha huyo mkuu alikuwa mkali sana na akisema kitu lazima kifanyike. Alikuwa mtu mwenye mamlaka makubwa mno kiasi kwamba aliogopwa na kila taasisi iliyopo nchini na kila mkazi wa nchi hii kwa wakati huo.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya ma-profesa wa kitanzania na maprofesa wa nchi za ulimwengu wa kwanza. Wa nchi za ulimwengu wa kwanza anakueleza jambo la kitaalamu kwa lugha nyepesi mpaka unaelewa jambo lenyewe kwa urahisi.
Hawa wa kwetu anatafuta lugha tata na ngumu ili umuone anajua kuliko wewe. Mfano mtu anaongelea "legal anthropology" kwa wabunge badala ya kueleza kwa lugha nyepesi kwa nini sheria za ndoa za watoto ni ngumu kubadilishwa. Halafu anaongea kwa jazba utadhani kuna kitu wanajaribu kuficha. Sijui tatizo la hawa wetu ni nini hasa?
Ni ulimbukeni wa kuona hakuna wasomi kama wao!
 
Kabudi kalewa madaraka hata mshahara wa kwanza hajapokea,je akianza kupata masurufu ya kazi yake si atawatemea makohozi huyu baba?.

Ha ha ha,naye atakuwa walewale tu,wachumia tumbo,
wanajifanyaga wanaharakati wakishapewa vyeo wanabadirika,

kiongozi mwenye msimamo hii nchi ni Seif sharif hamad,
kwani kakubali kuuacha umakamu wa rais kwa kusimamia anachokiamini,
hata Lisu nae naweza nikamuamini ,
Hukumwona siku ile anaapishwa alivyokuwa anamsujudia aliyemteua....kile kitendo ilikuwa ni red flag! Bongo tuna wasomi wachache sana wanaojiamini.
 
Mwalimu wangu wa part time wa Legal Anthropology
Huwa ananogewa kuongea mpaka anatokwa povu kwenye kingo za mdomo,ana kipawa sana cha kuongea na ni mtaalamu kweli wa const. Law

Ana "Academic Arrogance" ya Class A...wakati wa mchakato wa katiba alisema sio kila mwanasheria anajua "Constitutional Design" na "Constitutional draft"....Hizi ni taaluma za wao wachache.Kama walivyo madaktari,wanaujua mwili wa mtu juujuu lakini linapokuja suala na "specialization" kuna wengine wamebobea kwenye macho,meno,magonjwa ya watoto na kina mama n.k.

Hivyo si kila mwanasheria anajua namna katiba inapaswa kuwa.Prof akaenda mbali na kusema tatizo kwenye mvhakato wa katiba,wanasheria wasiokuwa na utaalamu wa Katiba ndio wanabwabwaja sana wakati ni weupe.

Nakumbuka Prof alisema mjinga hushangaa na kutoa nafasi ya kujifunza,lakini mpumbavu hushupaa na kuwa na kiburi,hulazimisha mambo na huwa mbabe...Waliounda Bunge la Katiba na kuikataa rasimu ya Warioba wanaweza kuwa kundi la pili,maana walishupaaa kuikataa rasimu bila kujua kilichopo ndani.
Kweli kabisa. Hao wa kundi la pili chini ya hayati 6 walibaki kujadili katiba na ndio mpaka leo hakuna katiba mpya na wengine bado wanaonesha ubashite wao hadharani
 
"We spoke when the law was law, and when the President was President." By Prof. Kabudi, 2017. Je, leo hii hatuna 'law' kwa maana yoyote ile? Je, leo hii hatuna 'president' kwa maana yoyote ile?

Ninaamini hii itaingia kwenye Hansard.
Mbona kama uchochezi? Hakuambiwa atengue kauli?!
 
"We spoke when the law was law, and when the President was President." By Prof. Kabudi, 2017. Je, leo hii hatuna 'law' kwa maana yoyote ile? Je, leo hii hatuna 'president' kwa maana yoyote ile?

Ninaamini hii itaingia kwenye Hansard.

