Prof. Ndalichako: Kiama kinakuja wanaotumia vyeti feki makazini

prof. ndalichako ni mnafki mbona ameenda kinyume na maneno yake? au hakujua kwamba wanasiasa hawaguswi
 
Hatukopeshi anaetetea vyet feki na yeye yumo la sivyo baba ake,mama ake,babu/bibi zake, shangaz/mjomba zake,Dada/kaka zake limewaptia fagio la chuma wapishe tupate na sis hzo nafasi
Pole sana mkuu kwa kusubiri kama herufi 'x' mi na ukoo wangu wote tuko safi mkuu hakuna mwenye feki si tunajituma.
Lakini unapotoa maoni ni lazima kuangalia jamii nzima nje ya familia na ukoo wako wataathirika vipi. Tusiwe wabinafsi, by the way uamuzi ulishapita na tushasahau haaaa
 
Wengine wanasafishwa mbona kwamba sifa ni kujua kkk. ila wanatumia vyeti vya wengine.
Mkuu, narudia tena kusema,

" hakuna namna yoyote ya kumsafisha mtu anayefoji Cheti, nasema waondolewe maana hamna namna nyingine. "

Haijalishi ni nani, ana status gani ama ana ukwasi kiasi gani.

Nafikiri umenielewa mkuu, Kadhi Mkuu 1:
 
Mtaalamu mwenye
Hili jambo litaleta imapct kubwa mno limefanywa kwa mkurupuko na mihemko waliopita waliliona lakini walijali hatma ya wataalamu wetu
Mtaalamu mwenye cheti feki
Acha kuzingua basi au yamekukuta.
Kiukweli hakuna mtaalamu mwenye cheti feki zaidi ya viongozi kama akina bashite tu na hawatakiwi
 
Ni upuuzi kama upuuz mwingine! maslahi ya wafanyakazi hasa walimu na madaraja mumeyaweka kwapan! Ni upuuzi mtupu!Hyu mama mpuuz tu kama wapuuzi wengine! Hana jpy na wabunge wanang'aa macho tu!
 
Kiukweli,elimu huwa ni ya mtu binafsi. Kila aliyeipata elimu anajua changamoto zake katika kuipata elimu ya ngazi yoyote. Elimu,hasa ya Tanzania,si ya lelemama. Kila anayeipata hujivuna kwakuwa anakuwa amevuka vikwazo lukuki na kuruka viunzi vya kutosha.

Katika hali hiyo,kwa sisi tuliopata elimu kihalali,hupata maumivu makali ya moyo na fikra kuona kuna matapeli na walaghai wa elimu. Tunakasirika na kuchukia kuona au kusikia matapeli wa vyeti vya elimu wakitumia na kutambia. Tapeli wa elimu kwa kuwa na elimu feki au cheti feki ni wa kupingwa na kupigwa vita kwelikweli. Ni tapeli hatari.

Ndiyo maana,mimi kama mtanzania mzalendo na mdau wa elimu,naunga mkono juhudi za Serikali na za watu binafsi kupambana na matapeli wa elimu wenye vyeti feki au elimu feki. Naunga mkono kwa moyo wote na nguvu zote. Utamu wa elimu ni kuitafuta na kuifaidi na kufaidika nayo katika kuitumia. Tapeli wa elimu apigwe vita popote alipo!
 
Serikali inaongelea swala la elimu majukwaani, kisiasa. Ni aibu kuwa na wabunge ambao wana elimu ya darasa la saba au chini. Neno kkk ndio kigezo cha wateule linaua elimu nchini.
 
Back
Top Bottom