Profesa Assad ashtakiwe kwa kukiuka maadili akiwa ofisini. Alimpeleka dereva kufanya kazi masjala isiyoendana na proffession yake

Kama itakupendeza naomba CV ya Waziri wa Afya wa sasa
Hivyo vyeo vya kisiasa siingilii huko

Raisi unakuta anaitwa Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama wakati hajawahi kuwa mgambo au sungusungu au kukanyaga JKT
. Hili tatizo liko dunia nzima Raisi kuitwa amiri jeshi mkuu wakati hajui kurusha hata jiwe kurushia music

Vyeo vya kisiasa achana navyo havizingatii fani ukikuta nchi inazingatia fani ni moja kati ya mia
 
Dereva kama magari ya kuendesha hamna mnataka kusema akae tu angojee mshahara ?
Kazi yake kama haipo ni kama cheo kufutwa mpe chake apambane huko aendeko

Sheria za kazi ziko wazi kazi kama haipo mlipe chake muda kafanya kazi aende huko mbele ya safari usimpe kazi isiyo yake ashinde tu anasoma magazeti huku ukimplipa where is value for money?

Kazi ya HR na CEO awe wa private public au religious sector yeyote kazi yake mojawapo ni kuhakikisha value for money ya akipatacho slo tu kuwekana mjini at the expense ya taasisi or taxpayers au watoa sadaka au contributors
 
Nyie ni wafanyakazi wa kuajiriwa? Angalia job description ya mkataba wako wa ajira. Je haisemi utafanya kazi hizi, hizi, na point ya mwisho kusema ...na kazi yoyote nyingine utakayopangiwa na mwajiri wako? Sasa tatizo liko wapi?

Na je, inapotokea dereva hana kazi kwa sababu kuna madereva wengi, mnataka alipwe bila kufanya kazi, wakati labda kuna nafasi kwenye masijala ambayo haina mtu? Kwa sababu option inakuwa ni kumpunguza dereva arudi nyumbani au kumwambia kaa hapa masjala (bila kuathiri mshahara wake) hadi tukiwa na gari nyingine ya ziada, badala ya kuajiri mtu wa masijala wakati kuna mtu hana gari na ni dereva. Mmefikiria hilo au hamjui mambo ya HR management mnalaumu tu?
Kazi nyingjne zinazohusiana na proffesion yako udreva mpaka kupanga mafaili mbona ni kama mbingu na ardhi
 
What????? Unajua maana ya kuajiriwa kwa proffession yako?

Mfano yeye Assad ana leseni ya udereva huwa anaendesha gari zake

Kwa hiyo siku Raisi kaamka vibaya aseme kuanzia leo wewe sio CAG utakuwa kazi yako udereva kuendesha gari la bosi wa masjalq wa ofisi ya CAG

Unasikitisha.
 
Proffessor Assad akihojiwa amewahi sema alimpeleka dereva kwenda kufanya kazi masjala isiyoendana na proffession yake

Hayo yalikuwa matumizi mabaya ya madaraka na kinyume cha sheria za maadili za viongozi yanayozingatia proffession za mhusika dereva aburuzwe tume ya maadili na mahakamani hata kama kastaafu
Kwa mindset kama hii nani atawekeza Tanzania, hasa private sector? Ukimwajili Marketing Officer itabidi umwajili na dereva, mpika chai, mfagizi?

Kwenye Ofisi fulani nilikuta kuna TV, nilienda kwenye meeting, kwa saa moja na zaidi. Napoondoka nilishangaa wale watu bado wanaangalia TV. Jamaa nilimuuliza ofisi yenu ina huduma nzuri, kuna TV! Akajibu pale kuna madereva, wahudumu nk. Nilichoshangaa ofisi ina Mkurugenzi tu ndiyo boss kwa mapato na gharama gani? Kumbe ruzuku
 
Nyie ni wafanyakazi wa kuajiriwa? Angalia job description ya mkataba wako wa ajira. Je haisemi utafanya kazi hizi, hizi, na point ya mwisho kusema ...na kazi yoyote nyingine utakayopangiwa na mwajiri wako? Sasa tatizo liko wapi?

Na je, inapotokea dereva hana kazi kwa sababu kuna madereva wengi, mnataka alipwe bila kufanya kazi, wakati labda kuna nafasi kwenye masijala ambayo haina mtu? Kwa sababu option inakuwa ni kumpunguza dereva arudi nyumbani au kumwambia kaa hapa masjala (bila kuathiri mshahara wake) hadi tukiwa na gari nyingine ya ziada, badala ya kuajiri mtu wa masijala wakati kuna mtu hana gari na ni dereva. Mmefikiria hilo au hamjui mambo ya HR management mnalaumu tu?
Huyu atakuwa kwenye ripoti ya cag ana uchungu kuna siku yataripuka
 
Proffessor Assad akihojiwa amewahi sema alimpeleka dereva kwenda kufanya kazi masjala isiyoendana na proffession yake

Hayo yalikuwa matumizi mabaya ya madaraka na kinyume cha sheria za maadili za viongozi yanayozingatia proffession za mhusika dereva aburuzwe tume ya maadili na mahakamani hata kama kastaafu
Duh!!! Kwani lazima uanzishe thread????
 
Hata mimi nikishangaa, yeye kama mtaalamu, anawezaje kumpangia kazi ambayo muhusika hajasomea?

Nje ya usomi wake, pia ana ka namna fulani ka roho mbaya. Na inawezekana huyo jamaa alikuwa wa imani/dini tofauti, kwa hiyo akawa anachukia.

Ni yeye huwa anakomalia utawala wa sheria, utawala wa sheria ni pamoja na kufuata job description, kwa msingi kwamba mkataba wa kazi ni sheria iliyotungwa na wahusika, na inalindwa na sheria ya mikataba.

Sasa JPM angempa kazi ya kufanya usafi wa mazingira na vyoo pale ofisi ya CAG angekubali? Unavyotaka kutendewa, tendea wengine
Sio jambo la ajabu, hiyo ni inhouse training ama job rotation.
 
Nani wakumshtaki!Lakini ukisikiliza vizuri alifanya hivyo kwa private sector(Chuo cha Kislam Morogoro) Akiwa kama ndie kiongozi wao.Sasa ashtakiwe na nani?
 
What????? Unajua maana ya kuajiriwa kwa proffession yako?

Mfano yeye Assad ana leseni ya udereva huwa anaendesha gari zake

Kwa hiyo siku Raisi kaamka vibaya aseme kuanzia leo wewe sio CAG utakuwa kazi yako udereva kuendesha gari la bosi wa masjala wa ofisi ya CAG
Una uwezo mdogo sana wa kujenga hoja, unajenga hoja kama kilaza hali inayosababisha mtu kabla hajakujibu apoteze muda mwingi akupe elimu kwanza maana hauna knowledge ya unachobishania
 
Dereva kama magari ya kuendesha hamna mnataka kusema akae tu angojee mshahara ?

Profesa yuko sawa tu, dereva kwenda masijala iko sawa, tena qualification zinaingiliana.

Ofisi fulani mhudumu aliwahi kuwa dereva, kulikuwa na upungufu naye akawa na leseni wakampa test akafaa akawa reallocated.
Shida tuna uswahili sana.

Umeajiriwa, boss amekupangia majukumu mengine baada ya kuona ulipo kuepo mwanzo hakuna nafasi tena kwa muda huo, Ustaarabu ni kuamua kuacha kazi kama unaona haiendani na expectations zako au kuikubali.

Maamuzi yoyote utakayo chukua, utakua sahihi na boss wako alikua sahihi kwa wakati huo.
 
Back
Top Bottom