Hata mi nilishangazwa na hiyo kauli. Huyu ni type ya Prof Mhongo.....ego kubwa kuliko uwezo.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya ma-profesa wa kitanzania na maprofesa wa nchi za ulimwengu wa kwanza. Wa nchi za ulimwengu wa kwanza anakueleza jambo la kitaalamu kwa lugha nyepesi mpaka unaelewa jambo lenyewe kwa urahisi. Hawa wa kwetu anatafuta lugha tata na ngumu ili umuone anajua kuliko wewe. Mfano mtu anaongelea "legal anthropology" kwa wabunge badala ya kueleza kwa lugha nyepesi kwa nini sheria za ndoa za watoto ni ngumu kubadilishwa. Halafu anaongea kwa jazba utadhani kuna kitu wanajaribu kuficha. Sijui tatizo la hawa wetu ni nini hasa?
Vipi kuhusu Prof Muhongo?
Prof Lipumba bingwa wa uchumi alipoasisi UKAWA na kuwaita Ccm maintarahamwe alipewa sifa lukuki.
Kazi IPO
 
Wanajamvi salaam!
Naomba Ku declare interest kuwa mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana waziri mpya wa katiba na sheria Profesa Palamagamba Kabudi. Licha ya hayo baada ya kuteuliwa kwenye nafasi yake ya uwaziri na kumsikiliza akiwa bungeni nimethibitisha mambo niliyokuwa nikiambiwa kumhusu Profesa huyu mkongwe kutoka kitivo cha sheria pale UDSM.

Profesa unatakiwa ujirekebishe unajiamini mno, unamajigambo na kujiona unajua kuliko mtu mwingine yeyote, na kama ukiendelea hivyo bunge na watanzania watakuchoka ndani ya muda mfupi na unaweza ukavurunda katika wizara hiyo zaidi ya Mawaziri waliokutangulia hususani Mwakyembe!

Ndugu wanajamvi simchukii Profesa Kabudi nina circumstantial evidence kuhusu nalolizungumza na ninaweka hapa scenario kadhaa kuthibitisha hoja yangu juu ya majigambo ya Profesa Kabudi.

1. Profesa Palamagamba Kabudi alifeli mara kadhaa mtihani wa bar exams ambao ilikuwa ni lazima mwanasheria aufanye ili awe wakili kipindi hicho kabla ya law school kuanzishwa. Baada ya kufeli mtihani huo wa bar exams mara kadhaa Profesa Kabudi alitoa maneno ya majigambo dhidi ya watahini wa bar exams ambao wengi wao walikuwa wanafunzi wake aliowahi kuwafundisha. Profesa Kabudi alidai kwamba yeye anajua zaidi yao hivyo wanamfelisha makusudi hivyo hata kama wanamfelisha wajue tu kwamba yeye anawazidi kila kitu na ni mwalimu wao. Baada ya majigambo hayo Profesa Kabudi alipewa uwakili wa viti maalumu kwenye sahani (honorary advocate).

2. Profesa Kabudi amesikika mara kadhaa akijigamba kwa wanafunzi wake kuhusu uwezo wa wanasheria wengine na hasa Tundu Lissu, huku akijisifu kuwa wanasheria wenye first class UDSM wapo wanne tu na wengine si kitu si chochote.

3. Profesa Kabudi aliwahi kujigamba na kumdharau Profesa Shivji kuwa hajui kitu kwenye maswala ya katiba hivyo akae kimya akaenda mbali zaidi na kusema wengine (akina shivji) wamesomea uprofesa wa sheria za ardhi wanajifanya waongeaji wa maswala ya katiba.

4. Profesa Kabudi aliwahi kudharau bunge maalumu la katiba na kuliita la Wapumbavu kwenye mchakato wa bunge la katiba huku akijiita yeye mjinga hivyo anaweza kuelimika.

5. Ushahidi mwingine ni jinsi Profesa huyu anavyojibu maswali bungeni kwa njia ya lecture akiwachukulia wabunge kama wanafunzi wa sheria huku akijionesha kama yeye ndiyo anajua sheria bunge zima.

6. Kitendo cha Profesa Kabudi kulidanganya bunge kwa kusema Uingereza haina katiba ni ishara sasa ameshadharau mhimili huo na watanzania wote. Utasemaje Uingereza haina katiba katika dunia ya sasa ya sheria katiba is not defined in that narrow sense anymore.

