Kwamba siasa ni mchezo mchafu, nakubaliana na wewe na ndio maana I trust no politician... iwe ni wa upinzani au upande wa chama tawala!!Mkuu siasa ni mchezo mchafu. Kinachozungumzwa hadharani mara nyingi hakuuwakilishi usafi wa mtu kimaadili.
Kuna minong'ono kuwa yule mkuu wa kyela anataka kuachana na nafasi yake kwa sababu binafsi za kifamilia.
Ndio maana JPM ameona bora ampe ubunge Kabudi ili aende akairithi nafasi. Naamini hawezi kwenda kinyume na msimamo wa bosi wake kikazi.
Yapo mengi zaidi ya suala la serikali tatu, ambayo msomi huyu anaweza kuyafanya kwa faida ya Tanzania.
Kuhusu kwamba yapo mengi zaidi ya serikali 3; hilo la serikali 3 nimelitaja tu kwa sababu ndilo ambalo lilitofautisha watu mbalimbali kwa uwazi! Isitoshe, binafsi sio mfuasi wa serikali 3 kwahiyo hata akianza kuhubiri serikali 2 atakuwa tu anahubiri upande ambao mimi nauunga mkono! Lakini kama suala sensitive kama hili anaweza kubadilika, basi atakuwa ananipa mashaka ya kuogofya!