Wanajamvi Mheshimiwa Kabudi kama ataendelea kujigamba na kuwaona wengine si kitu atawachosha watu mapema na huenda akaiona kazi ya uwaziri kuwa ngumu zaidi anaweza kuvurunda kwani anaweza fika hatua asikubali ushauri. Profesa Kabudi zingatia taaluma heshimu wengine huna hati miliki ya sheria kuna wanasheria wengi wazuri wametulia usijione wewe ndiyo wewe ndani ya bunge na serikali. Kumbuka avumaye baharini papa kumbe wengine wapo, pia ajionaye amesimama aangalie asianguke

lazima utakuwa na mtindio wa akili, na kwa kifupi unakuwa mmoja wa wapumbavu au mpuuzi, au stupid ( ya kiswahili kikavu kavu)

huna hoja una wivu!! una attack personality............

1. hakusema haina katiba, alisema haina katiba ILIYOANDIKWA!!...mpuuzi wewe, RUDIA TENA ILE CLIP
2. kuhusu kudharau bunge la katiba, kama uliona CCM, CDM walichofanya bunge la katiba ilikua sawa kwa mstakabali wa nchi itabidi upimwe akili x 100. walikula 200bn ya watanzania and they ended up on discussing 2 or 3 governments onlly!!stupid!


mengine ni wivu, akijigamba, jigambe na wewe mbele yake

akikidharau na wewe mdharau mbele yake

kufeli bar exams is just an exams haimaanishi mtahiniw hajui, anye person can fail any exams kutegemea na intention ya mtoa mitihani/mtihani

kwa hiyo umejikunja weee a kuleta utumbo huu wa wivu??
 
Mwalimu wangu wa part time wa Legal Anthropology
Huwa ananogewa kuongea mpaka anatokwa povu kwenye kingo za mdomo,ana kipawa sana cha kuongea na ni mtaalamu kweli wa const. Law

Ana "Academic Arrogance" ya Class A...wakati wa mchakato wa katiba alisema sio kila mwanasheria anajua "Constitutional Design" na "Constitutional draft"....Hizi ni taaluma za wao wachache.Kama walivyo madaktari,wanaujua mwili wa mtu juujuu lakini linapokuja suala na "specialization" kuna wengine wamebobea kwenye macho,meno,magonjwa ya watoto na kina mama n.k.

Hivyo si kila mwanasheria anajua namna katiba inapaswa kuwa.Prof akaenda mbali na kusema tatizo kwenye mvhakato wa katiba,wanasheria wasiokuwa na utaalamu wa Katiba ndio wanabwabwaja sana wakati ni weupe.

Nakumbuka Prof alisema mjinga hushangaa na kutoa nafasi ya kujifunza,lakini mpumbavu hushupaa na kuwa na kiburi,hulazimisha mambo na huwa mbabe...Waliounda Bunge la Katiba na kuikataa rasimu ya Warioba wanaweza kuwa kundi la pili,maana walishupaaa kuikataa rasimu bila kujua kilichopo ndani.

Hizo sifa zote ulizozitaja hapo anazo pia Prof. SosiPeter Muhongo yaani naye ana Academic Arrogance ya class hiyohiyo A au labda A+
 
Juzi anasema bungeni "watu wakasome legal athropology" kuelewa kwanini sheria inayoruhusu watu kuoana wakiwa na miaka 14 ilitungwa na imekuwa ngumu kuifuta. Nilimuona mpumbafu sana kwa hiyo kauli yake. Ni sawasawa na kusema kila anayeuliza kwanini ajali ni nyingi nchini akasomee uaskari wa usalama barabarani.

Div 5 zimeondolewa siku hizi? I am afraid haukumuelewa

chuki hizi kila mara zitautesa wewe na kila mara utakuwa unaaibika
 
Zawadi umefanya vizuri, sio kumsema pembeni bali kumshauri wazi wazi. Naamini atapata nafasi ya kusikia na kutafakari ushauri wako
 
Tatizo maprofesor wengi ni usalama wa taifa hivyo wanakuwa hawana option ya kukataa hizo teuzi maana wanajua kabisa wanaenda kuharibu image yao, na watawala wetu wanawateua hawa maprofesor ili kuwahadaa wananchi kwamba waonekane kweli wako serious katika kutatua matatizo yao.
Umeongea point kubwa mkuu na kuna mambo nilikuwa sielewi nimepata majibu kwa hii comment yako
 
Back
Top Bottom